Lijualikali, chozi la mwanaume halina thamani, kabla ya kulia ungetafakari yafuatayo

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Niseme machache kuhusu rafiki yangu Lijualikali. Nimeona baadhi ya wafuasi wa Chadema wakimshambulia baada ya kueleza kuwa hana mpango wa kuendelea tena na chama hiki baada ya bunge hili kuisha, na kwamba atahamia CCM na ameomba apangiwe kazi yoyote hata kama ni ya ulinzi au kufagia. Yani yupo tayari akafagie CCM lakini si kuendelea kubaki Chadema.

Pengine Lijualikali ameshambuliwa sana kutokana na kutoa tuhuma zisizokua na ushahidi, pamoja na kashfa kwa chama chake cha zamani (Chadema) kilichomlea na kumkuza kisiasa. Hata hivyo si kosa kwa Lijualikali kuhama chama, kama ambavyo haikua kosa kwa Nyalandu kuja Chadema au Maalm Seif kwenda ACT.

Kila mtu ana haki na uhuru wa kujiunga na chama chochote cha siasa akipendacho na ambacho anaamini katika falsafa na itikadi yake. Hata Mwalimu Nyerere aliwahi kusema CCM sio baba yake wala mama yake, licha ya kwamba yeye ndiye aliyeiasisi.

Kwahiyo Lijualikali hakua na sababu ya kutoa kashfa kwa Chadema ili apate uhalali wa kuondoka. Angeweza kuondoka tu kistaarabu na isingekua dhambi. Nobody knows what tomorrow hold for us.!

Anyway. Watu wengi wamemtaka akumbuke chama kilikomtoa. Wengine wameeleza maisha binafsi ya Lijualikali kuwa kabla ya ubunge alikuwa akiishi chumba kimoja (hichohichio sebule, dinning, chumba, stoo, jiko). Wengine wakamkumbusha fedha za kampeni alizopewa na Mbowe. Wengine wakamkumbusha kipigo alichopewa na polisi na kufungwa jela miezi sita kwa sababu ya CCM haohao ambao leo anawaona wema.

Lakini hizo zote ni "personal attacks" kwa Lijualikali. Kwangu hazina maana yoyote. Lijualikali kukosa mahali pazuri pa kuishi kabla ya ubunge ni maisha ya kawaida kwa watanzania wengi. Inawezekana Lijualikali ni miongoni mwa watanzania waliokua wanaishi chini ya dola moja kwa siku kabla ya ubunge (absolute poverty), lakini umaskini haumuondolei mtu sifa ya kuwa kiongozi. Huko Bulgaria kuna mtu alipigiwa kura akawa mbunge akitokea barabarani (homeless man), bora hata Lijualikali aliyekua na chumba kimoja.

Kwahiyo nadhani tujikite kwenye hoja alizotoa badala ya kumshambulia mtoa hoja. Lijualikali alitoa hoja tatu. Ya kwanza alisema ndani ya Chadema maamuzi hufanywa na mtu mmoja tu ambaye ni Mwenyekiti. Ya pili wabunge kuchangishwa michango bila utaratibu. Ya tatu ni matumizi mabaya ya fedha za chama.

Hoja hizi zinapaswa kujibiwa kwa urari na uyakinifu ili kuondoa shaka miongoni mwa watu waliomsikiliza. Lakini kumshambulia yeye binafsi (personal attack) sio sawa kwa sababu wananchi watakosa majibu ya hoja hizo na huenda wakaziamini hata kama ni za uzushi.

Mimi nimejipa ‘assignment’ kidogo na ningependa kutumia wajibu wangu kama mwanachama hai wa Chadema (kwa miaka 13 sasa) kujibu hoja hizo tatu za rafiki yangu Lijualikali.

#Mosi; Maamuzi ya chama kufanywa na mtu mmoja. Lijualikali anadai maamuzi ya Chadema hufanywa na Mwenyekiti na watu wake wa karibu bila kushirikisha vikao halali vya chama. Ili kujenga msingi wa hoja yake akasema hata maamuzi ya wabunge kujiweka karantini, yalikuwa maamuzi binafsi ya Mbowe.

Hoja hii si kweli hata kidogo. Hakuna chama kinachofanya maamuzi shirikishi kama Chadema. Tanzania inajua hata wananchi ni mashahidi. Kwa mwaka huu Kamati kuu ya Chadema imeshakutana zaidi ya mara 5 kujadili na kufikia maamuzi juu ya mambo mbalimbali.

Nitajie chama chochote cha siasa hapa nchini ambacho kamati kuu yake imeshakutana mwaka huu angalau mara mbili. NCCR imekutana mara moja (March), TLP mara moja (April), CCM mara moja (February), ACT sina taarifa, CUF haijakutana kabisa.

Ukimuita mtoto mdogo ukamuuliza kati ya chama ambacho Kamati kuu yake imekutana zaidi ya mara 5 na chama ambacho kamati kuu yake imekutana mara 1 tu, kipi kinachofanya maamuzi shirikishi atakujibu bila tashwishwi. Lijualikali ameshindwaje kujua logic rahisi namna hii?

