Sudani Kusini, Somalia zaomba uanachama Jumuiya EAC

Sudani Kusini, Somalia zaomba uanachama Jumuiya EAC

Kwa akili hiyo watanzania mtaishia kuzikwa katika hiyo ardhi,sasa hiyo ardhi isio tumiwa kuzalisha mali itawasaidia nini? mbaki na udongo wenu wengine waendelee kuungana.

Ardhi ya watanzania ni ya watanzania.. hata ikichukua miaka 100 tuweze kuitumia it doesnt matter... tumeshashuhudia matatizo ya ardhi huko kwao.. hatutak kukaribisha matatizo kwetu.
 
>Somalia hapana...nchi zingine sawa lakini somaly? No no no no no!

Hivi kwani TZ bado ni mwanachama wa EAC??...................... tuwaachie wanachama waamue wenyewe!! Inawezekana wakakubaliana kwenye kikao chao cha leo kule Mombasa!!
 
Suala lenyewe liko hivi:1.Tanzania imekosea sana kujitumbukiza kijeshi migogoro ya maziwa makuu. Historically, yenyewe ndio ilikuwa kimbilio la hawa wengine wote. Soma hotuba ya Mwl. Nyerere kwenye mkutano mkuu wa CCM wakati wa mchakato uliompata Hon. Mkapa kama mgombea urais wa CCM. Kwamba tuna majirani 8 wanaotuzunguka na kwa hiyo inatakiwa rais mwenye busara ya hali ya juu jinsi ya kuishi nao. Hilo sasa tumelikosa na kwa miaka miwili iliyobaki litaendelea kutuandama.
2. Eac ina wanachama Burundi, Kenya, Rwanda,Tanzania na Uganda. Kura zikipigwa matokeo yatakuwa 4-1 (yaani wengine wote upande mmoja vs Tanzania upande mwingine. Ukumbuke pia kwamba Secretary General wa EAC ni kutoka Rwanda. 3. Kwa hiyo kwa sasa, sina hakika, inawezekana hawa wanne wakawa na kura ya kutosha kuwaingiza Somalia na Sudan kusini. Hii itafanya kura kuwa 6-1. Kwa hiyo watapitisha uamuzi wowote wautakao kwa wingi wa kura, na kwa maslahi. Kwa hiyo unapozungumzia demokrasia nk kama kigezo, utaanza kujiuliza nani kati ya hawa viongozi wa sasa aliyechaguliwa bila kuiba kura, utakuta ni wa Sudan kusini peke yake! Au nani hakutokea mazingira ya vita au kugandamiza wapinzani unaweza kokosa yoyote. Hilo ndilo tatizo lililopo mbele yetu kwa kukosea pointi namba 1 juu. Ni matumaini yangu kwamba, Rais Kikwete na Membe watafanya kila jitihada za kidiplomasia kurejesha mahusiano na Rwanda kwa faida ya Tanzania. 4.Ukweli ni kwamba, migogoro yote hii, mlengwa ni utajiri wa DRC na ndio uliowatoa roho Lumumba Patrice, Mobutu Seseseko na Kabila baba. Sitashangaa Joseph Kabila akifuata njia hiyohiyo-time will tell. Na watakaomtenda ni kati ya hawa wa hizi nchi sita on top of Usa,France,China,Israel, South Africa na Belgium. 5. Kenya peke yake ndio atafaidika na haya yote tena bila jasho wala jeshi lake maana mazingira yanakuja kutokana na makosa yetu. Siku zote tutambue hakuna Rwanda na Uganda na burundi-lao moja na watu wao na viongozi wao ni watu walewale. EAC sasa iko chini ya kundi hili na huo ndio ukweli. Tanzania ilitakiwa iwe macho tangu awali. Mwono wangu.
 
Kwa akili hiyo watanzania mtaishia kuzikwa katika hiyo ardhi,sasa hiyo ardhi isio tumiwa kuzalisha mali itawasaidia nini? mbaki na udongo wenu wengine waendelee kuungana.
Kwanini Watutsi walihama huko Ethiopia?
km ni kutafuta Ardhi ni bora tubaki nayo kuliko kuwakaribisha mijitu yenye tamaa ya kutawala kila waionapo ardhi
 
Hizo nchi zikikubaliwa agenda kuu kila siku itakuwa kujadili hali ya usalama. Agenda ya uchumi haitajadiliwa hata siku moja.

Wapewe kwanza masharti ya kupropagate kiswahili kwa miaka kumi, kiswahili kikitumika kiasi cha kuridhisha ndio maombi yao yaanze kujadiliwa. Kama waliweza kujiufnza kiarabu basi wanaweza kujifunza kiswahili pia...
 
Kuna umuhimu wa kupata maoni mapya ya Wananchi.
 
Kwa akili hiyo watanzania mtaishia kuzikwa katika hiyo ardhi,sasa hiyo ardhi isio tumiwa kuzalisha mali itawasaidia nini? mbaki na udongo wenu wengine waendelee kuungana.

