Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi Kavu (SUMATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani pamoja na Chama cha Wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani (lTABOA) imewataka madereva kusitisha mara moja mgomo wa mabasi ambao umetangazwa kufanyika siku ya kesho nchi nzima.
Kamanda wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani Fortunatus Musilimu amesema waliopanga kufanya mgomo waache kwani suala lao lipo mahakamani tayari.
"Niwaombe wote wanaosambaza vipeperushi vya kutangaza mgomo huo waache hili suala tayari lipo mahakamani na kuhusu hizo kero zinazungumzika hakuna sababu ya madereva kufanya mgomo utakaoleta kero kwa wananchi wasiona hatia" amesema.
"Tayari hatua za awali za kuwafuatilia wanaochochea mgomo huo zimeanza kuchukuliwa tunaamini kesho huduma ya usafiri zitatolewa tena zitatolewa kwa kiwango cha juu zaidi" ameeleza Kamanda Fortunatus Musilimu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa mabasi yaendayo Mikoani, Shabani Mdemu amesema kuwa, "Ni kweli vijana wametishia kugoma kesho lakini mimi kama kiongozi wao nimewaomba kusitisha mgomo huo naamini watanisikia,l. Ni kweli kuna tatizo Morogoro Sumatra tunaomba mfuatilie kama msipofuatilia hili tatizo vijana hawewezi kuvumilia hali hii"