SUMATRA na ratiba mpya ya mabasi

SUMATRA na ratiba mpya ya mabasi

Wa nyamadyaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2013
Posts
1,178
Reaction score
529
SUMATRA imeanza kutoa ratiba mpya za mabasi ambapo ruti za mbali mf. Mwanza na Mbeya mabasi yatatakiwa kulala njiani na kuingia asubuhi kesho yake kama inavyonekana kwenye ratiba hapa chini.

Hatua hii inakuja ili kuthibiti mabasi kutembea usiku na kuingia mf, Mbeya saa nane usiku, kisha saa 12 asubuhi basi linageuza kurudi Mwanza.

Yapi maoni yako kuhusu hatua hii mpya?

1459338561590.jpg
 
Ni ufinyu wa mawazo,
wanaotoa hizo ratiba wanasafiri na kilimo kwanza 7 hours yuko mbeya. kwanza mie naona hata sheria za kutosafiri ucku ni upuuzi kabisa.
1. ni kwa nini mpaka leo hakuna dalili za kujenga highway
2. zamani arusha ilikuwa nenda rudi na magari ya zamani barabara za vumbi leo lami ZONGTONG na YUTONG BADO WALAZIMISHWA KWENDA MASAA 12 Upuuzi ni majipu hayo!!

Mie naona watu wachagye kama wataka la kulala njiani sawa kama wataka la one day trip sawa.
I.E Kulikuwa na bus la ALyys dar mwanza lilikua linaingia mwanza saa 12 na nusu
Musoma express linaingia musoma saa nne au tano!!

mbona bado ajali zatotokea?
gari ndogo je?
 
Labda na ajali pia zitapungua kwani mwendo utakuwa wa wastani,haraka ya nn wakati unafika siku ya pili
 
Ni ufinyu wa mawazo,
wanaotoa hizo ratiba wanasafiri na kilimo kwanza 7 hours yuko mbeya. kwanza mie naona hata sheria za kutosafiri ucku ni upuuzi kabisa.
1. ni kwa nini mpaka leo hakuna dalili za kujenga highway
2. zamani arusha ilikuwa nenda rudi na magari ya zamani barabara za vumbi leo lami ZONGTONG na YUTONG BADO WALAZIMISHWA KWENDA MASAA 12 Upuuzi ni majipu hayo!!

Mie naona watu wachagye kama wataka la kulala njiani sawa kama wataka la one day trip sawa.
I.E Kulikuwa na bus la ALyys dar mwanza lilikua linaingia mwanza saa 12 na nusu
Musoma express linaingia musoma saa nne au tano!!

mbona bado ajali zatotokea?
gari ndogo je?

Akili zako
 
Ni upuuzi tu, ushawahi sikia ajali za mabasi yanaouwa watu zinatokea usiku? Ni kuongezea garama abiria tu
ukisikia vituko ndio hivi, akili zetu kama za fundi seremala kila sehemu gonga msumari, isitoshe sababu za kuzuia magari yasitembee usiku ni za ajabu tu, fikiria unatoka Dar unaambiwa ulale misigiri kisa sekenke kuna majambazi yaani ka mlima kama kichuguu askari wameshindwa kuwadhibiti hao majambazi miaka ishirini sasa? tukiwa na misitu kama rwelu triangle itakuwaje?
 
Wanataka madereva wapate mda wakupumzika. sawa, lakini ingekuwa vizuri zaidi kama madereva wa safare ndefu wangekuwa wanapokezana
 
@SUMATRA wekeni utaratibu ambao ni rafiki zaidi. Mfano trip ya Mwanza-Mbeya. Simamieni dereva anaetoka na gari mwanza anabaki Dodoma kusubiri gari ya kampuni hiyo itakayopita hapo Dodoma kesho yake. Hili mkiliwekea mkazo linawezekana. Hivyohivyo, gari linalosafiri trip hivyo lisiruhusiwe kugeuza kesho yake. Kama sikosei trip ya Arusha-Mbeya enzi hizo, mabasi ya Hood yalikuwa yakipumzishwa.
 
Back
Top Bottom