Suluhisho la Kiingereza Shule za Sekondari

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,595
Kwa utafiti nilioufanya ni kuwa sababu mojawapo ya kufeli kwa wanafunzi shule za sekondari ni Lugha ya kufundishia yaani kingereza. Nyingine ni malipo duni kwa waalimu,mazingira magumu ya kufundushia, mitaala kubasilishwa bila maandalizi pia maadili.
Tuanze na lugha ya kufundishia; Nashauri shule zinapofunguliwa kwa kidato cha kwanza itumike miezi miwili ya mwanzo itumike kwa kufundishia somo moja tuu LA KIINGEREZA, hii itampa mwanafunzi mwanga wa kuelewa lugha ya kingereza tofauti na kuanza kufundusha masimo mengine wakati mwanafunzi hana msingi wa lugha husika!
Hii itampa uhueni mwalimu kufundishia maana inafika wakati unafundisha mwanafunzi anauliza " Mwalimu "The' INA maana gani? What maana yake nini? neno "From" lina maana gani?
Kama wewe ni mwalimu maswali kama haya yanapoteza mood ya kufundisha! hapa mwalimu huishia kwa kuwaambia wanafunzi ' wakariri kuelewa ni baadae!

RATIBA
Asubuhi kipindi cha kwanza kiwe English
Cha pili kiwe English
kipind cha tatu kiwe English
Kipindi cha NNE kiwe ni Mrudio ya siku nzima.
Siku ya Ijumaa iwe ni siku ya Test!

Ni matumaini yangu utaratibu huu ukitumika kwa miezi miwili( week 8) mwanafunzi itakuwa amepata mwanga wa somo la kiigereza na masomo mengine itakuwa rahusi kuelewa!
 
Watu wengine bana kwahiyo hujui alitaka kumaanisha nini? Soma hoja toa mawazo ili elimu ya watoto wetu iboreke

Sasa hao watoto ndio uwafundshe kwa mikanganyo hyo,ebu tulia mwambie andike upya tumfikishie muheshimiwa
 
Unajua kuwa hata walimu wengi pia hawakimudu Kiingereza sawasawa? Hao nao nani atawafundisha? Na ni nini kinakufanya uamini kuwa mwanafunzi aliyeshindwa kufahamu Kiingereza kwa miaka yote ya primary ataelewa kwa miezi miwili? Unajua cho chote kuhusu language acquisition? Unajua kuwa wanafunzi wanaofeli ndo tunawachukua na kuwafanya wawe waelimishaji wa taifa letu hasa primary ambacho ndicho kipindi cha muhimu sana kwa mtoto kumudu lugha sawasawa?
Tatizo letu la lugha ni kubwa mno na suluhisho lake siyo rahisi namna hiyo.

Suala hili limegeuzwa kuwa la kisiasa lakini kuna tafiti nyingi za kina zimeshafanyika na kuna mapendekezo mengi tu lakini wanasiasa hawataki kusikia. Naweza kukupa reference ukitaka kuhusu suala hili.
 
Nakubaliana na mtoa mada.Hapa haimanishi kujua Kingereza ni kupata mwanga wa Kingereza kidogo itasaidia kuboresha uelewa wa wanafunzi darasani au kupata japo nini kinaendelea hata km hawajui neno kwa neno!!
 
Tukubali tukatae muda wa kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia shule za msingi ulishapita.
Tuanzie hapo
 
Unajua kuwa hata walimu wengi pia hawakimudu Kiingereza sawasawa? Hao nao nani atawafundisha? Na ni nini kinakufanya uamini kuwa mwanafunzi aliyeshindwa kufahamu Kiingereza kwa miaka yote ya primary ataelewa kwa miezi miwili? Unajua cho chote kuhusu language acquisition? Unajua kuwa wanafunzi wanaofeli ndo tunawachukua na kuwafanya wawe waelimishaji wa taifa letu hasa primary ambacho ndicho kipindi cha muhimu sana kwa mtoto kumudu lugha sawasawa?
Tatizo letu la lugha ni kubwa mno na suluhisho lake siyo rahisi namna hiyo.

Suala hili limegeuzwa kuwa la kisiasa lakini kuna tafiti nyingi za kina zimeshafanyika na kuna mapendekezo mengi tu lakini wanasiasa hawataki kusikia. Naweza kukupa reference ukitaka kuhusu suala hili.

Hapa namzungumzia mwanafunzi anayefika form ONE For the first time anamwagiwa notes kibao za kingereza asome wakati haelewi kingereza hali inayompelekea kuishia kwenye kukariri tuu!
Endapo angepata msingi mzur wa lugha ya kingereza ingemsaidia
Ieleweke simaanishi miezi miwili mwanafunzi itakuwa kaelewa kingereza kwa uhakika ,hapana ila atapata mwanga mzur wa kukielewa!
 
