SUMATRA yasitisha mabasi 14 ya Dar Express | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SUMATRA yasitisha mabasi 14 ya Dar Express

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by EMT, Nov 2, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imesitisha safari za mabasi 14 ya kampuni za Dar Express kutoa huduma kati ya Dar es Salaam- Arusha na Arusha-Tanga kuanzia kesho.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sumatra jana, mamlaka hiyo kupitia kifungu namba 15 cha Sheria ya Sumatra namba 9 ya mwaka 2001, imeiagiza Kampuni ya Dar Express kusitisha utoaji huduma kwa magari yake yote yanayotoa huduma ya usafiri kati ya Dar - Arusha na Arusha- Tanga kuanzia kesho.

  "Kutokana na kuwapo kwa matukio mengi ya ajali yaliyohusisha mabasi yanayomilikiwa na kampuni hiyo kwa kipindi kisichozidi miezi 10, mamlaka inatilia mashaka sifa za madereva wa mabasi ya Kampuni ya Dar Express," inaeleza taarifa hiyo. Pia, taarifa hiyo ilieleza kuwa imebainika Kampuni ya Dar Express imekiuka Kanuni namba 22 ya Kanuni za Ufundi na Usalama na Ubora wa Huduma kwa Magari ya Abiria za 2008.

  "Kuanzia Januari 2011 hadi sasa, mabasi ya Kampuni ya Dar Express yamehusika katika matukio ya ajali maeneo mbalimbali ambayo kampuni hiyo inatoa huduma za usafirishaji abiria. Matukio hayo ni kama lile la Januari 4, mwaka huu basi la Dar Express lilimgonga mpanda pikipiki na kusababisha kifo maeneo ya Kifaru- Mwanga, mkoani Kilimanjaro. Kwa mujibu wa taarifa za polisi chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi," ilieleza taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo inaeleza pia kuwa Septemba 22, mwaka huu, basi la Dar Express likitokea Arusha kwenda Tanga lilimgonga mtembea kwa miguu Ramadhani Hassan na kusababisha kifo eneo la Mkumbara - Mombo na Oktoba 24, basi jingine la kampuni hiyo liligonga gari jingine kwa nyuma kisha kuacha njia na kupinduka maeneo ya Kitumbi - Korogwe. Katika ajali hiyo watu tisa walijeruhiwa.

  Mwananchi
   
 2. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  aaah mbona mohamedi trans nayo ilisababisha ajali kibao afu bado inapeta road???????
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,181
  Trophy Points: 280
  Mohamed na Sumri ni magwiji wa hongo na rushwa ndio maana wao hawakumbwi na fagio la chuma.
   
 4. v

  valid statement JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  dar express tunaipenda sababu wamiliki wake hawatutoi abiria KAFARA. Ajali zote hapo juu ni mpita kwa miguu alofariki.
  Magari mengine, unasikia si chini ya abiria 16 walifariki.
   
 5. v

  valid statement JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  wakati mwengine unakuta hii ni mkakati wa kibiashara zaidi.
  Yani lengo lao ni kuwachafulia jina lao (dar express) kibiashara kwa watu, ili watu wasiyaamini tena haya magari.
  Mjini shule, SUMATRA kuhongwa na wamiliki wengine wa mabasi wafanye ivo hawashindwi.
   
 6. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #6
  Nov 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  siamini kama hizo ni sababu za kusitisha huduma labda sumatra watuambia sababu nyingine lakini siyo kama walivyoeleza
   
 7. v

  valid statement JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  mjini shule.... Chekecha!
   
 8. B

  Balozi Chriss Senior Member

  #8
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli sheria imewekwa kwa ajili ya kuadhibu makosa madogo madogo tu....Haya bana,kina Abood wanapeta,na lile kampuni maarufu la safari za Dar,Mbeya hadi Mapanda..
   
 9. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Hyo ni kazi ya mmiliki wa Kilimanjaro.
   