#Pili Wabunge kuchangishwa fedha kila mwezi. Lijualikali anadai wabunge wanachangishwa bila utaratibu na kwamba hakuna maelekezo ya KATIBA wala miongozo ya chama inayomtaka mbunge kuchangia, badala yake ni mawazo ya Mwenyekiti yaliyoamua hivyo.

Hii ni hoja mufilisi sana. Lijualikali kitaaluma ni mwanasheria, na bila shaka alisoma sheria ya katiba (Constitutional Law) alipokua anafanya shahada yake pale Chuo kikuu Tumaini. Sasa najiuliza alishindwaje kusoma Katiba ya Chadema kuhusu utaratibu wa kuchangia? Maana utaratibu huo umeelezwa kwenye Katiba sehemu ya Miongozo ya Chama, Wajibu wa mbunge kifungu cha 7 (a) na (b) vikisomwa kwa pamoja.

Ina maana Lijualikali amekuwa mbunge kwa miaka mitano bila kuona kifungu hicho? Au katiba kwake ni pambo tu? Haisomi? Hajawahi kuuliza hata wenzie kwamba kwanini tunachangia wakampa hicho kifungu asome? Kama ni kweli amechangia fedha kwenye chama kwa miaka mitano bila kujua kama ni wajibu wa kikatiba basi hana sababu ya kuendelea kubaki Chadema. He has proven to be a low minded person.

Mtu kama huyu akipewa uwaziri si anaweza kuingia mikataba ya ajabu dunia ikashangaa? Kama katiba ya Chadema yenye kurasa 200 imemshinda kusoma kwa miaka mitano, nini atasoma aelewe? Mikataba ya madini yenye kurasa 4,000 zilizoandikwa kwa kiingereza kigumu cha Ulaya vijijini?

#Tatu ni kuhusu matumizi mabaya ya fedha za chama. Lijualikali anadai fedha zinatumika vibaya. Anahoji ruzuku na michango ya wabunge kila mwezi. Lijualikali anatumia fursa hiyo kupotosha kwamba wabunge walipokuwa wakichangia waliambiwa fedha hizo zitawasaidia wakati wa kampeni. Lakini walipoenda kuuliza wameambiwa hazipo, zimetumika. Anahoji zimetumikaje?

Kwa lugha rahisi ni kwamba Lijualikali anamaanisha kwamba Chadema ni SACCOSS ambayo wabunge hukikopesha chama, halafu wakikaribia kampeni chama kinawarudishia fedha zao.

Hii ni hoja ya UONGO kabisa yenye nia ovu. Chadema sio SACCOSS wala KIKOBA. Katiba ya chama inasema wabunge watachangia kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa chama, na sio kwamba watarudishiwa wakati wa kampeni. Mwambieni asome Katiba vizuri.

Pesa zinazochangwa na wabunge pamoja na zile za ruzuku zinatumika kwenye shughuli za ujenzi wa chama kama vile operesheni mbalimbali, mikutano ya hadhara, vikao vya ndani, ununuzi wa vyombo vya uenezi kama magari, bendera, kadi, kulipia kodi ofisi za chama, kulipa mishahara maafisa wa chama, kununua samani (furniture) za ofisi etc.

Mwaka jana Chadema ilinunua magari mapya 20 (zero KMs) aina ya Ford Ranger kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa chama. Na magari hayo yalienda hadi Ifakara kumsaidia Lijualikali kwenye zoezi la Chadema ni Msingi. Leo anasema hajui fedha wanazochangia zinakwenda wapi. So funny.!

Halafu kama kweli hoja ya Lujualikali ingekuwa na mashiko basi CAG angeshawapa Chadema hati chafu kwa ubadhirifu wa fedha. Lakini kila mwaka CAG anapita na kukagua hesabu za chama anaridhika.

Mwaka juzi ndio chama kilipata doa kidogo kilipomkopesha mbunge mmoja 140M kwa ajili ya kununua gari. Na bahati mbaya CAG hakumtaja mbunge huyo, kwahiyo si ajabu akawa Lijualikali 🤣. Hata hivyo chama kilifanyia kazi ushauri wa CAG kwa kumtaka mbunge husika arudishe gari hilo, na kwa sasa linatumika kwa shughuli za chama.

Halafu jambo la mwisho Lijualikali analopaswa kujua ni kwamba kuchangia chama si dhambi. Mimi binafsi si kiongozi lakini nimekua nikichangia mara kwa mara shughuli za ujenzi wa chama kupitia majukwaa mbalimbali. Nimewahi kupewa fedha na baadhi ya marafiki zangu (Friends of Malisa) just from nowhere wakaniambia "we kadeposit tu zitasaidia kununua hata bendera maeneo yasiyo na bendera." Imagine that spirit.!

Na sio mimi tu, wapo wengi wanaofanya kama mimi au zaidi yangu kwa sababu ni wajibu wa mwanachama kufanya hivyo (wajibu namba 2 kwenye kadi). Kila mwanachama anapaswa kuchangia gharama za uendeshaji wa chama.

