Suluhisho la kudumu la Muungano bora baina ya Tanganyika na Zanzibar

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
1,494
1,874
  1. Watu wa Tanganyika wenye makazi ya kudumu Zanzibar na Wazanzibar wenye makazi ya kudumu Tanganyika, wapewe uhiari, haki na uraia wa kuendelea kuishi Zanzibar au Tanganyika mtawalia.
  2. Endapo Tanganyika na Zanzibar zitaendelea kuwa na uraia wa nchi moja, basi nchi hizi mbili ziwe na makubaliano maalum ya uraia maalum wa nchi mbili (Duo Exclusive Treaty on Special Dual Citizenship) kwa Watanganyika na Wazanzibari ambao watahiari kuwa na uraia wa nchi mbili baina ya Tanganyika na Zanzibar pekee.
  3. Tanganyika na Zanzibar ziwe madola huru kama ilivyokuwa kabla ya muungano na zijiunge katika jumuiya au taasisi mbalimbali za kikanda au kimataifa ikiwa pamoja na Umoja wa Mataifa (UN), FIFA, nk.
  4. Pasiwepo viza ya kusafiria kati ya Tanganyika na Zanzibar isipokuwa vitambulisho vya uraia au hati za kusafiria (passports) zitumike kumtambua Mtanganyika au Mzanzibari.
  5. Iundwe Tume ya Mahusiano na Ujirani Mwema baina ya Tanganyika na Zanzibar (Commission for Relations and Good Neighbourhood). Tume hii pamoja na mambo yatakayojitokeza, ifanye yafuatayo:
    • Kuweka utaratibu wa kuimarisha uhusiano na ulinzi wa pamoja wa Majeshi ya Ulinzi ya Watu wa Zanzibar (Zanzibar People’s Defence Forces - ZPDF) na Majeshi ya Ulinzi ya Watu wa Tanganyika (Tanganyika People’s Defence Forces -TPDF). Wanajeshi wa Tanganyika na Zanzibar wataendelea kutumika kwa pamoja kulinda watu na mipaka ya Tanganyika na Zanzibar.
    • Kugawana madeni ya nje kulingana na uwiano halisi wa jinsi yalivyotumika kusaidia nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar. Hii ni pamoja na mali zingine zozote za pamoja baina ya Tanganyika na Zanzibar.
    • Kuratibu balozi za nje ili ziendelee kutumiwa pamoja kiofisi (shared consulates) kwa Tanganyika na Zanzibar hadi wakati ambapo uwezo wa kila nchi utaruhusu kuwa na ubalozi wake.
    • Kuratibu fedha na/au sarafu za aina moja ili ziendelee kutumika kihalali kati ya Tanganyika na Zanzibar ili kudumisha uhusiano na utambulisho wa kihistoria.
    • Kuratibu mikutano ya pamoja na ya mara kwa ya kuimarisha ujirani mwema na undugu kati ya Rais wa Tanganyika na wa Zanzibar.
    • Kudumisha moyo na uzalendo wa kiafrika (Panafricanism)
Hitimisho

Nikiwa mwanafunzi mbobezi wa Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, nihitimishe kwa kusema alichokataza ni kufukuzana baina ya Watanganyika na Wazanzibari. Akaita dhambi kubwa sawa na kula nyama ya mtu. Hakukataza maelewano na makubaliano ya amani. Na sitegemei watu wanaokubaliana kwa amani watapigana. Wala si sahihi kulinganisha hilo na Sudan ambao walipigana miongo kadhaa wagawane nchi.

Wakati vita vya Uganda na Tanzania vikielekea ukingoni kabisa Mwalimu Nyerere alilaumiwa kuwa anataka kuimeza Uganda, wengine wakadiriki kusema kama alivyoimeza Zanzibar. Yeye alijibu kuwa lililo la msingi ni kudumisha amani na nchi jirani na kuwa na uhusiano mwema - si kuunganisha nchi. Tubakie majirani wema kama ilivyo kwa Zambia, Msumbiji, Rwanda, Kenya na kwingineko. Kuwa na mahusiano mema na jirani ni jambo la msingi na si lazima muunganishe nchi.

