n00b
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 1,013
- 2,684
Sumaye ameipiga kijembe serikali kwa kusema mlinzi na mtetezi wa katiba wa kwanza ni rais wa nchi akifuatiwa na viongozi wengine.
"Ndivyo wanavyoapa viapo vyao vya uaminifu kwa nchi. Kwa hiyo katiba nzuri lazima iambatane na serikali adilifu inayojali maslahi ya umma na rais anayeiongoza awe mchapakazi na anayejali maslahi ya umma mpana na siyo maslahi yake binafsi, ya watoto wake au ya marafiki zake.
"Yeye mwenyewe awe na uadilifu usiotiliwa mashaka ya aina yoyote na apigane vita vya wazi dhidi ya rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya na maovu mengineyo katika jamii. Tukifanikiwa katika yote hayo, basi tutakuwa tumevuna na kuyala matunda mema ya katiba nzuri."
Kayasema akiwa Mzumbe Campus - Mbeya