Suala la Q Chila na madhara ya kupiga ramli

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,111
27,095
Alitoka kimuziki mwaka 2002 na wimbo wake " Ulinikataa". He was very big in the industry and he made a lot of money ( KWA viwango vya wakati huo)

Then baada ya miaka kadhaa akapotea hewani.

SABABU HALISI ILIYO FANYA Q CHILA AFE KISANII.

1. Alikuwa anatumia pesa zake vibaya bila mipango. Legend has it that aliwahi kupangisha nyumba kama tano KWA ajili ya michepuko.

2. Kibri na kugombana na wanamuziki wenzake mfano Jaffarai. Jaffarai alimualika CHILA afanye chorus ya wimbo wake baadae wakapishana kwenye malipo CHILA akaona suluhisho ni kuichukua hiyo chorus na kuitengenezea wimbo mpya akiuita ' my boo'. CHILA alijipambanua kama Msanii mwenye jeuri na kibri asiye weza ku keep urafiki na wasanii wenzake. So wasanii wengi wali m side line.

3. Dharau, jeuri na kibri KWA wadau wa muziki ( KWA maoni yangu hii ndio SABABU HALISI ya anguko la Q CHILA)

Legend has it that Q CHILA aliwahi kumzaba kibao Marehe Ruge Mutahaba ( Rest In Peace) jijini Mwanza or something baada ya show ya Fiesta. Kisa? Baada ya show Ruge alisema wasanii wote waliopanda jukwaani watalipwa kesho yake CHILA akasema yeye pesa yake huwa hailali nje then baadae issue ika escalate mpaka CHILA akampiga kibao Ruge.

Mimi Naamini hapo ndipo lilipo zaliwa anguko la CHILA kwenye muziki.

HE WAS BLACK LISTED

SOME YEARS LATER.

Ngoma za Q CHILA zikawa hazipigwi tena redioni.

Hakuna show wala simu ya show.

Hakuna endorsement.

Mwaka nenda mwaka rudi.

REACTION YA Q CHILA:

Kwenda KWA mganga kupiga ramli. Akaambiwa amefungwa.

Oga dawa oga dawa na wewe hakuna kinacho badilika.

CHILA akaona njia rahisi ni ku escape his problem through imagination, na kitu pekee kinge timiza hilo ni kuingia kwenye drugs.

CHILA akawa drug addict. Habari zikasambaa nchi nzima kwamba CHILA amekuwa teja.

CHILA ANA TUHUMU KUROGWA NA DIAMOND.

Mwaka 2009 Diamond Platnum anatoka kimuziki.

Mwaka 2013 Diamond akiwa juu sana kimuziki anahojiwa " kabla hujaingia kwenye muziki nani alikuwa role model wako?"

JIBU LA DIAMOND: Q CHILA.

Q CHILA ANATOA TAMKO KUHUSU DIAMOND KUMTAJA KAMA ROLE MODEL WAKE.

Miezi kadhaa baadae Q CHILA anasema AMEROGWA NA DIAMOND. Kwamba CHANZO CHA YEYE KUSHUKA KIMUZIKI NI KWA SABABU DIAMOND AMEIBA NYOTA YAKE. YANI ULE UKUBWA WA DIAMOND WA KIPINDI KILE ULIPASWA KUWA NDIO UKUBWA WAKE LAKINI HAKUWA HIVYO KWA SABABU DIAMOND AMECHUKUA NYOTA YAKE NDIO ANAITUMIA.


NSIO SABABU DIAMOND AMESEMA ALIKUWA ANAMUONA CHILA KAMA ROLE MODEL WAKE.



KITU GANI KILIPELEKEA CHILA KUTOA KAULI HIYO? CHILA atakuwa alienda kupiga ramli na mganga akaamua kucheza na akili yake na kumwambia Diamond ndio kachukua nyota yake (Kumbuka hiki ni kipindi ambacho CHILA alikuwa amekaa bila show ya maana KWA almost miaka mitano au sita hivi) Hii ina maana alikuwa na frustration na alisha kwenda kwa waganga kutafuta mchawi kumbe mchawi ni yeye mwenyewe.



REACTION YA DIAMOND: " SIWEZI KUIBA NYOTA YA TEJA"


KAULI ya CHILA dhidi ya Diamond ilizidi kumzika CHILA ktk ulimwengu wa muziki.

KWA sababu:

1. Diamond alikuwa anapendwa sana kipindi hicho kama Fei Toto alivyo kuwa anapendwa mashabiki ya Yanga. Kumsema Diamond vibaya kulisababisha aonekane hater wa Diamond lakini pia kilifanya mashabiki wa Diamond wamchukie CHILA.


2. KAULI ya Diamond " Siwezi KUIBA NYOTA ya TEJA " ilizidi kufanya CHILA azidi kupuuzwa KWA sababu ilithibitisha kwamba kumbe kweli CHILA ni teja, na teja ni mtu ambae hawezi kuaminika. Kampuni haiwezi kufanya kazi na teja. Hakuna kampuni yenye akili ingeweza mpa CHILA show wala ubalozi.

Ni kama vile Diamond aliwaambia wadau wa muziki acheni kufanya kazi na CHILA KWA sababu ni teja.

Isitoshe kitendo cha CHILA kusema kaibiwa nyota na Diamond tena hadharani kilionyesha yeye ni teja kweli kwa sababu mtu mwenye akili timamu asingeweza kuzungumza hivyo...

CHILA AJA NA MPYA MWAKA 2022.

Anasema SASA amekuwa Shareef Mganga.

Anatibu watu wenye matatizo mbalimbali.

Anaondoa vifungo n.k ( ,😂😂very funny wakati yeye mwenyewe anaonekana yupo kwenye kifungo)

Anasema amepewa mkoba na mizimu ya kwao ( ubabani)

Vita yake kuanzia kushuka KIMUZIKI HADI kuingia kwenye uteja inatoka KWA watu ubabani kwake KWA sababu hawakutaka yeye achaguliwe kupewa huo uganga ndio maana wakamtupia jini limkate mapema ILI huo uganga uende KWA mtoto mwingine ( wa ndani ya ndoa)

Ila pamoja na yote anasema tayari mizimu ya kwao imempa mkoba na.sasa yeye ni mganga kamili.

HAYO NDIO MADHARA YA KUPIGA RAMLI KWA WAGANGA.. OBVIOUSLY HII ISHU YA UGANGA NI MGANGA WAKE NDIO KAMWAMBIA KWAMBA ANA MAJINI WA UGANGA WANATAKA AWE MGANGA. NA KWAMBA NDUGU ZAKE WALIKUWA HAWATAKI APEWE UGANGA YEYE NDIO MAANA WAKAWA WANAMROGA ASIFANIKIWE NA NDIO SABABU YA KUSHUKA KIMUZIKI NA KUWA TEJA.

Watu wengi Wana amini CHILA amechanganyikiwa.

NDIO MAANA VITABU VYA DINI VINASEMA RAMLI NI HARAAM.
 
Duniani kuna watu hutumika km mfano na wengine hutakiwa kujifunza kwa wengine
 
Back
Top Bottom