Subiri ipite tuisome namba ya Matarimo!

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,425
Gari ya ubia iliyokuwa inawapeleka kazini jamaa wane imesababisha ugomvi mkubwa! Bwana Matarimo amechoka kuchangia gari ameamua kuwafukuza wawekezaji wenzie waliodunduiza pamoja na kuchangia gharama za ununuzi wa gari hilo.

Wabia wamemkubalia, lakini kila aliyeondoka ameandoka na kiungo kimojawapo cha gari kulingana na mchango wake wa pesa. Kuna aliyeondoka na usukani na taa, mwingine vioo na swichi; mwingine kaondoka na injini yote pamoja na giaboks yake!

Pamoja na kubaki na kopo, Matarimo yumo tu: Kila asubuhi anawaamsha mapema wanae na kuwaamuru wamsukume mpaka ofisini na jioni wamrudie!

Kituko cha Matarimo kimeamsha mjadala mtaani; watu wengi wanaodhani kuwa si bure, lazima kuna fyuzi moja au mbili zilizokatika kichwani mwa Matarimo; wengine wanadai Matarimo yuko sawa, eti usafiri wa kuchangia hautufai Waafrika, tuwaachie wazungu.

Wenye busara zao wamemshauri Matarimo kuwa hawezi kuendelea kukiita chombo chake motokaa ilihali kinategemea nguvu ya kusukumwa, ni heri akiite mkokoteni dunia itaelewa. Matarimo hakubali; anadai ili mradi inaserereka, ina paa na imepakwa rangi, basi hiyo ni gari!

Awali tulidhani sababu ya vitimbi vyote hivi ni roho ya choyo lakini baada ya kufuatilia tumekuja kugundua kuwa kumbe sababu kubwa Matarimo kuwafukuza wenzie ni kutaka wawe WANAISOMA NAMBA ya ule mkwama kila anapowapita. Ana hofu wakiwa ndani hawawezi kukiona kibao cha namba!

©James Gayo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom