Suala la posho - Nkamia na CCM wengine kuwa na aibu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suala la posho - Nkamia na CCM wengine kuwa na aibu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Barbaric, Jan 2, 2012.

 1. B

  Barbaric Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Niliusikiliza kwa makini sana mjadala wa posho za wabunge A.mashariki na kati uliokuwa unarushwa hewani na radio bbc, nilishikwa na bumbuwazi nilipokuwa nasikia hoja za utetezi za nkamia kuhusu posho.
  Hoja ya kuwa zito amepokea posho bunge lililopita kwa nini sasa anakataa.
  kwa msomo na mwanahabari wa cku nyingi kama nkamia ni aibu, kama yeye haoni aibu mimi naona aibu kwa niaba yake, inamana alishindwa hata kujiuliza kwamba, KAMA MTU ALIKUWA MWIZI KWA KUDHAMIRIA AU KUTOKANA NA MAZINGIRA, AMEAMUA KUACHA, UNAWEZA KUMUULIZA KWA NINI UNAACHA WAKATI UMEIBA MIAKA YOTE? INA MAANA KWA MTAZAMO WAKE, UZOEFU UNAHALALISHA MAOVU.
  Hoja ya kwamba kuna chadema wanazitaka ila tu wanafuata mkumbo.
  Hilo nalo halifanyi posho kuwa halali kwa sababu kutozitaka posho watu wengine hakugeuzi mitazamo ya watanzania wengi kuhusu posho, na nina hakika naye nkamia hajawaohoji wabunge wote wa ccm ili wampe mcmamo wao kuhusu posho, nina hakika wapo wanaozipinga ila wanaogopa mkate wao kuingiwa mchanga 2015.
  KWA KIFUPI MSOMI NA MWANAHABARI KAMA JUMA NKAMIA HAKUSTAHILI KUTUMIA HOJA HIZO, WENDA ANAWEZA akawa na hoja ZA MCNGI KUHUSU POSHO LAKINI NAMSHAURI ATUMIE HOJA ZENYE MSHIKO KWANI ANAZOTUMIA ZINAMDHARIRISHA.
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  hawa watu ni walafi sana aiseeeew
   
 3. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  aliupania Ubunge hivo kaingia na kuanza kushabikia posho kwa kutaka hela za haraka haraka bila kujali kipato cha wapiga kura wake nacho kinaongezeka ama kinabaki palepale
   
 4. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  shibuda kasema hivi,viongozi wa ccm na wanachama wake ni wachumia tumbo
   
 5. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Siyo kila mbunge ana uwezo wa kudadafua mambo; Juma Nkamia uwezo wake wa kufikili na kudadafua mambo ndo umefikia hapo, tusimlaumu sana.
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ndo mana wapo bungeni
   
 7. Rocket

  Rocket Senior Member

  #7
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani huyu naye ni kati ya wabunge wenye njaa kweli,ni mropokaji kila anapochangia bungeni
   
 8. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,379
  Likes Received: 691
  Trophy Points: 280
  kinachonishangaza mimi hawa jamaa hawajui hata wanadai nini? hawaelewi kiukweli hawastahili hata hiyo posho ya 70,000
  kama maisha magumu si waombe per diem ziongezeke? ambazo zinahusisha kupanda kwa maisha, hawataki ziongezwe per diem kwa kuwa wengine watapata. vile vile ieleweke fedha inayotolewa kwa ajili ya vikao sio ya kufanyia mambo mengine ni gharama za vikao sasa ukishaingiza matumizi mengine yatakusumbua? hivi ni nani aliwaambia mdanganye wapiga kula wenu? nani aliwaambia mkope magari ya gharama kubwa? nani aliwaambia muongeze nyumba ndogo japo hili hamlitaki sasa zitatoshaje? taabu kwelikweli
   
 9. Kahise

  Kahise Senior Member

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 144
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu, wanasiasa jamii ya Ngamia wanajionyesha jinsi walivyo malimbukeni. Kumbukeni msemo wa kiswahili wa masikini akipata............. Hivi wanaotunga sera hizi ni watanzania kweli. Diwani wa Ngamia anapata posho ya mwezi laki moja na elf 20. Kati ya mbunge na diwani nani anafanyakazi zaidi za maendeleo? Wabunge haohao wameshindwa kuwatetea madiwani wao, bado wataka kuendelea kuwakamua watz, ni aibu ya hali ya juu. Mshahara wa mbunge mmoja unalipa madiwani zaidi ya 60, is there equality?
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  posho ziongezwe hadi kufikia laki tano na ziitwe ujira wa mwia......

  hapa nina mialiko 27 ya wananchi,yote inataka pesa kama posho hazitaongezwa mimi ntazitoa wapi pesa za kwenda kuchangia?
   
Loading...