Sumaye: Rais ajaye apambane na madawa ya kulevya!

Sumaye: Rais ajaye apambane na madawa ya kulevya!

Sumaye chunga sana!hata kama ni haki yako Kikatiba utashangaa ukikatiwa mrija wako wa posho na stahiki!sijui utapiga kelele au utakimbia nchi?usichezee walioshika mpini!nakushauri tu maneno mazuri sana hayo lakini watawala hawatayapenda!watakusambaratisha!unaweza kuwa mzalendo mzuri sana ila tunakuonea huruma!wakijibu hao na wapambe wao itakuwa tabu!

Kwa nini unahubiri woga?

Natumai Sumaye amekuwa Waziri mkuu anajua zaidi nini kinaweza tokea !

Tatizo naloliona mimi ni kuwa kama assumption ama tuhuma si za kweli basi ni kosa kubwa ...ila kama ni kweli Fear Not.....Unatakiwa usiogope chochote zaidi ya kuogopa uwoga usikukumbe....
 
Sumaye ameipiga kijembe serikali kwa kusema mlinzi na mtetezi wa katiba wa kwanza ni rais wa nchi akifuatiwa na viongozi wengine.

"Ndivyo wanavyoapa viapo vyao vya uaminifu kwa nchi. Kwa hiyo katiba nzuri lazima iambatane na serikali adilifu inayojali maslahi ya umma na rais anayeiongoza awe mchapakazi na anayejali maslahi ya umma mpana na siyo maslahi yake binafsi, ya watoto wake au ya marafiki zake.

"Yeye mwenyewe awe na uadilifu usiotiliwa mashaka ya aina yoyote na apigane vita vya wazi dhidi ya rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya na maovu mengineyo katika jamii. Tukifanikiwa katika yote hayo, basi tutakuwa tumevuna na kuyala matunda mema ya katiba nzuri."

Kayasema akiwa Mzumbe Campus - Mbeya

Kwani rais Kikwete ameshindwa kutatua hayo matatizo?
 
Chadema wake up, make a blow;

CCM sasa hivi hoi!!

Mkuu usiwe na wasiwasi hiyo wake up pamoja na kutoa blow vinakuja. Wewe subiri swala la wauza madawa CDM wanakusanya data ambazo zitakuwa black and white ili hata waje na vyombo vya dola wasiambulie chochote. Tusubiri tu kwani data zitakamilika wakati wowote kuanzia sasa!
 
mabwimbwi taita wanapeta tu mjini kipindi hiki cha jk..my shout out to hon.idd azan
 
kwahiyo huyu Bwana mzaliwa wa Msoga vita ya dawa ya kulevya imemshinda kabisa !
 
Ni unafiki uliotopea mseme na huyu anayekuongoza hizo ni kampeni za kuusaka uraisi2015
 
Najua wote tunapenda kusikiliza na kuzungumzia ndoto za alinacha, Hakuna cha Sumaye wala Jk hapo, Je Sumaye kesha rudisha zile eka 600 alizopora Morogoro, na ukizungumzia madawa ya Kulevya na Ufisadi hapo CCM ndio wanaongoza na hakuna mpiganaji wa kweli kwa sababu uongozi wanapata kwa kutumia pesa ambazo Chanzo chake hakuna anayejua mtu hana biashara yo yote ya wazi ila kila anachangia hapa 100m, Kule 400m, pale 510, anabiashara gani na hizo pesa yeye atarudisha vipi Tuangaliye, ,,,,,!!! Tena sasa hivi ndio wanajitahidi kweli kweli wanataka kuteka Makanisa na Misikiti

'ustazi abudalah uyo mi chimo kabichaaaa...'
 
Haa haa, sumaye naye kwa usanii, hivi ndani ya ccm kuna asiye fisadi? Wanatofautiana viwango tu, rais wetu amekuwa msemaji kuliko hata msemaji wa ikulu, matendo ni 0.000%. Ccm ni janga kwa taifa letu!
 
kwani Sumaye yeye orodha hana? si aende kwa JK ampe tuone naye kama anajeuri ya kuwataja, kama kucha zake hazitaki ataje
 
Tatizo wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ndio wanaofadhili CCM hivyo ni ngumu sana serikali kupambana nao.
 
Ningemwona wa maana kama angesema wazi kuwa "kama Raisi ameshindwa kutekeleza kiapo alichokula cha uaminifu kwa Nchi ni bora akaachia ngazi kwa hiari yake"! Kwa hali ilivyo mbaya kutokana na biashara hii haramu hatuwezi kusubiria Raisi ajae, ni lazima hatua madhubuti zichukuliwe sasa! 2015 ni mbali sana na sifa ya Taifa itakuwa imepotea kabisa!

Mkuu aliyepo hakuna analoweza,hata wenzie hawana imani naye kabisa yaani wamekata tamaa,wanatamani aondoke hata kesho!!!
 
Jk ni kiongoz mzuri tatizo lipo kwa walio mwingiza ikulu kwa hela zao, wana kula matunda.....mme nisoma
 
Back
Top Bottom