Mkuu povu la nini .. Hatutaki kwani lazima bana..
 
Suala lenyewe liko hivi:1.Tanzania imekosea sana kujitumbukiza kijeshi migogoro ya maziwa makuu. Historically, yenyewe ndio ilikuwa kimbilio la hawa wengine wote. Soma hotuba ya Mwl. Nyerere kwenye mkutano mkuu wa CCM wakati wa mchakato uliompata Hon. Mkapa kama mgombea urais wa CCM. Kwamba tuna majirani 8 wanaotuzunguka na kwa hiyo inatakiwa rais mwenye busara ya hali ya juu jinsi ya kuishi nao. Hilo sasa tumelikosa na kwa miaka miwili iliyobaki litaendelea kutuandama.
2. Eac ina wanachama Burundi, Kenya, Rwanda,Tanzania na Uganda. Kura zikipigwa matokeo yatakuwa 4-1 (yaani wengine wote upande mmoja vs Tanzania upande mwingine. Ukumbuke pia kwamba Secretary General wa EAC ni kutoka Rwanda. 3. Kwa hiyo kwa sasa, sina hakika, inawezekana hawa wanne wakawa na kura ya kutosha kuwaingiza Somalia na Sudan kusini. Hii itafanya kura kuwa 6-1. Kwa hiyo watapitisha uamuzi wowote wautakao kwa wingi wa kura, na kwa maslahi. Kwa hiyo unapozungumzia demokrasia nk kama kigezo, utaanza kujiuliza nani kati ya hawa viongozi wa sasa aliyechaguliwa bila kuiba kura, utakuta ni wa Sudan kusini peke yake! Au nani hakutokea mazingira ya vita au kugandamiza wapinzani unaweza kokosa yoyote. Hilo ndilo tatizo lililopo mbele yetu kwa kukosea pointi namba 1 juu. Ni matumaini yangu kwamba, Rais Kikwete na Membe watafanya kila jitihada za kidiplomasia kurejesha mahusiano na Rwanda kwa faida ya Tanzania. 4.Ukweli ni kwamba, migogoro yote hii, mlengwa ni utajiri wa DRC na ndio uliowatoa roho Lumumba Patrice, Mobutu Seseseko na Kabila baba. Sitashangaa Joseph Kabila akifuata njia hiyohiyo-time will tell. Na watakaomtenda ni kati ya hawa wa hizi nchi sita on top of Usa,France,China,Israel, South Africa na Belgium. 5. Kenya peke yake ndio atafaidika na haya yote tena bila jasho wala jeshi lake maana mazingira yanakuja kutokana na makosa yetu. Siku zote tutambue hakuna Rwanda na Uganda na burundi-lao moja na watu wao na viongozi wao ni watu walewale. EAC sasa iko chini ya kundi hili na huo ndio ukweli. Tanzania ilitakiwa iwe macho tangu awali. Mwono wangu.

Nijuavyo mie Mkataba wa EAC (kama sijakosea) hakuna utaratibu wa majority-based decisions bali consensus-based decisions kwa hiyo hakuna wengi wape hata kama watakuwa 10:1(Niko tayari kukosolewa). Lakini mi kwa upande mwingine naona kama Sudan kusini ikiwa mwanachama itakuwa ahueni kwa Tanzania, kwani inaweza ikapunguza "land tension" (kama tunavyoamini kwamba hitajio kubwa sana kwa membres wengine) kwa vile nchi nyingine zenye uhaba wa ardhi zitatupia macho pia na huko badala ya Tanzania pekee (delflection of demand for land ).
 
Tatizo hili lijumuiya halina vigezo maalumu vya kujiunga, kila mtu anajiunga tuu. nilisikia wakati fulani hata congo nao wanataka. Sio kwa sababu uko afrika mashariki kijiografia una sifa za kujiunga na EAC. kama ni hivo basi nchi zote za ulaya zingekuwa kwenye EU, lakini kuna vigezo wanavyoshindwa kuvitimiza. Ona Rwanda na Burundi zilivyoingia kinyemelea, burundi wako vitani lakin wanaruhusiwa kujiunga. Political stability ilitakiwa iwe ni moja ya vigezo vya kujiunga. Eti wana tuma ujumbe kwenda somalia kukagua kama wanakidhi vigezo!!! hivi unahitaji kwenda kulijua hilo., liko wazi.Tatizo akina kagame wanatafuta malisho ya wafugaji wao, so wameona Tz hakuingiliki wameamua kutafuta kwingine. Kama tunahitaji alliance ya kiuchumi tuendeleze mtwara corridor, tujiunge na msumbiji walio na rasilimali nyingi kama sisi, tuna historia inayofanana, pia uchumi wao unakuwa kwa kasi na si uchumi kwa kenya ulio-saturate au kauchumi ka Rwanda kenye ukubwa sawa na soko la kariakoo na soko la watu milioni 5. PERIOD

Mkuu,
Naungana nawe juu ya fursa lukuki zilizopo Msumbiji, na nijirani zatu wazuri kuliko hizi nchi za Magharibi yetu.
 
