Sugu Awaka, Amwaga Cheche Bungeni!

Sugu Awaka, Amwaga Cheche Bungeni!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,188
Reaction score
128,908
Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu, leo amemwaga cheche bungeni kwa kuiwakia serikali kuhusu vurugu za wamachinga Mbeya hivyo kutaka tume huru iundwe ili kuchunguza kadhia hiyo.

Mhe. Mbilinyi ametoa cheche hizo bungeni mjini Dodoma wakati wa kujadili Tanzania kuridhia mkataba wa kimataifa wa haki za vijana wa Afrika.

kufuatia vurugu hizo, Sugu amesema mgambo walishindwa, polisi walishindwa, FFU walishindwa na jeshi pia lilishindwa, lakini wakazi wa Mbeya ndio wanaomjua ni nani alituliza vurugu zile!.

Sugu alisema kwa hasira kuwa kijana msukuma guta John Bosco aliuwawa kwa risasi huku diwani wa CCM akidai yeye ni nesi na siku hiyo alijuwa zamu, hakuna mtu yoyote aliyeumia wala kufariki!. Ametoa RIP kwa kijana huyo na kuomba matokeo ya tume tume yasisitize fidia kwa wahanga wa vurugu hizo!.

Sugu ameitaka serikali kutowanyanyasa tena machinga bali waachiwe kufanya shughuli zao kwa uhuru kama alivyofanya Satta wa Zambia mpaka hapo serikali itakapo wapatia utaratibu maalum.

Pongezi za dhati kwa Mhe. Sugu na pongezi kwa Chadema kutuingizia watu kama hawa Bungeni.
Pasco
 
Work experience ya miaka 3 imewekwa kwa ajili ya watoto maskini wakose kazi ili watoto wa vigogo wanaotoka chuoni wapate kazi bila usumbufu
 
Nadhani hata ccm na serikali yao wanalitambua kuwa pamoja na sera yao yakutumia nguvu ilishindikana yafaa bunge kumpa sugu pongezi kwakuweza kuzima vurugu hizo
 
anadai kamati ya vazi la taifa ni makini , hawezi kufanya uteuzi kwa kuangalia nani haelewani na waziri kivuli , kusaga na wengine ni makini viongozi wajenge tabia ya kusamehe
 
Jamani naomba kujuzwa hivi kati ya mh. Sugu na mh. Nchimbi kuna nini mbona wanapigana vijembe vya taarabu bungeni? Mpaka nimetamani hata kuzima tv.
 
Hivi clouds wana kitu kipi spesho kuhusu utamaduni wa tz kiasi cha serikali kuwatumia sana?!!ukigusia vazi la taifa clouds wamo,THT wamo,so what kuna nini nyuma ya pazia na ukiinanga clouds Nchimbi lazima atokwe povu!!!
 
Huyo jamaa nilimsikiliza kma dakika moja hivi nikaona anapiga kelele tu, hata kuongea hajui.

Dada yangu FF, kwani kwako Chadema wanajua kuongea?, wanaojua kuongea si ni CCM tuu?, Chadema wao si ni kupiga tuu kelele?.
Nchimbi katika majumuisho, amemkubali.

Kitu kimoja muhimu tukubaliane, sisi binadamu, sio tuu tunatofautiana uwezo wa kuelewa, bali pia tunatofautiana uwezo wa kiwango cha kusikia, wakati mwingine anasikia kikawaida kwa mwingine ni kelele kama ilivyo kulia na kucheka zote ni kelele!.
 
Huyu **** hajui anachoongea nan hajui ye na kusaga ni ma best? Maralia no more,tht,birthday ya raisi etc afu bado nchimbi anakuambia hana ushikaj na kusaga?
 
Nijuavyo mimi ni kwa sababu Mh Sugu na Joseph kusaga mmiliki wa Clouds FM ambae ndie analalamikiwa na Sugu kuwa amekuwa akiwanyonya wana muziki na pia amekumbati studio iliyotolewa na JK,sasa sugu na Joseph haziwivi.ila Nchimbi na Joseph ni maswaiba,sasa Sugu wakati anachangia alimchana live Nchimbi kuwa amechagua washikaji zake kwenye kamati ya vazi la taifa.hivyo Nchimbi alipopata chnce ndipo akaanza kumpiga vijembe.
Ila nchimbi hakupaswa kuanza kutetea juu ya kusaga kana kwamba watu hawajui kinachoendelea.
Nawasilisha
 
Pia amesema Nchimbi kaweka " washkaji" zake kwenye kamati ya vazi la taifa,hawana utaalam wowote
Wakati wa majumuisho, Nchimbi kaipangua hii hoja na kumopaka sana Sugu kuwa hawezi kuwateua watu makini eti tuu kwa sababu anajua fulani ana bifu na fulani. Pia akapaka hauwezekani ugomvi udumu zaidi ya miaka 10, ukishakuwa mbunge ni kiuongozi wa umma, hivyo sasa wewe ni kioo cha jamii, sahau yaliyopita songa mbele, haya ma bifu mpaka kuimbana na kutukanana matusi mpaka ya nguoni sio mambo!.
 
Dada yangu FF, kwani kwako Chadema wanajua kuongea?, wanaojua kuongea si ni CCM tuu?, Chadema wao si ni kupiga tuu kelele?.
Nchimbi katika majumuisho, amemkubali.

Kitu kimoja muhimu tukubaliane, sisi binadamu, sio tuu tunatofautiana uwezo wa kuelewa, bali pia tunatofautiana uwezo wa kiwango cha kusikia, wakati mwingine anasikia kikawaida kwa mwingine ni kelele kama ilivyo kulia na kucheka zote ni kelele!.
Sina cha kuongeza mkuu! kudos!
 
Back
Top Bottom