Suala la baadhi ya viongozi wa kisiasa kutafuta hifadhi za ukimbizi ubalozini, mashirika ya wakimbizi ni "Cover Story"

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,039
3,486
Wakuu,
Limeibuka wimbi la baadhi ya viongozi wa kisiasa kukimbilia kwenye balozi zinazowakilisha nchi zao au mashirika ya ukimbizi kwa madai ya kuteswa (persecution). Kwa tafsiri ya jumla kwa kiingereza inaakisi yafuatayo: "...... is the act of harassing or oppressing a person or a group of people, especially because of their identity. Throughout history, people have faced persecution because of their religion, race, ethnicity, political beliefs, sexual orientation, and many other factors. ........ "

Hili suala lisichukuliwe juu juu kutokana na historia ya aina ya viongozi husika na malengo yao; hivyo kwa maoni yangu kama raia nashauri Serikali iwasiliane na taasisi ambazo zinawapokea wakimbizi hao kwa kuzingatia sheria za kimataifa, kidiplomasia, sheria za nchi na utamaduni kupitia wazee na viongozi wa kiroho ili kubaini sababu halisi kuliko hizi zinazotolewa na ufumbuzi utafutwe haraka iwezekanavyo kuepusha Taifa kuingizwa kwenye mfarakano wa kijamii, kiuchumi na kimahusiano na mataifa mengine.

Inatakiwa utafutwe ukweli ni akina wanawatishia hao viongozi wa kisiasa, kwanini na malengo ni yapi.

Sina uhakika kama Tanzania kuna hali ya hatari kisiasa endapo wahusika hawavunji sheria ambapo hata hivyo si kigezo cha kutishiwa. Serkali msifumbie macho kwa maana haba na haba hujaza kibaba mwishowe kunaweza kutengenezwa vikundi vya uasi na ugaidi na kuhatarisha wananchi wasio na hatia kwa sababu za wachache wanaotafuta kupata mamlaka ya utawala wa nchi kwa nia OVU.

[The great thinkers of this renowned transparent fora are solemnly appealed to thrive with constructive arguments to mend tthe ongoing animosity segragation which a few individuals are determined to plunge the nation into civil unrest without apparent and justifiable reasons to advance the longed ambitions at hooks and crooks.]

Nawasilisha
 
Hio issue kwa muelewa alie vizuri kichwani na asiekuwa na pande yoyote (Sio CCM wala UPINZAN) hawezi kusema ni "COVARAGE STORY", atasema either ni "TACTICS au REALITY/UHALISIA" ndio maana Mashirika Ya Wakimbizi kuingilia kati.

Serikali haina mtazamo kama unaosema, yenyewe imesha jihakikishia "UTAWALA NI WAO", piga ua. Ila wana "MISJUDGE" consequences zake. Kenya wameamka ndio maana wakamuachia Godbless Lema huru na aendelee kwenda Nairobi bila pass yoyote kuomba hifadhi (Wanajua outcome yake kama wangemrudisha Tanzania then akakamatwa au kuuliwa - wao ndio wangebeba mzigo wa lawama).

Kama ni tactic inatumika na upinzani kupata "POINT" ya claims zao za serikali kutumia mabavu na wizi kwenye uchaguzi (Trust me, itazoa point nyingi in favor kwa upinzani kutokana na matendo yaliofanyika katika uchaguzi mkuu 2020 - Ndio maana mashirika hayo yameingilia kati haraka sana).

Na kama ni "REALITY", basi ndio uhalisia wa mambo yanayofanyika na mikakati inayopangwa dhidi yao. Na dunia itaamini kutokana na "SERIKALI KUWA KIMYA".

NB: Mtu ambae ana "TABIA" fulani iliozoeleka/inayoaminika kwenye matendo yake, hasa matendo mabaya ya kupoteza/kuua/kufunga/kufilisi/kutesa/ubabe, plus kuzima mitandao na kufatilia simu za raia basi posibility ya "REALITY/UHALISIA" ni 100%, na hata kama anasingiziwa basi dunia bado itaamini kwa 100% kutokana na mazoea aliojiwekea.

