Suala la Umeme linafanya niwaze siasa

KAGAMEE

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
3,882
4,511
Mimi ni wale watu ambao hawajihusishi wala kujishughulisha na kitu kinaitwa SIASA. Ni mwezi sasa hapa nilipo kumekuwa na mgao mkali sana wa Umeme. Yaani ndani ya siku 30 naweza kuwa nimepata umeme siku 5 tu (Yaan ukiunganisha unganisha mgao kufikia masaa 120-5days).

Hii inanifanya nijiulize maswali ya kisiqsa kama ifuatavyo÷

1. Hii Nchi ina Rais?

2. Kama ina Rais anapenda watu wake wakae gizani?

3. Kama hapendi watu wake wakae gizani mbona hachukui hatua yeyote yupo yupo tu anawachekea wateule wake licha ya raia wengi kuumizwa na jambo hili?

4. Hii Nchi ina vyama vya upinzani?Mbona wapo kimya juu ya huu mgao mkali wa umeme?Where is Zito Kabwe,Mbowe,Lissu e.t.c?Ukimya wao unaashiria nini juu ya hili janga?

5. Hii Nchi haina wabunge wa kuwasemea wananchi wao?Je Raisi na wabunge washaandaa uongo wa kuwaambia wananchi kwenye uchaguzi mkuu 2025 juu ya hili sakata la mgao?Au ndiyo maana wanaogopa tume huru ya uchaguzi?

6. Je viongozi wa kisiasa kama Rais,Waziri Mkuu Wabunge e.t.c wanasali/wanaswali?Kama ndio hawaoni hatia kuumiza wananchi wao?Hawajui kama hivyo vyeo vinapita?.

7. Kuna maduka nayaona yamefunguliwa mtaani unaitwa JAZA. Unachukua betri na taa yake kwa 2500 per week. Je ni mradi wa wakubwa?

Hakika tutakukumbuka uncle.

Rest in peace 🙏
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom