salimkabora
JF-Expert Member
- Nov 10, 2012
- 2,441
- 653
Jamaa analia lia kweli sasa kama rais analia lia atawezaje kuongoza nchi
huyu jamaa amejidhalilisha sana,amekuwa icon ya unafiki na uchu wa madaraka,atajuta sana baada ya october
Pamoja na ushabiki wote wa kisiasa na kama unazijua siasa hasa za Tanzania, na dunia kote, huwezi kumtukana mtu kiasi hicho hasa mawaziri wakuu waliopita na binadamu yeyote katika medani za kisiasa vingnevyo unatumika na pia huna akili timamu, Tanzania ni nchi ya mfumo wa vyama vingi na hakuna aliyezaliwa kuwa mpinzani na walioko upinzani wote walikuwa na kadi za ccm chama chetu, kila mwanaccm ana haki ya kujiunga na upinzani kama anadhani anaweza kuwatetea watanzania na yy mwenyewe akiwa nje ya ccm au chama chochote cha upinzani na akiwa upinzani au ccm hawezi kusifia kule alikotoka kwani vingnevyo hakuwa na haja ya kutoka chama kimoja kwenda kingne na anayefanya hivyo watanzania wanasema amenunuliwa naahasimu wao.
Nadhan FS na wenzake wote upande wa upinzani wanahaki kwa kile wanachokisema imradi hawavunji sheria za nchi, na hata mpande wa chama chetu ccm wanasema na wanawasema wapinzani madhaifu yao, thats politics,washabiki,wapenzi wa vyama na wagombea tunatakiwa tuwe na akili zaidi ya wafanye siasa zaidi. Hakuna mwanasiasa ambaye sio mpenda madaraka na ni hulka ya kiumbe hai yeyote yule, binadamu anahitaji kutambuliwa,kuthaminiwa na kuwa maisha mazuri. Na siasa za Tanzania mwanasiasa ndo tajiri kuliko mhadhiri, daktari hata akiwa bingwa,uinginia na wataalamu wote hawana kitu ukilinganisha na mwanasiasa
Huwezi kutumia lugha chafu kiasi hicho kwa viongozi wakuu wa nchi hii hasa wastaafu hasa kwa mambo ambayo ni ya kisiasa.
Naamini hakuna binadamu yeyote yule asiyetaka madaraka yenye tija kwake, vingnevyo hata upande wetu wa ccm kusingekuwa na wagombea wa nafasi zote.
Kenda kuungana na wezi wenzie. Hayo ndo yaliitwa magamba sasa yamevuka na ccm imebaki safiii. ccm oyeeeeeeeeeeeee!
Miaka 53 gani niliodanganywa wakati ccm imeanza mwaka 1977 na mimi nimezaliwa 1980! sasa hata hesabu hujui unapelekwa tu kama ling'ombe! Lowasa out.....!
Sumaye arudishe mahekari ya ardhi kule mvomero na nyumba zaidi ya 5 alizonunua kwa bei ya kutupa, na atuambie miaka 10 Ya u PM wake alishindwaje kutukomboa maskini badala yake akapora mali na ardhi za wanyonge!?
Zuzu yule anayesinzia jukwaani na kutokwa udenda.
huna hoja full stop..badala yake unacheza mazingaombwe ya ukawa.
Hakuna kitu! mtatepeta tu! by the way na wewe Mmawia , unapata mgao wa Chaga Development Manifesto?
Tatizo la mtu mwenye mawazo finyu, huwa anadhani kikomo cha mawazo yake, ndio ufahamu wote uliopo. Sasa Nikuulize, umeelewa Nilichokiandika?
Mengi kulalamikia umasikini ni tofauti na hoja niliyoizungumzia hapo. Hao wanane ni mifano tu michache ya waliofanikiwa katika mfumo wa utawala wa CCM na Nimewataja kwa sababu wanajulikana na karibu kila mtu. Hata hivyo, ukiangalia kiuhalisia, kuna mamilioni ya watu walio na nafuu kubwa ya maisha hata kama si mamilionea, sasa wao waliwezaje kujikwamua katika mazingira hayohayo ambayo watu wanadai hayachochei mafanikio?
Haina uhusiano na hoja yangu kama vipi anzisha uzi wa kudai hizo pesa, mi namwambia huyu mwizi Sumaye arudishe ardhi za wanyonge.
Sumaye ni mzigo Kwa ukawa hajielewi yupo kimaslahi zaidi pale chadema
Kwa hiyo wote waliotajirika au kujikomboa kiuchumi ndani ya utawala wa CCM ni mafisadi walioneemeshwa na mfumo usio wa haki wa CCM? Kuwataja Mbowe na Mwenzie, Nilikusidia kumulika wale waliofanikiwa kupitia huo mfumo bila kuwa watawala ndani ya chama tawala lakini hapo hapo wanaupinga huo mfumo.
Pia kuna mamilioni ya watu ambao wako vizuri kiuchumi ambao wamekuza uchumi wao ndani ya huohuo mfumo.
Sijui unasemaje kuhusiana na hilo?
Akili ndogo haiwezi kuifundisha akili kubwa hata siku Moja. Una Elimu gani mwenzangu?
Kazi ya Serikali ni kutengeneza Sera ambazo zitanufaisha Wananchi.
Kwa Mfano Kenya maBenk yanakuja na mbinu mpya kila siku ya kuwakopesha fendha wakenya wakati hapa ukitaka kukopa uweke bank pesa kwanza miezi sita hadi mwaka tutaendelea kweli?
hauwezi kuwa Tajiri katikati ya dimbwi la Masikini haiwezekani.
Sijui wewe unafurahia pesa za wavija jasho zinavyoliwa na wachache kama vile Tegeta Escrow?
sijui unafurahia kwenda kilomita 7kwa masaa manne?
Sijui unafurahia kwenda Hospital ya Umma usikute Dawa?
Sijui unafurahia Kukosa umeme unapouhitaji?
Sijui unafurahia watoto kukaa chini shuleni?
Sijui unafurahia Mkulima kunyonywa mazao yake na kukopwa?
Una nafasi gani katika wanaowadhurumu watanzania mpaka unatetea hivyo?
Hadi leo analishwa na serikali, au hujui hilo?
Una tabia za kike kushupalia mambo.
hahahahaa Sumaye gani kama ni yule Mr ZERO usijidanganye kijana.....Suma na Edo ni Pwagu na Pwaguzi
Hakuna aliyekuza Uchumi kwa mfumo wa ccm wewe.
Vipi maana hueleweki kabisa.
Benja alimwaga Ngano ya Bakhressa hii ni.kukuza uchumi?
Ndio siasa hizo, unalialia nini sasa ye angekaa kimya watu wangemuheshimu sasa huu mpira unaitwa chandimu, pole.
Umeweka blah blah nyiiingi sana lakini ilichokusaidia ni kuanika mapungufu makubwa uliyonayo. Ndio maana mwanzoni Nilikueleza kuwa mtu mwenye ufinyu wa mawazo huwa anadhani kuwa kile anachokifahamu ndicho kila kitu. Hizo sentensi tano ulizoziandika ungezisummerise kwa neno moja tu, mfumo au mazingira.
Ndio maana basi, hata mwanzoni Nilihoji kuwa pamoja na yote unayodai kuhusu mfumo wa CCM, hao waliofanikiwa, waliweza vipi? Hilo ndilo swali la msingi hapa.