Na kama sio reality, basi hio "TACTIC" ina draw attention dunia nzima yaliofanyika/yanayofanyika ndani ya nchi (Ukizingatia kuna maombi yameshafanywa Mahakama Ya Jinai Ya Kimataifa kuwajibisha viongozi kwa yaliotoke kwenye uchaguzi 2020). Hii italeta mashiko na umuhimu ya maombi yale yatazamwe kwa jicho la tatu na kufanyiwa kazi (UN na ICC wasipoyafanyia maombi yale kazi then likitokea la kutokea kwa kiongozi yoyote wa upinzani kuuliwa/kupotea, wao ndio WATALAUMIWA kwa kudharau kufanyia kazi maombi yale).

*Hata ikitokea upinzani wakamtoa "KAFARA" kiongozi mwenzao, dunia itaamini serikali ndio wamefanya.

*Serikali bado imelala, ila kwa waelewa wa maswala ya international politics, mpaka sasa "UPINZANI 2 - 0 CCM". Wengi watapinga kwasababu athari haijaanza kutokea moja kwa moja. Ila yajayo yatafurahisha sana.
 
Hili pia litabuma!

Seif alitwambia kafika hadi UN,
Lisu yeye tukaambiwa kwa vile kahojiwa hard talk basi haki itakuwa mbaya sana.

Msichokijua ni kwamba, huko wanakotegemea watapata msaada wao wenyewe wapo hapa hapa nchini na wanaona kila kitu. Na wao wapo kwa faida siyo kwa ajili ya kina Lema.

Kiufupi hiki wanachofanya kina Lema watakuja kujiona wajinga sana baadae.
 
Haya sio ya kupuuzwa kweli kama unavyosema,pia kwa sasa sahauni wawekezaji wapya kuleta pesa zao kuwekeza
 
Watanzania wengi sana wangekuwa na uwezo wa kukimbilia nje ya nchi wangekimbia.

Wewe nchi gani unaminywa uhuru mpaka wa kikatiba?.

Kazi za manati na kujuana.

Ukichakalika upate kibiashara chako ukitangaze mtandaoni, mpaka mtandao unaminywa.

Ukisema utumie VPN, kutumia VPN ni kosa.

Ni basi tu watu wana hulka ya hewala hewala na funga bakuli mwanaharamu apite.

Hao viongozi wa upinzani wote wakikimbia nchi siwezi kuwashangaa wala kuwalaumu.
 
Sasa ni muda mzuri kwa baadhi kuwa na akili timamu na kuwa wakweli.

Ndugu zanguni, hawa wanajifanya wanakinmbia Nchi ni waongo tu.

Lengo lao ni kutaka kuuaminisha Ulimwengu kwamba Tanzania si Nchi salama tena kwa kuishi.

Ebu jiulizeni, miaka 5 iliyopita wamekuwa wakitukana Viongozi wa Serikali lakini hakuna aliyewatisha mpaka wakakimbia Nchi.

Wakati wa Kampeni za Uchaguzi mkuu 2020, wamekuwa wakitukana matusi ya kila aina, lakini hakuna aliyewatisha mpaka wakakimbia Nchi.

Leo Uchaguzi umekwisha, mshindi kapatikana, kwa akili ndogo tu, utamtishaje mtu aliyeshindwa? Utamtisha wa nini?
Haya ni MAIGIZO, MAIGIZO, MAIGIZO, MAIGIZO.
 
Acha kutupumbaza akili sisi sio wajinga kama hao wasio tumia akili kwenye siasa. Siasa imewashinda hao na katu usijifunze kwa watu walioshindwa. Wanafanya siasa kimihemuko bila kutumia akili sasa wamebaki kukimbiakimbia tu. Hofu imewajaa tu kwa mambo ya kijinga wanatesa familia zao. Siasa ni mchezo inatakiwa uucheze kama Mpira kwa tahadhari kubwa sio unacheza cheza tu hadi rough ili ufumbiwe macho.
 
Back
Top Bottom