Sudan: Baraza la mpito limekubali kumkabidhi Rais wa zamani Omar al Bashir kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
2,392
3,017
Baraza la mpito limekubali kumkabidhi rais wa zamani Omar al Bashir kwa mahakama ya kimataifa ya ICC.

Rais huyo wa zamani anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, juu ya mzozo uliotokea katika mkoa wa Darfur mnamo 2003.

Aliondolewa madarakani mnamo Aprili 2019 kutoka na maandamano na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili kwa kukutwa na hatia katika makosa ya Rushwa na Utakatishaji Fedha.

Kabla ya kuhukumiwa Al-Bashir alikuwa akishikiliwa tangu mwezi Aprili, baada ya Jeshi kumtoa madarakani kutokana na maandamano ya mfululizo dhidi yake na kusababisha Jeshi kuchukua nchi likiongoza kwa kushirikiana na Raia.

Baada ya hukumu hiyo, kwa mujibu wa Sheria za Sudan, al-Bashir angefungwa katika gereza la Serikali ambalo ni kwa ajili ya Wazee waliokutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo kisicho na adhabu ya kifo.

Aliingia madarakani katika mapinduzi ya kijeshi mnamo 1989 na akatawala nchi kwa kwa kile kilichoitwa ngumi ya chuma.
====

My take;
Maana yake, toka kipindi kile,ICC watoe warrant yakumkamata,sasa wamefanikiwa kwenye hili suala

Onyo kwa viongozi wengine wa Africa, mambo hubadilika, Uganda M7 kua macho, kuna siku watakudandia.
 
Uganda, Rwanda, Burundi na Congo hizo nchi ziache zilivyo, zina mrengo tofauti wa kiutawala.

Hao marais waliopo wanajua diplomasia sana na wameachwa hapo sababu angalau wamejaribu kuleta utulivu kwenye nchi hizo.

Ukija kwa akina Kenya, Tanzania, Malawi, Zambia ndio angalau tunafanana mfumo wa siasa, hivyo kiongozi yoyote akijifanya kufuata status quo za Rwanda, Uganda, Burundi na Congo atapoteana sana.

Unforgetable
 
Back
Top Bottom