Sumaye afanyiwa upasuaji wa bega MOI

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye,
anaendelea kufanyiwa mazoezi ya bega kwenye
Taasisi ya Mifupa Muhimbi (Moi), baada ya
kufanyiwa upasuaji hivi karibuni ameitaka
Serikali kuisaidia Hospitali ya Taifa Muhimbili ili
itoe huduma nzuri zaidi kwa wananchi. Sumaye ambaye alifanyiwa upasuaji baada ya
kuanguka na kusababishia maumivu upande wa
kushoto wa bega, alisema Serikali lazima itazame
Moi kwa upana zaidi, maana ndicho kituo pekee
wanachotegemea wananchi kwa huduma za
upasuaji na mifupa. “Hapa ndiyo tunategemea ili kupata huduma,
kwa hiyo Serikali lazima ipatazame vizuri kwa
kuweka miundo mbinu mizuri na kuongeza idadi
ya wataalamu ili kuondoa usumbufu,” alisema
Sumaye. Pia, Sumaye alisema idadi ya wagonjwa
katika hospitali hiyo imekuwa kubwa, hivyo hata huduma zimekuwa hafifu kwa upande
mwingine maana wataalamu wamekuwa
wadogo ukilinganisha na idadi ya wagonjwa.
“Unajua idadi inavyokuwa kubwa halafu
wataalamu wakawa wadogo hapo ndipo
huduma inapoonekana hafifu, kwa hiyo Serikali iongeze idadi ya wataalamu katika kituo hiki
ambacho kinahudumia Watanzania wengi,”
alisema Sumaye. Sumaye alisema suala la
viongozi wengi kwenda nje ya nchi kutibiwa,
inategemea huduma ambayo inahitajika kwa
kiongozi huyo kama inapatikana nchini. “Suala la viongozi kwenda nje ya nchi kutibiwa
inategemea na huduma ambayo unaitaka,
huwezi kwenda huko moja kwa moja bila
kupewa ruhusa na madaktari wa hapa,” alisema
Sumaye. Amekuwa akipata huduma ya mazoezi
ya bega taasisi ya Moi kwa zaidi ya mwezi sasa. Wakati huohuo, Kamati ya Bunge ya Huduma za
Jamii, imeitaka Serikali kuanzisha hospitali za
magonjwa ya mifupa kila mkoa, ili kupunguza
msongamano wa wagonjwa kwenye Taasisi ya
Mifupa Muhimbili (Moi). Mwenyekiti wa kamati
hiyo, Margreth Sitta, alisema wamesikitishwa na msongamano wa wagonjwa katika taasisi ya
Moi, unaofanya baadhi yao kulala sakafuni. "Kuna
haja Serikali kuangalia tatizo hili na kulitafutia
ufumbuzi harakati, hii ni shida," alisema Sitta. Sitta
alisema hayo wakati kamati hiyo ilipotembelea
taasisi hiyo na baadaye kuzungumza na wafanyakazi.
“Tumejionea wenyewe wagonjwa wanalala
chini, tatizo ni vitanda na wanahitaji huduma
kwa hiyo huwezi kumrudisha nyumbani ili
asubiri kitanda kwa hiyo lazima Serikali itazame
suala hili,” alisema. Mkuu wa Moi, Profesa Paul Mseru, alisema kitengo hicho kilianzishwa
mwaka 1996 kwa malengo ya kutoa huduma
kwa matatizo ya mifupa na upasuaji.
Pia, Profesa Mseru alisema kitengo hicho kina
zaidi ya vitanda 180, lakini kinapokea idadi
kubwa kupita uwezo wake, ndiyo maana wagonjwa wengine wanalala chini na kuomba
Serikali kujenga kitengo kingine cha mifupa.
“Tunaomba Serikali kufanya utaratibu wa kutoa
huduma ya upasuaji kwa mikoa mingine, ili
tupunguze msongamano ambao unajitokeza
hapa,” alisema Profesa Mseru. Sitta alisema lazima suala la kutoa huduma ya
mifupa na upasuaji kwa mikoa mingine lifanywe
haraka kutoa usumbufu kwa wagonjwa
wanaolala chini. “Kwakweli ombi hili lazima lifike
kwa Serikali na tutaomba ifanyie kazi haraka
suala hili, maana idadi ya wagonjwa inatisha na hatari pia kwa wagonjwa kulala chini,” alisema
Sitta. Wagonjwa ambao walikuwa wakisubiri
huduma, walisema kupata huduma ni vigumu
kwa sababu ya wingi wao ambao wanatoka
mikoa mbalimbali.
 
Back
Top Bottom