Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 918
- 1,994
View attachment 262836
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu amemshtaki aliyewahi kuwa mchumba wake Faiza Ally na aliyezaa naye mtoto kwa madai kuwa mwanamke huyo hana maadili na anahofia atamharibu mtoto wao. Sugu anataka kumchukua mtoto huyo na aishi naye (child custody).
Faiza ameiambia Bongo5 kuwa baada ya siku chache zilizopita kupandishwa kizimbani na kujibu shtaka hilo, alisema yeye hawezi kukubali kumuachia Sugu mtoto huyo kwa kuwa yupo chini ya umri.
"Kweli Sugu amenipeleka mahakamani kumtaka mtoto," amesema Faiza. "Mimi naona ni mtu anayekwepa majukumu kwa sababu chanzo cha yote nilikuwa namkata atulipie kodi ya nyumba, kwa sababu toka tuachane hajawahi kulipa kodi ya nyumba na siyo baba ambae anajali majukumu ya nyumbani kama inavyotakiwa."
"Kwahiyo nilivyoanza kumshauri kuhusu hilo akaniambia yeye anaweza kumchukua mtoto wake na mali zake anaweza kumlea mtoto wake. Sasa nilivyobishana naye kuhusu hilo wiki moja baadaye ndo likaja ili suala la KTMA ndio akalichukulia kama sababu ya kuweza kupeleka suala mahakamani kwa kudai sina maadili, kwahiyo nitammharibu mtoto. Kwahiyo kesho Jumanne ndio hakimu anatoa hukumu juu ya hili.
Lakini mtoto bado ni mdogo ana miaka miwili na kama miezi tisa bado mdogo anahitaji malezi yangu, pia hili suala nitalipeka ustawi wa jamii ili waangalie haki ya malezi ya mama kwa mtoto."
=======
Muendelezo: Maamuzi ya Mahakama kuhusu kesi aliyoifungua Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu' dhidi ya mkewe wa zamani
Ni habari ambayo imeandikwa na gazeti ya Mwananchi June 23 2015 ikitokea Mahakamani Manzese Dar es salaam kuhusu kesi iliyokua imefunguliwa na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi kuhusu mke wake wa zamani.
Taarifa inasema Mahakama ya Manzese imeamuru Mbunge Joseph Mbilinyi akabidhiwe mtoto wao kutokana na kesi aliyoifungua dhidi ya mke wake huyu akidai anamuharibu mtoto.
Hii habari imekuja siku kadhaa tu baada ya TUZO ZA KILI 2015 ambapo mke huyu wa zamani aliingia kwenye headlines kutokana na vazi alilokuwa amevaa.
=======
Muendelezo: Alichosema mama wa mtoto wa mhe. Sugu baada ya maamuzi ya mahakama
Mahakama ya Sinza Mori imetoa hukumu ya hatma ya mtoto wa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na mama wa mtoto wake Faiza kwa kuruhusu mtoto huyo kulelewa na baba yake kwa madai kuwa mama hana vigezo vya kumlea mtoto huyo kimaadili.
Uheard ilipata nafasi ya kuongea na Faiza baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo huku akiwa na huzuni kubwa alisema hajatendewa haki na kudai Mheshimiwa Sugu amekua si baba bora kwa mwanae kwani aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuombwa kodi ya nyumba, mlevi sana pia amekua na safari nyingi hivyo hawezi kumuhudumia mtoto wao.
Ameongeza kuwa pamoja na lawama ambazo amepewa kuhusu mavazi yake amedai yuko tayari kujirekebisha lakini si kuchukuliwa kwa mtoto wake ambaye ana miaka miwili kwa kuwa amekua akimuhudumia na kumpa kila ambacho mtoto anastahili kupewa.
===========
Muendelezo: Baada ya Sugu Kushinda Kesi,Faiza Asema Bora Kufa Kuliko Kumuona Sasha Akilelewa na Mama Mwingine
Baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu' kushinda kesi mahakamani ya kutaka apewe amlee mtoto wake aitwaye Sasha,aliyekuwa mzazi mwanzake, Faiza Ally amefunguka kuwa ni bora kufa kuliko kumuona mtoto wake akilelewa na mama mwingine wakati yeye yupo hai.
Sugu alimfikisha mahamakani mzazi mwenziye kwa madai kuwa ameshindwa kumlea mtoto wao kwa kuwa mama huyo si mwadilifu.
Faiza ameandika hivi kupitia Akaunti ya Instagram:
"Sielewi joseph ameshindaje kesi - ushahidi wa picha peke yake sioni kama unatosha mimi kupokonya mtoto wangu- mtoto wangu ni mdogo sana ananihitaji sana – na sita rudi hata ikibidi kuuza kila nilicho nacho kwa ajili ya kusimamia hili- sijapewa nafasi nimepelekwa mahakamani ijumaa na leo jumanne nimepewa hukumu/ mwanangu achukuliwe….. hapana !
..Sitarudi nyuma na haitakua rahisi ninakata rufaa na kutafuta wakili wa kunisimamia hili- mwanangu anasoma vizuri anaishi vizuri na naamini kwenye mikono yangu yuko salama zaidi ya kokote/ yaani kuhusu kukosa kukaa na mwanangu ni bora kufa kuliko kuishi nikimuona sasha ana lelewa na mama mwingine ikiwa mimi mama yake niko hai na makini katika malezi ya mtoto wangu - nina ndoto na mwanangu nyingi sana – nahitaji kuishi nae yeye ndio kila kitu kwenye maisha yangu / nampenda sana mwanangu na sijashindwa kumlea - naona uchungu sana kupelekea mahakani na kupokonywa mtoto wangu bila sababu za msingi.
..Sitaogopa cheo chake cha ubunge kamwe - ntasimama kama mama mwenye haki kwa mtoto wake. Mungu naomba nielekeze, nisimamia na unihukumie huu ukatili ninaofanyiwa na baba Sasha".