Sumaye kupasua bomu...

Status
Not open for further replies.
How do you get good leaders if you don't rate them? After all we are " supposedly" living in a democracy, right?
Kwangu mimi EL was/is a good leader, crisis or no crisis.

sawa exercise your democratic right...ila ujue most good leaders "wanazaliwa" pale kunapokua na crisis ya aina yeyote katika muda wao. For me PM pinda is an obvious failure, Sumaye was about his script as a PM never wanted cheap popularity or attention, he was part of the team in a stable political environment of his time. EL ruthless-ambitious, self centered populist, who among fools was smart enough to use media to clear path for his presidential dreams and nothing more. He's even capable of creating artificial crisis just to aide his visibility in the media, a person who could hold his country for a ransom (without a presidency for me, nothing will ever be done in this state.)
 
sawa exercise your democratic right...ila ujue most good leaders "wanazaliwa" pale kunapokua na crisis ya aina yeyote katika muda wao. For me PM pinda is an obvious failure, Sumaye was about his script as a PM never wanted cheap popularity or attention, he was part of the team in a stable political environment of his time. EL ruthless-ambitious, self centered populist, who among fools was smart enough to use media to clear path for his presidential dreams and nothing more. He's even capable of creating artificial crisis just to aide his visibility in the media, a person who could hold his country for a ransom (without a presidency for me, nothing will ever be done in this state.)

Naona tunaelekea nje ya mada. Would you seriously give your vote to Sumaye for President? Why?Under what criteria? What has he done during his tenure as PM?
 
uchaguzi umekwisha ameshindwa kwa kura nyingi, hakuwa mbunge wa huko hanang, miaka 10 au kasoro alikua nje labda
na mwanzo alisema anapumzika siasa anataka kulima ana mashamba yake aliyotaifisha kule morogoro
sasa nini tena kina msibu ? angejipumzikia vyake amekuwa waziri mkuu pekee aliyekaa madarakani muda mrefu,miaka 10 si haba
na ukweli kugombea urais ajiangalie kwanza jee nakubalika ? jee sitakuwa mzigo kwa chama changu? je sina kashfa ambazo sasa hivi zipo kimya lakini once nikiwa mgombea zitafufuka na nitakosa majibu ?
sumaye kama kuna watu wake washauri wake wa siasa bora angeachana na ndoto ya urais ..si dhani kama anakubalika kiasi hicho,
b\na sidhani kama ana ubavu wa kumpiku Lowasa , ambaye pia japo yupo na nia yake ya kuomba urais lakini naye itakuwa ni mzigo kwa chama cha ke kuweza kumuuza
hivyo hawa watu bora wapime upepo.kumc
vikao vya chama vinaweza kuwapitisha kwa kutumia rungu la pesa lakini pia chama hicho kina turufu zake wanaweza kumchagua yoyote anaefaaa
rungu lilitumika na mwalimu kumkata kikwete dhidi ya mkapa ambaye ukweli ni kuwa mkapa alishindwa ila rungu lilitumika
hivyo kwa kulinda hadha ya chama hichi kina sumaye , lowasa , watazimwa na si kwa kuwaonea bali ukweli ni mzigo kwa ccm kwenye uchaguzi ujao
 
Sumaye, asiyekubali kushindwa si mshindani. kubali tu kwamba umeshindwa. waandishi wa habari hawatakusaidia kitu, jugular imeshakatwa no hope any more.
 
bagwell Mh. Simaye ana mgao wake wa keki inayomtosha maisha yake yote - 80% ya mshahara wa waziri aliye madarakani; aangalie mambo mengine ya kimaendeleo kama kutumia akiba zake kuibua miradi itakayoongeza ajira kwetu sisi walala hoi
tena 80% bila kazi anamzidi hata yule apateye 100% na huku anafanya kazi
 
sumaye hana jipya la kutuambia Watanzania. huyu jamaa wakati wa utawala wa Mkapa tulikuwa tunamwita "ziro" kumbuka kibonzo gazeti la mwananchi,si aina ya viongozi tunao wahitaji kwa sasa, amebahatika tu kupata madaraka makubwa asiyoyamudu

Tuna kumbukumbu kadha wa kadha za utendaji mbovu wakati akiwa waziri mkuu. pia tuna maswali magumu anatakiwa atujibu kabla ya kulipua bomu

1.uuzwaji wa nyumbaba za serikari
2.mikataba mibovu ya madini
3.ubinafsihaji wa mashirika ya umma usio na tija wa kama NBC bank, posta na simu nakadhalika
4.IPTL, SONGAS, AGRRECO
5.EPA
6.DEEP GREEN
7.KIWIRA
8.NET GROUP SOLUTION
7.RANCHI ZA TAIFA aliuza
8.MEREMETA

enyi waandishi wa habari acheni ushabiki muulizeni maswali magumu hapo juu, atuambie anapigania uongozi ndani ya chama chake ili iwe nini??? i hali amechangia kudumaza maendeleo ya nchi akiwa Waziri mkuu
 