 10. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Du hawa Sumatra sasa balaa!kufungia mabasi unamuadhibu nani?mwenye gari au abiria?na ni kwa nini wamfungie leo na sio kipindi hicho alipopata hizo ajali?kuna kitu hapa
   
 11. M

  Makfuhi Senior Member

  #11
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kama Dar Express inastahili adhabu hiyo kwa kumgonga anayekunywa gongo asubuhi basi Abood, Mohamed, Sumry, Delux na wengineo wanatakiwa wafutiwe leseni. Sumatra wanatakiwa kutafakari na kuchukua hatua.
   
 12. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Naona sasa hizi sheria zinapindishwa pindishwa.
   
 13. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hawa Sumatra hawana akili hata kidogo hivi unataka kuniambia unaweza ukalinganisha mabasi ya Sumri,Mohamed trans na ma Benz ya Dar Express kweli wamekosa cha kufanya hawa kwanza ana huduma nzuri kuanzia mabasi yake yote ni Benzi hakuna youtong pale chinesse bus,ukiyaona yanapita mpaka unapata hamu ya kusafiri ni mabasi ya ukweli,ss kimsingi hawa Sumatra watoe record za ajili za hayo mabasi mengine tu compare harafu ss kama wananchi ndo tuamue kio kisa umeenda kuwaomba rushwa wamekataa ndo unawachafua!!!!!!!!!!
   
 14. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kweli nji hii haki hakuna, SUMATRA wanafungia mabasi 14 ya Dar express kutembea kwa ajali tatu na vifo viwili na ajali tatu kwa miezi kumi! Kama kweli SUMATRA wanaamini hatua hiyo ni sahhi watumwagie data za ajali kwa kila kampuni, idadi ya vifo na majeuhi kama hawajaaibika.
   
 15. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  YAMEBAKI MANGAPI yanayofanya kazi? au ndo wamefungia yote? high season hii ndo inaanza wachaga na kuhesabiwa sijui itakuwaje
   
 16. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Eti leo Sumry wanajiita Mbeya express!
   
 17. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Mhh kama dar exp wanafungiwa basi tanzania hakuna usafiri tena wa uhakika maana dar exp hana body za malori pia anajitahidi kuwa na gari mpya kila wakati, hivi karibuni katoa bus 8 za m benz za mwaka 2010 leo sumatra wanazifungia?sumry,mohammed trans,abood wanaua kila siku.halafu mnasema wazawa wawekeze,kivipi?
   
 18. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #18
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  WANA JF KWA TAKWIMU ZA UHAKIKA BODA BODA-PIKIPIKI KWA SASA ZINAUA WATU SI CHINI YA 10 kila siku.jee sumatra wanasemaje juu ya hilo?
   
 19. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #19
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Hii move ina ukweli wowote au ni kutafuta kula?
   
 20. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi natilia shaka uwezo na reasoning ya hawa watendaji wa SUMATRA hivyo napendekeza ifutwe.
  Haya ndo madhara ya kuwaweka waliokimbia maths katika nyazifa zinazohitaji uwezo mkubwa wa ku-reason ili kuja na sababu halisi na za msingi kwenye matukio yanayogusa watu wengi. Ivi ukitilia shaka jambo kinachofuata ni hukumu, kuna haja kweli nyie Sumatra kutuambia mnatilia shaka sifa za madereva wakati sifa za udereva ziko wazi?na kama ni walevi si mkawapime, au hizo gari zinaendeshwa na msukule so wanaoendesha hawajulikani wala hawaonekani? Acheni u....ga nyie Sumatra, hata hizo ajali mlizo-account zinavyoonyesha zinatokana na huo ubabaishaji wa Serikali kutojenga service road za waenda kwa miguu au waendesha baiskeli katika maeneo ya makazi ya watu ambapo barabara kuu zinapita.
   
Loading...