Sasa najiuliza hivi mbunge unayeweza "kutengeneza" karibu 15M kwa mwezi unapata nongwa gani kuchangia just 500K kujenga chama chako? Kwanini roho ikuume? Unajua ni wangapi waliochangia kukufanya wewe kuwa mbunge?

Kuna watu waliamua wasile ili kile kidogo walichonacho wachangie kujenga chama bila kutarajia kulipwa. Chama kikakua na hatimaye umefanikiwa kuwa mbunge kupitia chama hicho. Kwanini roho ikuume unapoambiwa na wewe uchangie kidogo ili wengine wenye ndoto za ubunge kama wewe nao wafanikiwe kama ulivyofanikiwa?

Mbona ndugu yangu Peter umekuwa mbinafsi kiasi hiki? Si wewe uliyewasema wabunge wa CCM kuwa ni wabinafsi sana? Imekuaje kwako tena? Au kwa sababu unajiandaa kwenda huko kwahiyo unaanza kujifunza ubinafsi?

Anyway. Walioileta Chadema Kilombero mwaka 1992 unawajua? U were just 6 years old huwezi elewa labda kama ulihadithiwa. People suffocated bro. Walipambana kujenga chama, kwa jasho na damu. Na pengine wamekufa bila hata kuwa madiwani. Lakini walikujengea msingi ili wewe uje kuwa mbunge kupitia Chadema. Sasa na wewe ukichangia chama kule Newala nako akapatikana Lijualikali mwingine utapoteza nini?

Halafu hata huko CCM unakoenda sio kwamba hawachangii. Wabunge wa viti maalumu CCM wanachangia fedha kwa ajili ya umoja wao (UWT) lakini huwezi kuwasikia wakibweka wala kulialia kama wewe. Ni kwa sababu wana nidhamu na wanajua ni wajibu wao, lazima wautimize. Na wamekuwa wakifanya hivyo miaka yote. Ina maana umeshindwa hata na akina mama wa CCM? Jitafakari!!

Malisa GJ
 
Chadema acheni kujificha kwenye kichaka cha usaliti

Amkeni muangalie mlipokosea

Kumtusi lijualikali haiondoi mapungufu ya Chadema
 
Unajua wakati mwingine hata mbowe anaogopa kutoka kwenye uenyekiti kwa Mambo km hayahaya ya Juakali coz anajua akikiachia tu ndio chama kimekufa watu ni rahisi kurubunika. Ila nataman sn mwenyekiti ajaye wa chadema awe mwananmke hawa wanaume wa sikuhizi wanahongeka kirahisi mno. Asilimia kubwa waliounga juhudi ni wanaume, wanaamini chadema kunamaisha magumu hata huo upande mwingine nako kunamagumu yao wanayopitiaga kipind flani flani. Nasema ni afadhali awe mwanamke sio hawa wanaume wa sikuhizi kujiliza kwa mwanaume mwenzio km demu
 
Kwani wakati anajiunga hio katiba yao ya makubaliano ya kuchangishana ilikuwa likizo.Mbona anataka kuwa na tabia za waitara na katambi ukipata mpenzi mpya usimseme mabaya ex wako.Ashukuru hata amepata Mali nyingi nyumba,magari, viwanja nk ambavo mtaalamu afanyae kazi hawezi pata akistaafu.Ye kawekeza milioni 6 anavuna milioni 200 bunge likivunjwa
 
Unajua wakati mwingine hata mbowe anaogopa kutoka kwenye uenyekiti kwa Mambo km hayahaya ya Juakali coz anajua akikiachia tu ndio chama kimekufa watu ni rahisi kurubunika. Ila nataman sn mwenyekiti ajaye wa chadema awe mwananmke hawa wanaume wa sikuhizi wanahongeka kirahisi mno. Asilimia kubwa waliounga juhudi ni wanaume, wanaamini chadema kunamaisha magumu hata huo upande mwingine nako kunamagumu yao wanayopitiaga kipind flani flani. Nasema ni afadhali awe mwanamke sio hawa wanaume wa sikuhizi kujiliza kwa mwanaume mwenzio km demu
Njaa haina mwanamke au mwanaume
 
Tunaishauri Chadema ili isife Mkuu lasivyo hata October mtashindwa kusimamisha wagombea
Bia yetu jifunze kujenga hoja ndio hivo tu... kwa chuki zako dhidi ya CHADEMA huwezi kuishauri CHADEMA et isife nina uhakika ungekuwa na uwezo usaidia kwa 100% CHADEMA ife ili uwafutahishe waliokutuma, sasa maskini wa bia huna huo uwezo wala ushauri.. wanao tushauri tunawajua kwa majina na kwa sura sio ww, ww sio mshauri ila muuaji wa CHADEMA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila anayehama/kufukuzwa uanachama kuanzia enzi za akina Zitto! ukiondoa sababu zote ni lazima atamtaja tu Mwenyekiti! Hivi huyo Mwenyekiti naye siyo chanzo cha mgogoro kweli ndani ya Chama?
 
Back
Top Bottom