SoC01 Suluhisho la tatizo la ajira kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Dr wa Kaliua

JF-Expert Member
Sep 20, 2020
1,636
3,806
Tatizo la ajira limekuwa Tatizo kubwa Sana katika nchini mbalimbali za bara la Africa, Tatizo hili ni matokeo ya mfumo wa elimu tulionao katika nchi yetu ya jamuhuri ya muungano Tanzania.

Tangu enzi na enzi mitaala ya Elimu, imekuwa ikifundisha wanafunzi ili waje kuajiliwa na sio kujiajiri.

Hapa ndio Tatizo la ukosefu wa ajira linapoanza, wanafunzi wengi husoma wakiwa na matumaini kuwa watakapo hitimu masomo yao, itakuwa mwanzo wa kupata ajira hivyo Basi kujiandaa kisaikolojia kuja kuwa watumishi Bora wa serikali na kusahau, uhalisia wa Tatizo la ajira katika jamii.

Hivyo Basi Tatizo la ajira lipo mikononi mwa vijana wenyewe, wengi wao hushindwa kujiongeza au kucheza nje ya boksi juu ya Fani mbali mbali wanazosoma.

Ni kweli kuwa baadhi ya Fani wanazosoma wanafunzi zinawaandaa kuajiriliwa rakini, Kama wanafunzi hao, watatumia maarifa husika itakuwa njia pekeee ya kupunguza Tatizo la ukosefu ajira NCHINI.

ZIFUATAZO ni njia, ambazo zinaweza kutumika na wanafunzi walio katika masomo, na walio hitimu masomo kujikwamua katika Tatizo la ukosefu wa ajira.

1. Kujiandaa kisaikolojia katika suala zima la kujiajiri.
Wanafunzi wengi wanapohitimu masomo yao, kisaikolojia huamini ndio wakati wao wa kuajiriliwa, hii ni kinyume na uhalisia wa Maisha ya mtaaani, hivyo Basi Jambo la kwanza wanalotakiwa kufanya ni kubadilisha akili zao katika mtazamo wa kuajiliwa mpaka kwenye mtazamo wa kujiajili. Hii itakuwa ni njia thabiti katika kupambana na changamoto hii ya ukosefu wa ajira. Nasema hivi nikiwa na maana kuwa ni hisia zetu na mitazamao yetu inayotufanya kufanikiwa au kutofanikiwa, hivyo Basi wanafunzi wanatakiwa kubadili akili zao na kuamini kuwa, wanasoma ili kujiajili na sio kuajiliwa.

Hii itakuwa njia ya kwanza kwa vijana Hawa kujiandaa na kujipanga kinagaubaga juu ya kukabiliana na Tatizo la ukosefu wa ajira, kwa sababu kila mtu alipo Leo hii ni matokeo ya fikra au mawazo yake au mtazamo alionao.

2. Kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazowazunguka wakati wa masomo.
Ni wazi kuwa, Kuna baadhi ya masomo wanayosoma wanafunzi yanachukua muda na kuwafanya wawe bize na Masomo pekee bila kuangalia na kutumia fursa mbalimbali zinazowazunguka.
Maana yangu ni Nini? Maana yangu ni kwamba wanafunzi wanatakiwa kujiingiza katika masuala ya uwekezaji angali wakiwa katika masomo kupita fedha ndogo ndogo wanazo zipata kutoka katika bodi ya Mikopo.
Fursa hizo za uwekezaji ni pamoja na zifuatazo.
A.uwekezaji katika hisa na na hati Fungani.
Kutokana na maendeleo ya sayansi na Teknolojia, Nafasi za uwekezaji zimekuwa rahisi sana, hivyo basi mwanafunzi anaweza kuwekeza taratibu taratibu kwa Muda mrefu na Baada ya muda kunufaika na kupata Faida au pesa ya kuanzia baishara kipindi watakapo hitimu masomo yao.

Mfano.
Makampuni mbalimbali, Kama CRDB, bank of Tanzania BOT na Mashirika mbalimbali ya uwekezaji yanaruhusu uwekezaji, kupitia hisa na hati Fungani. Nasema hivi nikiwa na maana kuwa utajari Mkubwa wa wafanya biashara upo katika uwekezaji wa hisa na hati Fungani.
Hivyo Basi huu ni muda wenu wanafunzi kuwekeza katika hisa na hati Fungani ili kuja kujikwamua kiuchumi.

3. Wanafunzi waanze kutumia taranta zao wakiwa vyuoni. ( Kuanzishwa kwa mashindano ya kusaka vipaji wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, chini ya wizara ya michezo na utamaduni)
Njia hii inaweza kuwa Bora Sana katika kukuza vipaji. Kwa upande wa serikali na wanafunzi wao Kama wao.
Mfano. Niwazi kuwa taranta ya mpira wa miguu ni ajira, na wanamichezo wengi mno wamefanikiwa na kua mamilionea kwa sababu ya michezo, hivyo Basi michezo ni ajira. Wanafunzi wanatakiwa kutumia vipaji vyao ipasavyo kujikwamua kiuchumi.

4.Kuandaa nakala na maandiko mbalimbali ya kimaendeleo na mipango ya Biashara, na kuhitaji utekelezaji uwezeshwaji kupitia vyuo au Taasisi wanazosoma.
Kutokana na Tatizo la ukosefu wa muda kujishugulisha na shughuli mbalimbali nje na Masomo, wanafunzi wanatakiwa kuandika changamoto na fursa na jinsi ya kuzitatua. Na kupeleka kwa wakuu wa vyuo ili kuleta utekelezaji ulio na mashiko na Faida kwao.
Mfano, wanafunzi mnaweza kuandika mpango biashara uliokamilika na kuiwakilisha kwa mkuu wa chuo ili awawezeshe katika UTEKELEZAJI kupitia mitaji,
Hii pia itakuwa njia Bora ya kutatua Tatizo la ukosefu wa ajira.

Wanafunzi wanaweza kujiweka katika makundi makundi ili kukuza ubunifu katika suala zima la kukuza ushindani.

5. Kumtanguliza Mungu
Kumcha Mungu, maana yake Ni kufanya Mema na kuacha mabaya, hivyo basi Kama mtu atakuwa mtenda Mema kila siku Kwenye maisha yake, Basi Mungu haweza kumtupa atampigania ili aweze kutimiza ndoto zake.
Hivyo vijana wanatakiwa kutenda Mema mbele ya Mungu.
Kwani Mungu hamtupi mja wake.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom