Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Waziri mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu Frederick Sumaye amerudisha fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani, Sumaye ana wapinzani wawili ambao ni John Gugunita ambaye alihamia CHADEMA kutoka CCM mwaka jana na Gango Kidera.
Nafasi zingine za uongozi ambazo zipo wazi ni ile ya makamu mwenyekiti ambapo watu watatu wamejitokeza kugombea nafasi hiyo akiwemo Saed Kubenea, nafasi ya mwekahazina wagombea watatu wamejitokeza akiwemo aliyekuwa naibu waziri wa kazi na ajira wa serikali ya awamu ya nne, Makongoro Mahanga.