Suala lenyewe liko hivi:1.Tanzania imekosea sana kujitumbukiza kijeshi migogoro ya maziwa makuu. Historically, yenyewe ndio ilikuwa kimbilio la hawa wengine wote. Soma hotuba ya Mwl. Nyerere kwenye mkutano mkuu wa CCM .
Mwaka 1996, mjini Kigali, Rwanda kilikuwa kimeundwa kikundi cha wapiganaji waliojiita "wapinzani wa dikiteta Mobutu." Hawa walikuwa Wakongomani na Wanyarwanda kutoka Rwanda
Wakati kikundi hicho kinataka kuanza vita, kilitaka kuwa na msemaji. Mungu akupe nini! Hakuna uthibitisho wowote, lakini taarifa zinaeleza kiliomba ushauri wa Mwalimu Julius Nyerere "ambaye aliwapa Laurent Desire Kabila kuwa msemaji wa wapiganaji." Mwanzoni mwa vita ya kumg'oa Mobutu....
Hapo kwenye Green ni kwamba hujui lolote kuhusu Mgogoro wa Maziwa Makuu, na unapomuweka J.K. Nyerere ndio kabisa mtu km mm unanipoteza kwani alikuwa ana uwezo kabisa wa kumaliza huo mgogoro lakini alikaa kimya akijua ni nini kiko nyuma yake. pekua kwanza hii Historia ya wenyewe ndio tutaelewana SOMA LINK HIYO

Ijue Rwanda, Kagame, Mseveni na Uvamizi wao katika Ardhi ya Kongo

Tukirudi kwenye Mada ni kwamba haiwezekani kabisa kuanza kuwabeba Sudan Kusini na Somalia ni heri tujitoe huo Muungano wa EAC kwani ni kiini macho cha Watutsi kutaka kutawala tu katika haya Maziwa Makuu wao wameshajiwekea Imani kuwa ni Nchi waliyoahidiwa. Tafadhali chimbua hizi Historia
Kabila alikuwa tayari amesoma mwelekeo wa makubaliano yake na kuona kuwa yanatoa mwanya kwa kile kilichoitwa "Nchi ya Ahadi" ya Watutsi kutoka Rwanda, Burundi, Uganda, Somalia, Ethiopia, Eritrea na Tanzania. Baada ya kuingia ikulu, Kabila anadaiwa kuwageuka wenzake.
 
Wote wajinga, mnatakiwa kujua kuvunjika kwa East Africa ni propaganada za Western Countries. Western countries hawafurahi inchi za kiafrica kuungana ili waendelee kututumia kwa manufaa yao. Mgogoro unao endelea kati ya Rwanda na Tanzania umepandikizwa na western countries kwa manufaa yao. Sie tumebaki kujisifuu ooo inchi yetu kubwa, tunautajiri kuliko Rwanda, tuna nguvu za kijeshi...wenzetu saa hizi wamekaa wanatucheka .... wanasema (Mission Accomplished).
Jamani tufunguke angalau kidogo
 
Absolutely you exactly know what you are talking about... the problem is that among 100 people only one or two can understand this and this is where the Western Countries screw us.
 
Ardhi ya watanzania ni ya watanzania.. hata ikichukua miaka 100 tuweze kuitumia it doesnt matter... tumeshashuhudia matatizo ya ardhi huko kwao.. hatutak kukaribisha matatizo kwetu.

swadaktaa
 
Mnapo amua kuungana ina maana mna tofauti na tofauti ndizo zinazo wafanya muungane. Mwingine hana ardhi lakini ana rasilimali, mwingine anategemea kufaidika kibiashara na jirani yake ambaye bado haja amka kibiashara, kiuchumi , kielimu na kadhalika kuna mambo mengi sana tunategemeana. Sasa nashangaa kusikia baadhi yetu tukisema oo, wanafata ardhi, mara utajiri,..utajiri tulio kaa nao kwa zaidi ya miaka hamsini tangu tulipopata uhuru tumeufanyia nini? cam on!
 
Kama Somalia itapewa uanachama wa EAC, basi ninashauri Tanzania tujitoe tu tena kwa haraka sana. Tena ukizingatia kwamba shirikisho litakapoundwa kila mtu atakuwa na uhuru wa kuishi na kufanya kazi popote ndani ya nchi wanachama, hii ni hatari kwa nchi yetu. Kama wasomali wachache tu tulionao wanatuliza itakuwaje watakapomiminika kwa wingi.
 
Wageni ndio waleta chokochoko tumemkaribisha Rwanda ndo ivyo je ao wasiopatana wenyewe kwa wenyewe
 
Somalia hapana. Kumbukw kujiunga jumuiya ni pamoja na kuondoa vikwazo vya visa
 
Ardhi ya watanzania ni ya watanzania.. hata ikichukua miaka 100 tuweze kuitumia it doesnt matter... tumeshashuhudia matatizo ya ardhi huko kwao.. hatutak kukaribisha matatizo kwetu.

Umenena Mkuu !!
 
Back
Top Bottom