Suluhisho la Kiingereza Shule za Sekondari

Suluhisho la Kiingereza Shule za Sekondari

Hapa namzungumzia mwanafunzi anayefika form ONE For the first time anamwagiwa notes kibao za kingereza asome wakati haelewi kingereza hali inayompelekea kuishia kwenye kukariri tuu!
Endapo angepata msingi mzur wa lugha ya kingereza ingemsaidia
Ieleweke simaanishi miezi miwili mwanafunzi itakuwa kaelewa kingereza kwa uhakika ,hapana ila atapata mwanga mzur wa kukielewa!

Mie napendekeza vitabu vya english form I and II vitafsiriwe kwa lugha na picha, std vi, std vii,form one na form two viwe na theory na practical vitasaidia sana...walimu wa english wawe special kama hatuna wabobezi kwenye lugha tuwanunue hata nje.

Nchi ya China wamefanya ivyo kwa kutoa walimu USA na UK.......
Nitarudi kuelezea nadharia ya theori na practical hapa.
 
Kiswahili ni lugha ya Taifa weweee

Kama ni hivyo hiyo biology,chemistry,maths na physics vitungiwe vitabu kwa kiswahili.vijana wengi wanakosa uelewa kutokana na lugha.shule ya msingi ni kiswahili.sekondary ni kiingereza.huu ni mkanganyiko?
 
upo sahihi kumwabzisha mwanafunzi lugha ya kiswahili halafu unabasilisha kuwa kingereza ni mkanganyiko mkubwa! bora tuwe na lugha ya kingereza toka shule ya msingi hadi chuo kikuu
 
upo sahihi kumwabzisha mwanafunzi lugha ya kiswahili halafu unabasilisha kuwa kingereza ni mkanganyiko mkubwa! bora tuwe na lugha ya kingereza toka shule ya msingi hadi chuo kikuu

Hapo poa sana kiongozi. Awali ja chuo kikuu iwe kiingereza tuendane na dunia ya leo. Ni ulimbukeni kuendekeza kiswahili ambayo watoto wetu hawawezi kushindaa katika soko la kimataifa
 
Tukubali tukatae muda wa kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia shule za msingi ulishapita.
Tuanzie hapo

Kiingereza si njia ya kujifunza. Shule zote zihamie Kiswahili kama lugha ya mafundisho haraka iwezekanavyo.

1. Tafiti zote zinaonyesha ya kwamba matokeo ya kujifunza ni bora kama watoto wanajifunza katika lugha wanayojua - hii si Kiingereza kwa Mtanzania.

2. Nchi nyingi duniani wanatumia lugha ya taifa kama lugha ya mafundisho, halafu wanajifunza Kiingereza (pia lugha nyingine za kigeni kama Kifaransa, Kirusi, Kihispania, Kilatini...) kama somo mojawapo. Waswidi, Wajerumani, Waitalia waliopita mfumo huu wanajua Kiingereza afadhali kushinda Watanzania wengi. Sababu? Walitangulia kujifunza "kazi ya kujifunza" na kujenga akili kwa lugha wanayojua, baadaye kujifunza lugha ya kigeni kutoka mwalimu aliye mwalimu wa lugha hiyo - si mwalimu wa hisabati au jiografia.

3. nchi kadhaa za Afrika hutumia lugha ya kikoloni pekee. Kwa jumla kiwango chao cha Kifaransa au Kiingereza ni afadhali kuliko TZ, lakini kwao naona hali ya jamii na siasa ni ngumu zaidi - maana hakuna lugha ya pamoja kati ya wasomi watawala na watu wa kawaida... nchi nyingi za Ulaya walitumia mfumo huohuo zamani (hasa wakitumia Kilatini) lakini waliacha karne ya 19 na kuhamia lugha za kienyeji. Matokeo yalikuwa bora hadi leo hii! (au unafikiri ni nini siri ya taifa lenye makabila 120 kuendelea kwa amani miaka 50+?)

4. Tanzania ilijaribu njia iliyo mbaya kushinda zote mbili: Kuanza miaka 7 kwa lugha ya kienyeji halafu kukimbia Kiingereza na matokeo ni mabaya mno.
Twende Kiswahili kwa masomo yote!
 
Hvi kuna MTU anaejifunza kitu anachokijua? Nadhani changamoto is exactly needed for someone to learn. By the way, kiswahili chenyewe si kirahisi kama wengi wanavyodhani. Kwani mitihani ya primary school yote si inatungwa kiswahili? Mbona hawapati 100% wanafeli tu kama mitihani ya kingereza? Watazungukaa wee ila ukweli utabaki palepale waondoe siasa kwenye elimu kwa kufanya uwekezaji wenye tija huku wakikumbuka Education is mother of all professionals
 
Hapo issue ni kutafuta utararibu wa kubadili lugha huko government primary schools watumie english as a language of instruction.

Nimekuwa nikiwaza hivi hivi kwamba serikali ibadilishe-na iamue kwa dhati kusema kwamba kiswahili sio lugha rasmi ya kufundishia mashuleni.mtoto kuanzia chekechea atasoma masomo yote wa lugha ya kingereza. Kwa kuwa vitabu na masomo mengi kuanzia sekondari hadi vyuo vikuu yameandikwa katika lugha ya kiingereza itasaidia kukuza uelewa wa watoto kuhusu masomo yao na sio kukariri na kushindwa kuwa wabunifu...
 
