Sukari Tsh 4000 watu kimyaaa

Sukari Tsh 4000 watu kimyaaa

Ni miezi miwili sasa bei ya sukari haikamatiki lakini watu kimyaa huku serikali iko bize kukamata wachochezi inasahau mfumko wa bei ni mchochezi hatari zaidi ya kina Lissu ,maisha yanazidi kuwa magumu mtaani.

me sujui bei ya sukari maana chai mapiga restaulant
 
Ni miezi miwili sasa bei ya sukari haikamatiki lakini watu kimyaa huku serikali iko bize kukamata wachochezi inasahau mfumko wa bei ni mchochezi hatari zaidi ya kina Lissu ,maisha yanazidi kuwa magumu mtaani.
Hapa ndipo nnapo waona Maadmini wa JF nao hawajielewi uzi kama hu ulitakiwa ufutwe mara moja maana ni uzi ambao una taharifa za uongo leo tu asubuhi nimetoka kununua kilo ya sukari kwa shillingi 2500 wewe unaishi wapi hadi uuziwe 4000 au labda unaishi Kibiti.

Nawaombeni maadmini huu uzi usiendelee kuwepo. Halafu jitu kama hili likitafuta na polisi kwa kosa la kutoa taharifa za kichochezi linasema linaonewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni miezi miwili sasa bei ya sukari haikamatiki lakini watu kimyaa huku serikali iko bize kukamata wachochezi inasahau mfumko wa bei ni mchochezi hatari zaidi ya kina Lissu ,maisha yanazidi kuwa magumu mtaani.
Tatizo unakoishi kuna tatizo la usafiri hivo mpaka kufika huko lazima gharama ipande
 
Tunaendelea kufa na tai shingoni kila mtu amekua mwoga. Media nayo imeparalize kabisa inaogopa kuliandika suala hili. Tumebaki na kazi moja tu ya kumsifia bwana mkubwa ilihali hali ya uchumi na huduma za kijamii inazidi kua mbaya kadri siku zinavyokwenda. Kuna fukuto linakuja Wilaya ya mbinga kuna vituo vya Afya zaidi ya 10 vinakwenda kufungwa hivi karibu wananchi wajiandae kuteseka kufuata huduma Mbinga mjini.
 
na ipande ifike elfu 10000 maana watu tumekua kama mazuzu na malofa .
 
Kwa upande wangu naona kama nchi imesimama vile..Vitu haviendi kila kona,vitu vinapanda bei kila kukicha,shilingi yetu inazidi kupoteza thamani kila siku,deni la taifa linaongezeka. Honestly,sijui tunaelekea wapi. Halafu watu wanapiga siasa uchwara eti aongezewe muda wa kutawala. Hatuko serious kabisa

Acheni uongo nyie. Hakuna kitu cha maana kilichopanda bei. Badala yake bei inashuka sana. Sasa hivi nyumba zilizokuwa zinauzwa zaidi ya milioni 200 unapata kwa milioni 50 hadi 40. Viwanja hata ukiwa na 1.5M utapata maeneo ya Chanika na Kigamboni. magari ya 15-13M unapata kwa 8-9M. Kwa upande wa chakula, bei ya mahindi maeneo ya Songea, Mbeya na Rukwa unapata gunia la kilo 100 kwa 30,000. Hiyo shilingi iliyopoteza thamani ni ya nchi gani?
 
Hata ikifika 10,000/= kwa kilo watanzania naowajua Mimi watanunua tu na hautasikia kelele zozote zile.
 
Bei ya Sukari inanyooshwa kwani kuna mafisadi walikuwa wamejificha nyuma ya sukari wakawa wanakwepa kulipa kodi ya sukari. Wananchi tuvumilie mambo mazuri hayataki haraka.
 
Hyo bei ya kwenu mkuu,hapa nilipo bei 2700,kama unapigwa kwa 4000 ni sawa tu maana wajinga mjini hawaishi
 
Back
Top Bottom