Sudan kukubali kusini ijitenge?-Bado Tanganyika kukubali! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sudan kukubali kusini ijitenge?-Bado Tanganyika kukubali!

Discussion in 'International Forum' started by MrFroasty, Jan 19, 2010.

 1. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Rais Omar al-Bashir amesema atakubali upande wa kusini ujitenge iwapo raia wa eneo hilo watapiga kura ya maoni ya kutaka uhuru wao mwakani.

  Akizungumza wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka mitano tangu kumalizika kwa vita vya pande mbili za kusini na kaskazini, chama chake cha Northern Congress hakikutaka kusini ijitenge.

  Lakini amesema chama hicho kitakuwa cha kwanza kukubaliana na uamuzi huo.

  Wachambuzi wamesema Bw Bashir ametumia lugha isiyo ya kawaida, yenye kuonyesha kuridhia ambayo imepokelewa vyema.

  Katika miezi ya hivi karibuni wasiwasi umekuwa ukiongezeka baina ya pande hizo mbili.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Dhambi ya ubaguzi (against Mainland Tanzania) itakutafuna mpaka kizazi cha tatu na cha nne!
   
 3. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwani mushaacha kutuita wapemba hapo Dareselaam?...Mara ya mwisho mimi nilikuwa siitwi jina langu hapo Dar...nilikuwa "aaah hawa wapemba!"....sasa sijuwi nani mbaguzi?
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Tanzania haitogawanyika hizo ni ndoto zako za za Mchana Sahau kitu kama hicho Muungano utakuwepo pale pale kama ulivyowekwa na waanzilishi wa huo Muungano Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Mzee Abeid amani Karume Wanaotaka Muungano uvunjike hao ni Maaduwi wa Tanzania na ni Mafisadi wa nchi yetu iliyokuwa na Uhuru na amani Udumu Muungano wetu Amina
   
 5. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hakuna ubaguzi wowote, wananchi wakiuliza haki zao ni ubaguzi mawazo ya kikoloni hayana nafasi karne hizi

  Wazanzibar waachwe wenyewe, waunde serikali yao bila mikono isiyo na udhu kutoka bara
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Muungano siyo dini ukivunjika ni sawa, usipovunjika ukaimarika sawa, lakini kulazimisha, watu kwenye muungano ni ukoloni.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  pamoja na hayo yote uliyoyasema hata kama kukifanyika kura ya Maoni bara na Visiwani watu wa visiwani wote wakisema yes Muungano uvunjike na Watu wa Wabara wakisema No Muungano usivunjike basi utakuwa huo Muungano hauvunjiki Mkuu Tumaini hapa hatuzungumzii mambo ya Dini. Dini na Siasa ni vitu 2 Tofauti Mkuu Tumaini ukitaka mambo ya Dini nenda kule kwenye Dini hapa tunapeana mawazo tu asante sana
   
 8. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Kama mnavyowaita wenzenu wanyamwezi au wa Bara. Ninyi ni wapemba
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jan 20, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama ningekuwa natoa maksi za inferiority complex basi ungekuwa na 99.9%! Kuna watu wanaitwa Wachaga, Wangoni, Wahaya (hata humu JF kulikuwa na thread kuhusu wao), Wamakonde (hawa jamaa huwa wakitaniwa hudai: kwani Mmakonde chio ntu?), nk, lakini hawakasiriki! Kuna Wapemba wawili nimesoma nao mimi lakini tumeishi nao vizuri sana mpaka tumemaliza Chuo, tulikuwa tunawatania kuhusu Kiswahili chao ambacho ni tofauti kidogo na cha Bara! Kwa mfano sisi tunasema "kupiga photocopy" lakini mwenzetu anadai ni "kutolesha photocopy!" Alidai kwamba "kupiga" maana yake ni mpaka uwe na fimbo au kitu kingine! Wale wapemba sijui wako wapi mpaka sasa nawamiss sana! Tuache chuki, hazijengi, zinabomoa!
   
 10. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni kweli muungano wetu utaendelea kuwepo, lakini kuna marekebisho yanayohitajika.
  Angalia suala la sasa la Karume kuongezewa muda - vikao vya ccm vinaahirishwa kwa kuwa wajumbe toka zanzibar hawataki kuhudhuria kwani hawajaona kama ajenda yao ya kuongezewa muda itakubalika.Je vikao vitaahirishwa hadi lini?
  Hii inaonyesha kuwa muungano katika form tuliyo nayo sasa ina kasoro. Nadhani kama ingekuwa ni muungano wa serikali tatu mambo yangekuwa mazuri zaidi.

  Hivi sasa Zanzibar inasukuma ajenda zake kwa nguvu na mwishowe zinakubalika, lakini ukiangalia kwa makini utaona ajenda hizo zinadhoofisha muungano katika hali yake ya kabla ya ajenda hizo.
  Kumbuka kuchafuka kwa hali ya kisiasa Zanzibar kulikomlazimisha Rais Abdul Jumbe kujiuzuru. Aliyokuwa akiyadai na kuyafanyia maandalizi ni: Bendera ya Zanzibar, Wimbo wa Taifa wa Zanzibar, na Sarafu ya Zanzibar. Haya madai yalionekana kuwa ni maasi.
  Lakini hadi sasa tayari Wimbo wa Taifa wanao, Bendera wanayo bado sarafu - sisi tunaona haya si maasi kama baba wa Taifa alivyoyaona! Sarafu nayo wanaidai kwa mkakati maalumu. Huwezi kuwa na sarafu imara bila kuwa na uchumi imara - ndiyo maana wanadai mambo yanayoimarisha uchumu yaliyo kwao yawe ya kwao -kama mafuta nk. Tutakubali mafuta, baadae bandari, baadae bahari,baadae benki kuu na hatimae sarafu yao!
  Tatizo bara tukitishiwa nyau tunaogopa - yaani tukiambiwa bila hivi basi bora muungano uvunjike, tunaogopa na kukubali bila kujua kuwa tunaumomonyoa taratibu.Ukweli uko pale pale kwamba Zanzibar katika muungano wa sasa wanajitoa taratibu ila bara ndio tunawang'ang'ania - na sijui kwa nini!
   
 11. bona

  bona JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  sidhani kama zanzibar wanalizimishwa kua kwenye muungano, kura ya maoni ilipita na wote matokeo yakaonekana kua wanataka kubaki kwenye muungano, sasa hawa watu wachache wanajifanya kauli zao ni za wazanzibar wote ni nani? mimi kama mbara sina kitu nnachoweza sema iwapo muungano utavunjika basi tutapoteza labda mmoja wao atueleze ili tujue kwamba tunawabania au tutapoteza sana iwapo muungano utavunjika!
  ukweli ni kwamba majority ya wazanzibar wanataka muungano uwepo na kura ya maoni iliyofanyika imedhihirisha hilo na mimi kama mtanganyika muungano uwepo au usiwepo nadhani hautaleta changes zozote ktk mustakabali mzima wa tanganyika kijamii, kiuchumi na kitamaduni nadhani labda wazanzibar wengi ndio watasuffer kwani majority wako uku na wana earn daily bread uku kuliko watanganyika walio zanzibar!
   
 12. N

  Nanu JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa ni kwa ridhaa wa wananchi wa pande zote mbili. Leo hii wakitaka kujitenga na wajitenge tu.
  Mimi naheshimu sana hekima na busara za wamarekani, sijawahi kusikia hata state moja ya Marekani ikigusia kujitoa bali zingine zinataka kujiunga.
  Wamarekani husikii wakijiita mimi mu washington, mu-ney york, mu-texas, etc, utasikia tu wakisema I am an American. Sasa sisi unakuta mimi mzanzibari au mimi mpemba, sijawahi kusikia mtu akisema mimi mbara.
  Tatizo hili litawala sana hawa wanaopenda kujibagua wenyewe. Nasikitika sana mtu anapokuwa anatetea kila wakati mafarakano na kutengana badala ya mapatano na umoja. Ingetakiwa sasa hivi tuwe tunafikiria jinsi ya kujiunga na Comoro na Mauritius tuwe state moja, ingetujenga zaidi..
  Tuangalie na tujivunie tulichonacho ili tuweze kupiga hatua mbele zaidi kutafuta tusichonacho kwa umoja wetu. Tuache ubinafsi na uchoyo!
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Big-up mzizi..
  Umeongea points tupu mkuu
  You are a genius sometimes!
   
 14. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kura si ilipigwa na JWTZ?...acha pumba, ni lini kumepigwa kura ya maoni?Ni lini na nyaraka gani inaonesha kuwa sheria zilifuatwa katika kuhalalisha muungano?

  Tuzungumze points sio pumba tafadhali...
   
 15. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #15
  Jan 20, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  1.
  THE ARTICLES OF UNION
  between
  THE REPUBLIC OF TANGANYIKA AND THE PEOPLES' REPUBLIC OF
  ZANZIBAR

  WHEREAS the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar being mindful of the long association of the peoples of these lands and of their ties of kinship and amity, and being desirous of furthering that association and strengthening of these ties and of furthering the unity of African peoples have met and considered the union of the Republic of Tanganyika with the Peoples Republic of Zanzibar:
  AND WHEREAS the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar are desirous that the two Republics shall be united in one Sovereign Republic in accordance with the Articles hereinafter contained:-
  It is therefore AGREED between the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar as follows: -
  (i) The Republic of Tanganyika and the Peoples' Republic of Zanzibar shall beunited in one Sovereign Republic........
  IN WITNESS WHERE Julius K. Nyerere, the President of the Republic of Tanganyika, and Abeid Karume the President of the Peoples' Republic of Zanzibar have signed these Articles, in duplicate, at Zanzibar, on this twenty-second day of April, 1964.

  2. Zanzibar ni nchi na ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano (Ibara ya 1 ya Katiba ya Zanzibar, 1984).
   
 16. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Malizia mpaka mwisho wa hiyo nyaraka, nani akatia saini ?Nyerere na Msekwa, hakuna sehemu inayoonesha kama vyombo vya sheria vya Zanzibar ambayo ndio vinawakilisha watu wa Zanzibar kuwa vilipitia huo mkataba na kutia saini.

  Au unayo wewe saini kwenye huo waraka?
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Jan 20, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  IN WITNESS WHERE Julius K. Nyerere, the President of the Republic of Tanganyika, and Abeid Karume the President of the Peoples' Republic of Zanzibar have signed these Articles, in duplicate, at Zanzibar, on this twenty-second day of April, 1964.
   
 18. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Saini iko wapi saini ya Karume?Hilo ndio suali langu...sitaki porojo.Soma maelezo haya acha ubishi mwingi.

   
 19. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  MrFroasty usipoteze wakati wako kwa kubishana na watu vichwa mchungwa
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Jan 20, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Shame on you!
   
Loading...