Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 778
- 691
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mfumo wa Fahamu Muhimbili (MOI) inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kisasa, ikiwemo ujenzi wa majengo mapya ya OPD, huduma kwa wagonjwa binafsi na wa kimataifa, tiba na utengamao pamoja na Kituo cha Ubingwa Bobezi katika Mfumo wa Fahamu.
Miradi hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa, kupunguza rufaa za wagonjwa nje ya nchi na kuiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa ya huduma za afya.