Suala la Kujichukulia Sheria Mkononi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suala la Kujichukulia Sheria Mkononi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Aug 23, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu jana Kuna tukio nimeliona Mtaani kwetu muda wa usiku wakati narudi nyumbani mpaka saa hii nashikwa na mashaka sana kuhusu usalama wa raia na mali zao maeneo kadhaa nchini haswa yale ambayo yanawatu wengi na utamaduni huu wa kuchukuwa hatua mkononi unavyozidi kushamiri na watu wanapoamua kusingizia vitu kwa ajili ya maslahi yao wenyewe .


  Hiyo jana nilikuwa naelekea nyumbani kwa bahati nikasimama sehemu kuongea na mtu mmoja mara nikaona kundi kubwa la watu likimleta kijana mmoja huku akipigwa kwamba ni mwizi walipopita karibu yangu ndio nikamwona mtu mwenyewe na ndio nikakumbuka kumbe namjua ikabidi niende na mimi polisi .


  Kufika polisi wakamweka chini na ndio mama mmoja na motto wake pamoja na mumewe wakafika hapo na kusema kwamba mtoto wao amegongwa na huyo jamaa halafu akajaribu kikimbia wale wananchi wa mtaa huo wakaanza kumpiga na kumwita mwizi bahati nzuri baadhi ya watu wa mtaa wa pili walimuokoa kwa sababu walikuwa wakimjua .


  Nilipojaribu kumuuliza maswali akaniambia yeye hakugonga mtu lakini huyo mama aliteleza na mtoto wake wakajipiga kwenye gari lake wakati anaendesha mtaani hapo lakini vijana wa mtaani wakaanza kumrushia mawe na kumwita mwizi ndio akaamua kukimbiza gari kupeleka nyumbani alipofika hapo geti likawa limefungwa akaondoa gari hapo kwenda sehemu nyingi kwa nyuma ili apaki ndio hao jamaa wakawa wameshamzunguka na kuanza kumpiga huku wengine wakichukuwe vitu kwenye gari pamoja na kumsachi .


  JAMBO LA KUSIKILISHA ZAIDI
  Huyu jamaa wakati anapigwa na raia wenye hasira ndugu yake mmoja alikuwa hapo nje huyo ndugu yake akafiri ni kweli mwizi anapigwa akapuuza na kwenda zake ndani kumbe ni ndugu yake tena kaka yake watu wengine wa mtaani kwake nao wote walifikiri ni mwizi kwahiyo hawakuingilia wakaacha raia wenye hasira wafanye walichokuwa wanafanya ( hawa raia walitokea mtaa wa pili ambapo dereva alikutwa na mkasa na mama watoto )


  KILICHOFUATA
  Baada ya kuletwa polisi kwa kuwa niliweza kumtambua na yeye kunitambua kwa mbali nilimpigia dada mmoja simu ambaye ni mfanyakazi mwenzake ndio akaweza kutaarifu wengine ili waweze kufika eneo hili lakini wakati huo polisi pamoja na jamaa wengine walikuwa wameshamfunga pingu kwa ajili ya kwenda kwenye eneo la tukio kuangalia gari lake ili aweze kupelekwa Ubungo kwa askari wanaohusika na usalama barabarani .


  Gari lake lilikuwa zima sema kuna vitu vingi vilikuwa vimeshachomolewa na watu waliomtuhumu wizi majina na mahali watu hao wanapokaa yalitajwa ni watu wa mtaa wa pili tu , huko njiani pia ndio tulikutana na ndugu zake wengine ambao aliwaacha bar wanakunywa na mwisho kabisa ni Yule ndugu yake aliyeona mtu anapigwa akapuuza .
   
 2. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,205
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Mshahara wa polisi ni bei gani hasa, ili iweze kumwezesha kufanya kazi kitaaluma? Wameamua kuwaachia kazi wabuya unga wa mitaani wanaowaita polisi shirikishi. Wakijua ya kwamba haitawagharimu kusumbuana na wahalifu mahakamani, kwani wale wanaowaita raia wenye hasira kali watakuwa wameshasimplify kazi kwa kuchoma moto. Mimi nimetembea nchi zote zinazotuzunguka na nakuhakikishia kwa wakati huu uliopo hakuna raia wa nchi wenye kiu na shauku ya kuua kama Tanzania. Taifa lenye midomo inayomtaja Mungu bali wakimchukia na kumkana kuliko wengine. Na hii huenda ikawa imechochewa na uongozi usiozingatia maadili ya kiuongozi na tamaa ya kuwa mabilionea kwa kipindi kifupi cha utawala wao. Mungu irehemu Tanzania.
   
Loading...