Kuna nchi nyingi tunahusiana nazo vizuri sana na kwa ukaribu japo haziko jirani, sembuse Zanzibar na Tanganyika! Undugu ni mahusiano mema si kuunganisha nchi. Na ujirani na udugu wa kihistoria upo kwa nchi zote tunazopakana nazo na si Tanganyika na Zanzibar pekee.

HAYO NI MAONI YANGU NILIYOYATOA MIAKA KADHAA ILIYOPITA. YATUNZWE!
 
Mpaka Siku mfumo wa muungano wa Uingereza, Scotland, Ireland & Iceland utakaporekebishwa ndipo na sisi tutarekebisha, kwa sasa ngoja uwe hivi hivi tuwanyoshe.
 
Weye ni Mzanzibari au Mtanganyika? Je, huoni kuwa na vitambulisho viwili ni kosa? Ukija bara uwe na cha bara kule Ngara huku ukienda Zanzibar uwe na cha kule Chukwa?
 
Pamoja na ukweli kuwa Muungano huu una utata mkubwa sana mpaka unalinganishwa na ukoloni (mtanganyika amemkalia kimabavu mzanzibari), mapendekezo yako siyo realistic.

Tutakapotengana tofauti zetu zitazidi kukua na mwishowe tutawekeana vizingiti na kuishia kuwa maadui milele.

Sababu kuu itakayosababisha kuchukiana zaidi ni tamaa za viongozi kutawala na kuwa na mamlaka bila bughudha. Kwa mfano simuoni rais wa Muungano awe CCM au CHADEMA atakayekubali kupoteza visiwa vya Zanzibar kirahisi rahisi hivyo.

Tamaa ya viongozi wa Tanganyika ni kama ya wayahudi ya kuyapora mamlaka yote ya Zanzibar kama wapalestina walivyoporwa.
 
Maoni mazuri sana, lakini kuagana kwa amani na upendo kamwe si kutengana. Ni kujenga uhusiano mpya kwa namna nyingine mpya. Ndiyo maana nimependekeza namna ya kuendeleza udugu na ujirani mwema.

Kuna faida nyingi za kitaifa na kimataifa kwetu sote, kwa Wazanzibar kuwa na nchi yao. Hakuna haja ya kuweka kauzibe kwa ndugu zetu wa karibu na wa damu. Ni fursa!

Kuungana kwa kinyogo na/au manung'uniko moyoni ni kubaki mmetengana huku mkijifariji kinafiki kuungana. Hata kwenye ndoa kuna watu hujifariji kuwa mwili mmoja na nyumba moja, lakini kiuhalisia hawana umoja. Hubaki wametengana mioyoni mwao na wengine huwaza hata kuua mwenzake wakiwa kitanda kimoja! Hata hivyo naheshimu sana maoni yako.
Pamoja na ukweli kuwa Muungano huu una utata mkubwa sana mpaka unalinganishwa na ukoloni (mtanganyika amemkalia kimabavu mzanzibari), mapendekezo yako siyo realistic.

Tutakapotengana tofauti zetu zitazidi kukua na mwishowe tutawekeana vizingiti na kuishia kuwa maadui milele.

Sababu kuu itakayosababisha kuchukiana zaidi ni tamaa za viongozi kutawala na kuwa na mamlaka bila bughudha. Kwa mfano simuoni rais wa Muungano awe CCM au CHADEMA atakayekubali kupoteza visiwa vya Zanzibar kirahisi rahisi hivyo.

Tamaa ya viongozi wa Tanganyika ni kama ya wayahudi ya kuyapora mamlaka yote ya Zanzibar kama wapalestina walivyoporwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Malalamiko ya aina hii huyasikii sasa hadi mama atakapotoka madarakani akaingia m-bara, Why?
 
Akili za ufipa,hicho mnachotaka hakiwezi kutokea makubaliano yakuunganisha nchi yakishafanyika hakuna ruksa kubadili na viongozi huapa kuulinda muungano kwahiyo hizo ngonjera pelekeni kwingine.
 
Back
Top Bottom