Sio kila kitu abt EAC tusingizie ujanja wa wakenya tutakuwa tunawapa sifa bure zisizo na msingi, mambo mingine ni mawazo binafsi ya watu na mtazamo wa nchi juu ya jinsi gani itashirik ktk siasa za nje, mambo ya kuzingatia hapa ni kwamba HILI TAIFA NDIO KWANZA LIMEPATIKANA then wamekua ktk mapigano na Sudan kaskazin kwa takriban miaka 50 na zaidi so kuanza kwa kujitenda, kukata mawasiliano na kaskazini ni njia nzuri ya kujijenga pia kujitegemea! Mkuu kifup thread yako nimeipenda, nadhan hawa wakaribishwe tu wajiunge tena pasipo vikwazo vyovyote ili mradi wanavigezo vya utaifa, kwangu Sudan kusini ni kama mtoto anaejifunza kutembea hivyo anapaswa kushikwa mkono na mataifa yaliyo simama pamoja na Tanzania. bt napenda toa angalizo kwan kiasilia hawa watu niwakorofi sana, itabidi tujipange jinsi ya kudeal nao. Mh. John Garang ktk maisha yake aliishi km mtanzania na hata harakati zake mipango mingi, strategies yake nyingi zilipangwa Bongo, zaidi alisoma University of Dar es salaam, ndie Baba wa taifa hili jipya la sudan kusin, tuwapokee hawa ndugu pia tuwe makini nao mpaka watakapo settle!