Last edited:
Huu mkazo ungetiliwa huko Government Primary schools, sio secondary. unakuta form 1 karibu vitu vingi ni vile walivyosoma primary sema tu issue ni lugha that's why vinaonekana vipya kwa wale walotoka govt, ila hawa walotoka english medium wanapeta tu!

hii pia itakuwa na madhara ya kuua shule za private na kusaidia watu kupeleka watoto wao nje ya nchi kukwea gharama kubwa za shule huku kwetu.mzee wa hapa kazi tu alisimamie
 
Nimekuwa nikiwaza hivi hivi kwamba serikali ibadilishe-na iamue kwa dhati kusema kwamba kiswahili sio lugha rasmi ya kufundishia mashuleni.mtoto kuanzia chekechea atasoma masomo yote wa lugha ya kingereza. Kwa kuwa vitabu na masomo mengi kuanzia sekondari hadi vyuo vikuu yameandikwa katika lugha ya kiingereza itasaidia kukuza uelewa wa watoto kuhusu masomo yao na sio kukariri na kushindwa kuwa wabunifu...
Hapo wakimaliza itabidi wasome Kiswahili course angalau kwa miezi minne hivi,tena baadae kiswahili kitapotea nchini!
Kwa mawazo yangu naona ni heri iwe kiswahili tu toka chekechea mpaka chuo kikuu tu ili tukithamanishe kiswahili chetu kama lugha tunayoikubali wenyewe
 
Kiingereza si njia ya kujifunza. Shule zote zihamie Kiswahili kama lugha ya mafundisho haraka iwezekanavyo.

1. Tafiti zote zinaonyesha ya kwamba matokeo ya kujifunza ni bora kama watoto wanajifunza katika lugha wanayojua - hii si Kiingereza kwa Mtanzania.

2. Nchi nyingi duniani wanatumia lugha ya taifa kama lugha ya mafundisho, halafu wanajifunza Kiingereza (pia lugha nyingine za kigeni kama Kifaransa, Kirusi, Kihispania, Kilatini...) kama somo mojawapo. Waswidi, Wajerumani, Waitalia waliopita mfumo huu wanajua Kiingereza afadhali kushinda Watanzania wengi. Sababu? Walitangulia kujifunza "kazi ya kujifunza" na kujenga akili kwa lugha wanayojua, baadaye kujifunza lugha ya kigeni kutoka mwalimu aliye mwalimu wa lugha hiyo - si mwalimu wa hisabati au jiografia.

3. nchi kadhaa za Afrika hutumia lugha ya kikoloni pekee. Kwa jumla kiwango chao cha Kifaransa au Kiingereza ni afadhali kuliko TZ, lakini kwao naona hali ya jamii na siasa ni ngumu zaidi - maana hakuna lugha ya pamoja kati ya wasomi watawala na watu wa kawaida... nchi nyingi za Ulaya walitumia mfumo huohuo zamani (hasa wakitumia Kilatini) lakini waliacha karne ya 19 na kuhamia lugha za kienyeji. Matokeo yalikuwa bora hadi leo hii! (au unafikiri ni nini siri ya taifa lenye makabila 120 kuendelea kwa amani miaka 50+?)

4. Tanzania ilijaribu njia iliyo mbaya kushinda zote mbili: Kuanza miaka 7 kwa lugha ya kienyeji halafu kukimbia Kiingereza na matokeo ni mabaya mno.
Twende Kiswahili kwa masomo yote!
Kwa lugha yetu hili ni la msingi sana kwanza kuiheshimu,kuithamini na kujivunia nayo pia,ila shida ni kwamba lugha ya kiswahili itakuwa na changamoto sana kupokea misamiati ya baadhi ya masomo hasa ya sayansi kwakuwa haina misamiati ya kutosha. Hii italazimu kugeuza maneno ya kisayansi ya kiingereza kusomeka kama yanavyotamkwa kwa kiingereza ilihali hayo maandishi yameandikwa kiswahili.
 
changamoto hizo unazozisema ndo maananikawa nimeshauri tutumie kiingereza toka awali. Kenya wanaongea kiswahili, lakini ufundishaji ni kiingereza, uganda vivyo hivyo---wataalamu mtanisaidia. Ikija kwenye ushindani wa ajira pia, hata watu wenu wenyewe mliowaweka kama wasiamamizi, na watawala-MDs na HRs wanapotafuta watu kuajiri wanaangalia wanaoweza kujieleza kwa umombo
 
Form one wana orientation course miezi miwili ya kujifunza lugha ya kiingereza ila sidhan kama ina msaada wowote mtu asome miaka 7 atoke kapa miezi mwili ndo imbadilishe? Msingi wa lugha ungeanza tangu primary schools wanafunzi wafundishwe kiingereza na sie walimu tupigwe brush teh
 
Bora wasome kiswahili tu mwanzo mwisho ili tunaojua hata good morning tubaki wachache...........................hii ndoto jmn
 
KAMA KUNA YEYOTE MWENYE SHIDA KWENYE FIZIKSI NA KEMIA,

TUWASILIANE FASTA HAPA.
 
Back
Top Bottom