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, leo
anatarajia kufanya kile alichoahidi mara baada ya
kuangushwa na Dk. Mary Nagu katika uchaguzi wa
kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC)
ya CCM, kupitia Wilaya ya Hanang. Habari kutoka kwa watu wa karibu na Sumaye,
zilisema kuwa Waziri Mkuu huyo wa zamani
anatarajia kuzungumza na vyombo vya habari
katika Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam leo,
kuanzia majira ya saa sita mchana. Kwa mujibu wa habari hizo, Sumaye amepanga
kueleza mwenendo mzima wa uchaguzi huo na
jinsi Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa
alivyoingiza mkono na kusababisha aangukie pua. Alipoulizwa nini hasa anataka kusema, Sumaye
alisema: “Ukiweza kuja, utasikia mwenyewe
nitakachozungumza.” Ingawa hakuna aliyeweza kutoboa siri ya nini
Sumaye anataka kuwaeleza Watanzania, lakini ni
dhahiri kwamba ameamua kujifunga bomu na
kujilipua kwa kueleza kile anachoamini njama za
kummaliza kisiasa anazodai kufanyiwa na
Lowassa. Siku chache zilizopita mara baada ya kushindwa
kwenye uchaguzi wa NEC, Sumaye alimtangazia
vita Lowassa. Sumaye ambaye hajatangaza rasmi kuwania kiti
cha urais, anatarajiwa kupasua jipu leo kueleza
kilichotokea Hanang na msimamo wake, na
kwamba yuko tayari kuwania urais mwaka 2015
endapo Lowassa atajitosa. Sumaye aliangushwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Nagu,
katika kuwania nafasi ya ujumbe wa NEC wilaya ya
Hanang, matokeo ambayo anaamini yana mkono
wa Lowassa. Pamoja na Sumaye kushindwa na Dk. Nagu kwa
zaidi ya kura 167, amepokea matokeo hayo kwa
shingo upande kwa kile alichoeleza kuwa ushindi
huo ni wa mafisadi. Inaelezwa kwamba tayari mwanasiasa huyo
amefanya mazungumzo na baadhi ya wanasiasa
wenye ushawishi wanaojipambanua kama
wapiganaji wa ufisadi ili kuunganisha nguvu kwa
ajili ya kukabiliana na kambi ya Lowassa. Mbali ya kundi la Sumaye na wanasiasa wengine
kuanza mkakati huo, wapo pia wanasiasa wenye
majina makubwa ndani ya chama, serikali na
wastaafu wanaotajwa kuingia kwenye muungano
huo. Akijibu tuhuma hizo kwa kifupi, Lowassa alisema
endapo Sumaye ataitisha mkutano na waandishi
wa habari na kutoa tuhuma hizo, nitajibu. Hata hivyo, baadhi ya wafuasi wa Sumaye na
watendaji wa ndani ya serikali wamesema
kuanguka kwa mwanasiasa huyo mkongwe katika
uchaguzi wa wilaya kunamuweka vizuri zaidi
kisiasa kutokana na mazingira tete ya kisiasa ndani
ya CCM, chama ambacho kimechokwa na umma. Uchaguzi huo ulifanyika siku chache baada ya CCM
kupitisha majina ya walioomba nafasi hizo huku
wanachama wengi wakienguliwa kutokana na
kukosa sifa katika kikao kilichomalizika mjini
Dodoma hivi karibuni. Wakati Sumaye akijipanga kupasua jipu leo, CCM
kwa upande wake inasubiri kwa hamu kumsikia
atakachosema. Tangu Sumaye alipodokeza kwamba atazungumza
na waandishi na kupasua jipu, baadhi ya viongozi
wa CCM wamekuwa wakifuatilia kwa makini siku
atakayozungumza na waandishi. Sumaye na Lowassa wanatajwa kuwa miongoni
mwa makada wanaofikiria kutaka kuwania urais
mwaka 2015.
Source:tanzania daima
 
Asije akafanya kama yule mbunge wa Nzega mtikisa kibiriti na mchumia tumbo mkuu Hamis Kigwangala, akatusubirisha kwa hamu halafu aseme amepata dharura Hanang hivyo ataongea siku nyingine, magamba hawaaminiki.
 
Always nasema Lowassa ni heavy weight sana na lina mbinu mujarabu sana..kushindana naye ni kazi kubwa sana
 
iki na oko na che na che aliyekula dona na ngulu wa kuchoma......... kasema do salale mpenzi kaondoka leo.....! huu mchezo wa kitoto!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom