Suala la tanesco kutaka ushauri toka kwa wananchi:- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suala la tanesco kutaka ushauri toka kwa wananchi:-

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kamkoda, Oct 12, 2012.

 1. k

  kamkoda JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 20, 2012
  Messages: 396
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nina mashaka kidogo na propaganda za shirika letu la umeme kutaka maoni kwa wananchi kwamba sisi tunataka shirika liweje. Kimsingi matatizo ya shirika hili ni ya kimfumo na kiutekelezaji ambapo inahitaji upembuzi yakinifu kwa maana kwamba ili mtu atoe ushauri elekezi stahiki...ni sahihi kwanza aingie ndani ya mfumo wenyewe uliopo austadi ndipo ashauri njia bora zaidi...Sijaelewa bado wao wana maana gani ama wanataka maoni ya kisiasa katika mambo ya kiufundi?...kuna makampuni makubwa sana ambayo yanaweza kuwapa ushauri wa kitaalamu kwa kutafuta suluhisho za kiufundi na kimfumo na ikawa ni suluhu ya moja kwa moja...Tanesco mkumbuke ushauri unalipiwa na si dezo dezo...ama ndio mnataka baadae mseme kuwa yalikuwa maoni ya wananchi mambo yatakapo kwenda kombo?...wekeni masanduku ya maoni kwa mambo ya huduma kwa mteja na myafanyie kazi. Leo nimeona kigamboni kuna nguzo zimefichwa sasa hata hilo mnataka maoni? Jisafisheni!!!...Mnalipwa mishahara na posho nzuri fanyeni kazi zenu muwe wabunifu nasi twafanya zetu!...sipati picha kila shirika la umma litakapotaka maoni kwa wananchi wakati si wana hisa!!!
   
 2. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani kama ulikuwa mawazoni kwangu. Sijui hawa jamaa hawajui maana ya business/management consultancy?
   
 3. S

  Sakula New Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hawa wanataka kucheza mchezo wa kuigiza , wanaelewa sana! kuwa Consultant wengi wlishatoa ushauri,
   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Siyo mbaya nawe ukawapa ushauri. Kuwa consultant siyo paka uwe na vyeti, inaweza kushauri kitu na kama kikifanyika, tunaenda mbali.

  Mfano mie nashauri wale wote waliohusika kulihujum wanyongwe, na wakinyonga hata wawili basi umeme utarudi kwenye nidham yake.
   
Loading...