Ndugu wanajamii forum, hivi sasa tupo ndani ya nchi yetu ya Tanzania kama hatupo, maana viongozi tuliowaweka madarakani wanfanya watakacho nasi tumebaki tukilalama bila mafanikio. Kwani hatuna cha kuwafanya maana teyari wameshashikiria mpini nasi tupo kwenye makali. Nayasema haya kutokana na matukio ya hivi karibuni au yanaendelea mpaka sasa ndani ya hii nchi yetu. Yapo matukio kadhaa lakini naomba nielezee haya;
Posho za wabunge
Licha ya wanachi waliowengi kulalamikia kitendo cha wabunge kujiongezea posho, lakini wawakilishi hao wa wananchi bado wameweka pamba masikoni bila aibu wameshikilia tama zao za fedha bila kuwajali waliowachagua na jana 31 jan 2012 Waziri Mkuu mh Mizengo Pinda akatangaza kuwa posho hizo zimeongezeka naye Spika wa bunge akathibitisha kuwa rais Jakaya Kikwete ameshasaini muswada wa posho na sasa ni sheria kuwa wabunge walipwe posho hizo mpya wanazodai. Kwa hesabu za haraka haraka kwa mwaka mmoja tu posho za wabunge (ukiondoa mishahara yao, posho za vikao vya kamati, posho za semina wakati wa wikiend, gharama za mafuta, mchango wa maedeleo ya jimbo) zinafika karibu bil. 12,474,000,000/=. Hapa nimechukua wastani wa siku mia moja wanazotakiwa kukaa bungeni kwa mwaka mzima( wiki 3 mwezi February, wiki 3 mwezi April, wiki 3 mwezi October na siku 72 kwenye bunge la bageti mwezi June ukatoa wikiendi zote). Hizi ni gharama za vivuko viwili kama cha mv. Magogoni. Hapa najiuliza hawa wabunge wanania ya kweli kumtetea mwananchi?
Utetezi wa posho
Kwa kuzitetea posho hizi walijitokeza Spika na naibu wake pamoja na waziri mkuu ayejiita motto wa mkulima.
Katika utetezi wake Spika wa bunge Mh. Anne Makinda alisema poshohizo zimeongezwa kutokana na gharama za maisha pale Dodoma kupanda ikiwamo gharama za hotel, hata hivyo wamiliki wa hotel hizo wakajitokeza na kukanusha gharama hizo lakini bado spika akang'ang'ania msimamo wake.
Waziri Mkuu Mh. Pinda nae aksema wabunge huwapa wapiga kura wao fedha mara waendapo kuwalilia shida zao na hivyo haoni kama kuna ubaya wakipandishiwa posho hizo, kwangu mimi huu ni utetezi wa motto wa darasa la pili au la tatu maana sizani kama wabunge huchaguliwa ili wawe wasamalia wema kwa kugawa hela kwa walio na shida.
Naibu Spika yeye ndo alitoa mpya pale alipotetea posho hizo kwa kuzilinganisha na wafanyakazi wa idara nyingine kama uhamiaji, mahakama, TANAPA na TRA. Hapa napo nilibaki hoi maana njuavyo wabunge si wafanyakazi mpaka walipwe sawa au zaidi ya wafanyakazi. Ubunge ni wito (Sio kama wa waalimu, wauguzi au wanajeshi) hivyo sioni sababu ya wabunge kujilinganisha na wafanyakazi wakati ubunge sio ajira, Kwa wbunge wetu wa leo ubunge wanaona kama ajira wakati sio kweli. Na wala hawalazimishwi kuwa wabunge wakitaka waache kama gharama za kuutumikia ubunge ni kubwa. Hivi bila wabunge hatuwezi kuishi?Utetezi huu kwangu ni dhaifu kiasi kwamba inaonekana kama matusi kwa wananchi, kwani tunapewa sababu yoyote ilimradi kuna ufafanuzi kwani hatuna cha kuwafanya hata wakitekeleza matakwa yao.
Mgomo wa madaktari
Mwanzoni nilikuwa nasita kuunga mkono kwa umesababisha madhara makubwa kwa wananchi na niliona madaktari wanawatumia wananchi kama chambo ya kupata mahitaji yao! Lakini kwa hili la wabunge na madaktari nao walistahili kugoma. Serikali kila siku haina hela lakini ikifika kwa wabunge hela zinapatikana hapa nashangaa, kwa madaktari haina hela kwa wabunge zipo! Haya ni mambo ya firauni kabisa kabisa.
Mgomo huu navyoona hautafanikiwa kwani serikali kwa kujikosha itawapa nyongeza kidogo na sio kama walivyoomba mshahara wa mil 3.5 kwani inaonekana wananchi tumegawanyika wapo wanouunga mkono na wapo wanaoupinga kwani wanaonakama wametolewa kafara kwa madai ya wengine.
Maslahi ya wafanyakazi
Kwa mtazamo wangu wafanyakazi karibu wote wanamadai yanayofanana sijui wa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama maana hawa ndo huwalinda hawa viongozi serikalini na wala hawajawai kugoma wala kulalamika inaonekana kwao mambo ni mtelemko, lakini kwa kada zingine kama waalimu, manesi, madaktair,mahakama, TRL na wengineo wote madai ya mishahara na posho ni yaleyale. Kinachowashinda mpaka kila siku wanalialia ni utengano wao katika kudai hizo stahiki zao, mara utasikia leo waalimu, kesho TRL( ingawa siku hizi siwasikii tangu katibu wao Sylvesta Rwegasira afariki), kesho kutwa utaskia madaktari. Hivyo utengano wenu ndiyo unawanyima haki zenu. Siku zote najiuliza je hawa wafanyakazi hawana chama kinachowaunganisha? Na kama kudai kwanini wasidai kwa pamoja? Hebu tujiulize kama mahakama,walimu, madaktari na wengine wote wagome kwa pamoja serikali haitatikisika na kuwasikiliza? Lakini mkigoma madaktari tena wa muhimbili wataletwa wanajeshi kama kawaida.
Yangu ni hayo kwa leo hebu tujadili kidogo kwa hili wanajamvi.