Stress! Stress! Jamani watanzania je huu sio uonevu.

mdida

JF-Expert Member
Jul 14, 2011
1,607
772


UFAFANUZI KUHUS FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.
[FONT=Arial,Arial][FONT=Arial,Arial]Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.
1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.
2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.
3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.
4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.
5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia
[/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]2
[/FONT]
[/FONT][FONT=Arial,Arial][FONT=Arial,Arial]wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika
6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.
7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu
8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.
9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo. Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.
Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.
Wenu.
[/FONT]
[/FONT]Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii
[FONT=Arial,Arial][FONT=Arial,Arial]Irene Isaka
[/FONT]
[/FONT]MKURUGENZI MKUU
 
kaka the boss ina maana kuwa kama wewe unafanya kazi either kiwandani au mgodini, kama ukiacha kazi may be unamaliza miezi sita unachukua mafao yako, sasa hiyo hakuna mpaka ufikishe miaka 55 au 60.
 
its a dumb decision. wrong forum too, put this in the law section

EDIT: ukifukuzwa kazi jee? utalipwa mafao au hadi 55/60
 
Katokea wapi huyu? Kwanza title haiendani na alichokiandika. Pili hapa si mahali pake! Mod. Ondoa hii kitu haraka sana!
 
Iyo pesa ya kwao ama ya mfanyakazi siwaelewi:sleepy::sleepy:
 
Hayo nayo ni mapenzi? Situnataka kupumzika bhana hapa si mahali pake peleka hizo habari sebureni huku tumelala.

Lakini irene nimependa mwandiko wako!
 
hawa wa...nini nani ana garantee ya kuishi miaka 50/60 kwa maisha ya sasa au ndo wameamua kutuibia pesa zetu kwa nguvu, hopeless decision yaliyojaa na wizi mtupu,
 
waseme yooooote, mradi nikicha kazi pesa yangu wanipe yote.

Ndio hivyo huipati tena! Duh, yaani nilishaanza kuipangia na project kabisa.

Sawa nitakopa nyumba na kuiuza if that is the case. Very stressful indeed!
 
Yaani Kaunga, nimepanga acha kazi mwezi wa tisa
Nitumia NSSF kwa mambo yangu leo waichukue??

Am too old kuajiriwa now na mshahara wa laki na nusu.

Ndio hivyo huipati tena! Duh, yaani nilishaanza kuipangia na project kabisa.

Sawa nitakopa nyumba na kuiuza if that is the case. Very stressful indeed!
 
Yaani Kaunga, nimepanga acha kazi mwezi wa tisa
Nitumia NSSF kwa mambo yangu leo waichukue??

Am too old kuajiriwa now na mshahara wa laki na nusu.

Yaani mwenyewe nilijipa mwisho Dec, kama ni kweli wametuweza. Itabidi niongeze Mwaka mmoja while saving like chizi!
 
Back
Top Bottom