Tukubali tukatae muda wa kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia shule za msingi ulishapita.
Tuanzie hapo

Nakubaliana na wewe ila wapi ambao ndo wanamaliza elimu ya msingi! tuanze na hao kuwapa msingi mzuri wa kiingereza !
 
Huu mkazo ungetiliwa huko Government Primary schools, sio secondary. unakuta form 1 karibu vitu vingi ni vile walivyosoma primary sema tu issue ni lugha that's why vinaonekana vipya kwa wale walotoka govt, ila hawa walotoka english medium wanapeta tu!
 
Mkuu mbona kuna orientation course kwa form one ambayo inachukua karibu miezi miwili. Ila nadhani kuna changamoto ya namna inavotekelezwa zaidi maana wakati mwingine hata walimu wenyewe ni shida wakati wa kufundisha hao watoto.
 
Hapo issue ni kutafuta utararibu wa kubadili lugha huko government primary schools watumie english as a language of instruction.
 
Kuna kitu mleta mada hukielewi japokuwa una lengo zuri sana. Kwa mfano.
1/Mwongozo wa kufundishia unaonyesha kuwa miezi miwili ya kwanza ya Form One anapaswa kufanya English Orientation Course, na hii huwa inafanyika kwa karibu kila sekondary japokuwa sio effective sana.

2/Sera ya Elimu iliyozinduliwa mwaka huu 2015 inasema Kiswahili ndio lugha ya msingi ya kufundishia kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu. Hivyo tegemea msisitizo utabaki kuwa kiswahili zaidi huko tuendako. Hili jambo liko nje ya Waziri unless ashawishi kubadilishwa kwa hiyo sera jambo ambalo ni risk kwake kisiasa.

3/Tatizo la Kiingereza hapa Tanzania ni kubwa ajabu, ni kubwa kupitiliza. Lina chanzo chake na utatuzi wake. Issue ni kuamua tu, bahati mbaya sana Watawala hawako interest kabisa kuhusu kulitatua.

4/Ukiona Mwalimu hapa Tanzania anaongea kiingereza vizuri na Fasaha basi ujue alisoma zamani sana, au mgeni kutoka nje(hasa Kenya) au alisomeshwa shule nzuri za English medium kuanzia Primary au ni mtu mwenye bidii ya juu sana katika kujiendeleza binafsi katika lugha ya Kiingereza. Katika mazingira hayo, wanafunzi wengi sana English kwao ni kitu cha kimuijiza hivi.
 
Mtoto anaanza kujijenga kifikira kuanzia chini-hapa duniani sijaona taifa ambalo ni watu wake ni wagunduzi na wenye maarifa ktk elementary level watoto wanafundishwa kwa lugha mama badaye tena wanabadilisha
jawabu ni kuwa na lugha 1 pekee toka chekechea mpaka university
 
Kuna kitu mleta mada hukielewi japokuwa una lengo zuri sana. Kwa mfano.
1/Mwongozo wa kufundishia unaonyesha kuwa miezi miwili ya kwanza ya Form One anapaswa kufanya English Orientation Course, na hii huwa inafanyika kwa karibu kila sekondary japokuwa sio effective sana.

2/Sera ya Elimu iliyozinduliwa mwaka huu 2015 inasema Kiswahili ndio lugha ya msingi ya kufundishia kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu. Hivyo tegemea msisitizo utabaki kuwa kiswahili zaidi huko tuendako. Hili jambo liko nje ya Waziri unless ashawishi kubadilishwa kwa hiyo sera jambo ambalo ni risk kwake kisiasa.

3/Tatizo la Kiingereza hapa Tanzania ni kubwa ajabu, ni kubwa kupitiliza. Lina chanzo chake na utatuzi wake. Issue ni kuamua tu, bahati mbaya sana Watawala hawako interest kabisa kuhusu kulitatua.

4/Ukiona Mwalimu hapa Tanzania anaongea kiingereza vizuri na Fasaha basi ujue alisoma zamani sana, au mgeni kutoka nje(hasa Kenya) au alisomeshwa shule nzuri za English medium kuanzia Primary au ni mtu mwenye bidii ya juu sana katika kujiendeleza binafsi katika lugha ya Kiingereza. Katika mazingira hayo, wanafunzi wengi sana English kwao ni kitu cha kimuijiza hivi.
Ni kweli kabisa Ndugu Zanzibar ASP.
 
Back
Top Bottom