Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, amewataka wanachama wa CCM Mkoa wa Manyara kutobweteka kuwa wagombea wao watashinda bila kufanya kampeni na kujitokeza kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu.
Fredrick Sumaye, ambaye kwa sasa ndiye mratibu wa kampeni za uchaguzi za CCM mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Manyara, ametoa wito huo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za CCM Mkoa wa Manyara zilizofanyika katika viwanja vya Motel Papa mjini Babati.
Amesisitiza kila balozi wa nyumba anayetokana na chama hicho kuhamasisha wapiga kura katika eneo lake ili kukipa ushindi chama hicho, kwa kuwa katika ushindani wa kisiasa mshindi wa uchaguzi hutangazwa baada ya kura kuhesabiwa. Hivyo akasema ni muhimu wanachama wa CCM wakajitokeza kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu.

Halafu huyu naye slikuwa anausaka Urais. Mzee mzima anaendeleza Uchawa. Yaani Sumaye ni mtu wa kumnyenyekea Maza.... Sometimes ni kweli Watanzania hatunaga standards.