Suala la Wabunge kukatwa kodi si la kupuuza

Rwaz

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,968
3,319
Kuna mambo kama hatuwezi kuyakomalia basi hata mengine tuachane nayo. Maana yake hatujui tunataka kufika wapi! Suala la wabunge kukatwa kodi si la kupunguzia sauti. Si kwa mapato ya taifa tu bali pia kwa kuweka misingi bora ya elimu ya kulipa kodi.

Hivi mbunge anaombaje miundombinu na huduma Serkalini kama yeye halipi kodi? Je kwa watoto wake na jamii yake anapata wapi uhalali wa kuhamasisha walipe kodi?

Jamii yetu tukubaliane kulipa kodi si hiyari na ni kwa faida yetu. Mifumo ya kila raia kwa nafas yake kulipa kodi ijengwe. Bora mtu alipe kodi kidogo lakin alipe kodi.

Haiwezekani tusiwaze kutokuwa na bajet ya kujikopakopa. Tukikaa sawa kwenye kila raia kulipa kodi tunahamia kwenye matumizi bora na sahihi ya kodi. Kila mtu atakuwa na uchungu na kodi yake.

Nashauri serkali iwekeze kila ngazi ya kipato kuwepo kodi. kodi! kodi! kodi! Hata muuza kitumbua alipe kodi ya uwiano wake.

Leo hii mkulima wa mavuno ya mil 200 kama parachichi halipi kodi kwa uwiano wa mavuno yake lakin machinga wa mtaji wa mil 4 analipa kodi!

Elimu ya kodi, haki, rushwa na uzalendo viwe somo la msingi kuanzia chekechea!
 
Mradi ni msharahara wanapata lazima walipe kodi. Sijui kwa nini hawaoni aibu kupanga budget ya serikali na kuipitisha na kusimamia matumizi huku wenyewe hawalipi kodi.

Ingekua busara wabunge wenyewe wakalifikisha wenyewe suala hilo wakubali kwa hiyari yao kulipa kodi kuliko kusubiri hasira ya wananchi.
 
Back
Top Bottom