Sudani Kusini, Somalia zaomba uanachama Jumuiya EAC

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
[h=1][/h]

Arusha. Nchi za Sudani Kusini na Somalia, zimeomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki(EAC) na tayari mchakato wa kupitia maombi hayo umeanza.

Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Dk Richard Sezibera alitoa taarifa hiyo jana katika kikao na waandishi wa habari, wakati akielezea kuanza kikao cha baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo.

Alisema kikao cha baraza la mawaziri kinatarajia kupokea ripoti kuhusu maombi hayo, ambapo tayari timu ya maofisa wa jumuiya hiyo ilikwenda Sudan Kusini kutazama kama ina sifa za kujiunga na jumuiya hiyo.

Alisema kwa upande wa Somalia, baraza hilo linatarajia kuridhia uamuzi wa Sekretarieti ya jumuiya ya kutuma maofisa wake kwenda Somalia kutazama kama ipo tayari kujiunga .

Aidha alisema hadi nchi hizo kukubaliwa kuwa mwanachama kuna mchakato mrefu zitapiti
 
Wanayo Ardhi ambayo ndiyo kiu kubwa ya Mseveni na Kagame?
 
Rwanda wenyewe wameshatutoa kamasi sembuse tunataka kukaribisha matatizo zaidi?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Huu umoja unaendeshwa na wanasiasa ambao wanataka kukimbia mbio kabla hata hawajatambaa, na ndio maana haitashangaza kama utavunjika kwa sababu wananchi hawashirikishwi kabisa.
 
Kila nch yenye majanga inataka kuhamishia EAC matatizo yao kwa kicngizio cha UMOJA tangu watu weusi tukaweza kunia mamoja! Ubinafsi ndo tunaouweza2!
 
>Somalia hapana...nchi zingine sawa lakini somaly? No no no no no!
 
Wanayo Ardhi ambayo ndiyo kiu kubwa ya Mseveni na Kagame?

Kwa akili hiyo watanzania mtaishia kuzikwa katika hiyo ardhi,sasa hiyo ardhi isio tumiwa kuzalisha mali itawasaidia nini? mbaki na udongo wenu wengine waendelee kuungana.
 
...dah!...haya sasa yatakuwa ni zaidi ya majanga,hawa wasomali wachache wa chama cha mateje wameisha-tuchosha,sasa tena na huo uko mzima wa wasomali nao ukijiunga na EA si ndo tembo wetu walio baki waitaisha kwa wiki moja!!??...
 
Na sisi Watanzania tupeleke maombi ya kujitoa EAC! Hatuoni tuko meza moja na maadui wa vizazi vyetu vijavyo?
 
Rwanda wenyewe wameshatutoa kamasi sembuse tunataka kukaribisha matatizo zaidi?
[/QUOTE

Rwanda wanajipenga kamasi wenyewe, waache watasalimu amri tu ni swala la mda ila kwa msomali HAPANA itabidi TZ tujitoe EAC mapema zaidi.
 
Hii jumuiya ilipoteza mwelekeo tu pindi Burundi na Rwanda zilipojiunga nayo, na sasa itapoteza maana kama Sudan kusini na Somalia nazo zitajiunga
 
Mchakato wa nchi ya Uturuki kujiunga na umoja wa ulaya umechukua muda mrefu kwasababu ya kutokidhi vigezo muhimu leo tunataka Somalia ijiunge na EAC wakati serekali yake haina ubavu wa kutawala mikoa mingi ya nchi hiyo kama si kukaribisha majanga katika EAC ni nini ?.Kwanza wakimbizi watazagaa katika jumuiya yote,pili ujambazi na ujangili utatamaliki katika jumuiya yote na mwisho fedha chafu zitazagaa katika jumuiya yote na mwisho zitaamua nani anakuwa kiongozi wetu.
 
EAC inatakiwa iweke masharti mapya yanayojumuisha demokrasia, uhuru wa wananchi na vyombo vya habari kutoa maoni bila woga pamoja na suala la ukabila kutokutawala serikali za nchi waombaji. Hii itasaidia kuepuka migogoro ya kijinga kama wa hivi kati ya Rwanda vs Tanzania.
 
Rwanda wenyewe wameshatutoa kamasi sembuse tunataka kukaribisha matatizo zaidi?

mwenzangu...labda tungeanza kwanza mchakato wa kuiondoa Rwanda kwenye EAC kwanza ndo tuje na hilo la kuwaingiza hao wengine. lakini kwa kweli kuingia urafiki na watoto wakorofi mtaani si kitu salama kabisa. hawa wabakie hukohuko kwanza tumalizane na hili la kagame. labda sudani ya kusini...lakini somalia? noooooo.........wasubiri kwanza.
 
EAC inatakiwa iweke masharti mapya yanayojumuisha demokrasia, uhuru wa wananchi na vyombo vya habari kutoa maoni bila woga pamoja na suala la ukabila kutokutawala serikali za nchi waombaji. Hii itasaidia kuepuka migogoro ya kijinga kama wa hivi kati ya Rwanda vs Tanzania.

Very well said....
 
Naomba kuuliza.hivi wanyarandwa nao ni jamii ya nilotic?kama jibu ni ndio sishangai wasomali na wa-south sudanise kuomba kujiunga na east africa community.wanawafata ndg zao na hatimae kuendeleza utamaduni wao wa vita na mauaji.mtazamo tu.
 
kazi kweli hapo ni kujitoa mhanga kwa nchi zote kama wenyewe tu hawaelewani itakuwa kwetu
 
msimamo mkali wa alshabaaab hatuwataki wakaungane na uamsho labda wakija kuchukua nchi
 
Tatizo hili lijumuiya halina vigezo maalumu vya kujiunga, kila mtu anajiunga tuu. nilisikia wakati fulani hata congo nao wanataka. Sio kwa sababu uko afrika mashariki kijiografia una sifa za kujiunga na EAC. kama ni hivo basi nchi zote za ulaya zingekuwa kwenye EU, lakini kuna vigezo wanavyoshindwa kuvitimiza. Ona Rwanda na Burundi zilivyoingia kinyemelea, burundi wako vitani lakin wanaruhusiwa kujiunga. Political stability ilitakiwa iwe ni moja ya vigezo vya kujiunga. Eti wana tuma ujumbe kwenda somalia kukagua kama wanakidhi vigezo!!! hivi unahitaji kwenda kulijua hilo., liko wazi.Tatizo akina kagame wanatafuta malisho ya wafugaji wao, so wameona Tz hakuingiliki wameamua kutafuta kwingine. Kama tunahitaji alliance ya kiuchumi tuendeleze mtwara corridor, tujiunge na msumbiji walio na rasilimali nyingi kama sisi, tuna historia inayofanana, pia uchumi wao unakuwa kwa kasi na si uchumi kwa kenya ulio-saturate au kauchumi ka Rwanda kenye ukubwa sawa na soko la kariakoo na soko la watu milioni 5. PERIOD
 
Back
Top Bottom