Stress

Amateur

Member
Apr 18, 2011
34
5
Naomba kuuliza mnisaidie kumshauri rafiki yangu ambaye ni ofcmate wangu. Yeye ana mume na wana mtoto mdogo kwa sasa wa miaka miwili ( huyu ni mtoto wao wa tatu). Toka alipoconceive huyu mtoto wa tatu mpaka leo mume wake hataki kufanya nae tendo la ndoa. Hii mimba ya 3 mume ndio alidai sana kwamba anataka mtoto wa kike maana walikuwa na boys tu, na kweli akapata mtoto wa kike. Anadai ana stress nyingi. Mke anafanya ku beg mpka sasa anadai ameacha ku beg maa anaona kama anadhalilishwa. Siku nyingine akiomba mume anakuwa mkali na anamnunia for months. Anasema bado wanalala kitanda kimoja but no sex! She is very desperate na hajui afanyeje na mume hataki kabisa mazungumzo. Naombeni ushauri maana alivyonieleza nikamwambia ngoja nilifikirie pia najua hana muda wakusoma jamiiforums ndio maana nalileta kwenu mnisaidie.
 
Duuu hii ni kali aisee, na nina shawishika kuamini kuwa kuna kitu ambacho kimetokea ndani ya wanandoa hao ambacho kimemfanya mwanaume huyo kuwa kama alivyo - Hakuna marefu yasiyo na ncha- Si jambo la kawaida mwanaume kususia hiyo kitu na kwa kuwa imetokea, basi ni vzr huyo dada kuzitafakari njia zake na mwenendo wake.

Pia kwa asilimia ndogo sana kama kweli hakuna ugomvi wowote ndani ya ndoa, inawezekana huyo mwanaume akawa
1. Amepata nyumba ndogo na hivyo hana hamu na mkewe
2. Frustration za kazini
3. Minong'ono juu ya ukweli kama huyo mtoto ni wake au la

Mpe pole na mwambie ajitafakari kwanza ....

HP.
 
Je wewe ni He?
Kama ni He soma alama za nyakati basi kama huwezi hata utabiri wa hali ya hewa waweza kukusaidia.
 
Kitu alichoniambia ni viwili, kimoja ni kwamba mume wake yuko stressed sana kazini na huwa anachoka sana. Alikuwa anatafuta kazi na mkewe alikuwa pia anajaribu kumsaidia kuna wakati alitaka hata kuresign bila hata kupata kazi sehemu nyingine. Hivi sasa ana mwezi mmoja tu kwenye kazi yake mpya na sasa hata yeye anakiri yuko more relaxed. Kingine alichonigusia ni mume wake anaona kama hamridhishi. Mke anadai alishamwambia kwamba yuko fine lakini mume anadoubt. Mazungumzo hayo yalikuwa yanafanyika hapo zamani wakati mambo yako shwari lakini sasa hathubutu kukumbushia. Bahati nzuri watoto wote wanafanana sana na Baba tena copyright huulizi. Mimi nina langu ambalo siwezi kumuueleza ni kwamba mkewe ni mzuri tena sana na anamvuto sana kuanzia sura, shape and dressing pia anauwezo. (Sijui kama kampita mume wake) Ila yuko well off hata ndungu wa mmke wako vizuri. Labda mume anafeel inferior??
 
Inawezekana Bwana HP umesema sawa, Ila kwenye Ndoa kuna mambo mengi,
Inawezekana jamaa kapimwa kakutwa hana uwezo wa kuzalisha , sasa ana watoto watatu, hiyo ni shida

au Kampima HIV status yake kaona anamaambukizi, anatafuta jinsi ya kulisema home

Pia inawezekana amepata story za Mama ku cheat na mtu ambaye afya yake si njema

Kwenye Ndoa Tuombe Neema ya Mungu Tufike salama
 
1. ndoa bila tendo la ndoa kwa muda mrefu maana yake ndoa hapo haipo
2. Maadamu ni wana ndoa na wana watoto watatu wawe wawazi ili kumaliza hilo tatizo kwa manufaa ya hao watoto
3. Wajibu wa tendo la ndoa ni wa kila upande tena hasa wanaume manake sisi tukigongewa roho inatuuma sana kwa hiyo ni muhimu kutimiza hilo tendo ili kupunguza mazingira kugongewa.
4. Kama mwanaume aiendelea kugoma kutoa huduma aangalie njia muafaka na salama ya kupata hilo hitaji la mwili bila kuathiri familia.

ngumu sana kwa mtoto wa kike kukaa bila ile huduma, ngozi inanyauka.. machunusi kibao...

tafakari...........
 
Kwenye ndoa kuna mambo mazito kweli kweli. Isije ikawa kuna maugomvi mazito huko. Atafute mtu wa kumpiga upin tu(joke). Mpe ploe
 
Hana lolote huyo mwanaume ana lake jambo alikuwa anamtaftia sababu kwan yeye dada ndo mungu kwamba anapanga azae gal o boy.mungu nsamehe si bora amkacrikie mungu maana yy ndo mpangaji wa yote
 
nachoweza kumshauli huyo dada kwanza atafakari kama kuna kikwazo cha aina yoyote upande wake au wa mume akishagundua tatizo amshirikishe mungu kwani yeye anaweza yote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom