Strategic spinning na upanzi wa fikra katika jamii ni hatarishi kwa udumavu wa nchi

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,411
11,061
Habarini nyote.

Wasilisho la Wadiz a.k.a Baharia

Kipimo cha jamii na nchi ni pamoja na akili za watu hasa katika nyanja ya kumbukumbu na kujadili mambo yenye tija kwa kirefu.

Sambamba na hilo kinyume chake jamii na nchi dumavu hasa kifikra na dira za kimaendeleo hudekeza usahaulifu ama wanakosa akili pevu zenye kumbukumbu thabiti katika maisha yao.

Jamii na nchi za namna hio watu wake na viongozi wake hupenda sana maisha binafsi na si wenye kutilia maanani nguvu ya ujumuifu wa mambo kwa ustawi wa jamii.

Wivu, ubinafsi na uchoyo endelevu ni janga kubwa kwenye nchi yoyote dumavu hasa katika lishe ya fikra.

Hivyo ipo namna jamii hio hupambazwa ili iwe sahaulifu kwenye fikra, agenda na mikakati ya msingi ya kimaendeleo kwa jamii au nchi kwa ujumla wake.

Nayo hio namna au kanamna hufanywa kuhuishwa na siasa za chombezo, mbwembwe, vioja kama sehemu muhimu ya kupoteza mawimbi ya fikra kumbukizi na watu hafifu kwenye kumbukumbu hasa nyakati wanasiasa, watawala, viongozi hupitia jambo gumu au wamechemka pahala fulani.

Yaweza kuwa kiuchumi, kijamii, kiungozi, kisiasa, kisera, muongozo au utendaji.

Hii iitwayo strategic spinning ipo katika namna nyingi mfano, viongozi kuja na kauli za vioja, vichekesho, katuni za matamshi katika kuhadaa jamii kuhama kwenye fikra msingi na huishi katika ustawi wa nchi husika.

Pia viongozi ama watawala wanaweza kuweka mkazo na nguvu ya matumizi katika mambo yasiyo msingi na kurusha pesa kwenye jambo furahishi kwa jamii husika ili kupooza fikra na kumbukumbu za maswala moto kitaifa.

Yaweza kuwa mkazo katika burudani, starehe,kunena vioja vyenye mvuto kwenye masikio ya wapofu na dumavu wa fikra na watenda dhambi furahishi kwenye mioyo yao zisizoleta ustawi jumuishi.

Watu hawa huweka kisogo ustawi jumuishi na uchanya na utekelezaji wa sera, sheria, kanuni, miongozo, taratibu kwa mawanda mapana ya ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla. Watu hawa hufanya kwa niaba yao na kikundi chao.

Sisi kwanzo wao baadae na hata kama hio baadae ikiwa ni sisi wenyewe nayo sawa.

Katika taifa lolote mambo msingi kwenye fikra na mijadala yakidumazwa na kutopewa kipaumbele ni sumu endelevu kwenye angamizo la maendeleo ya watu na vitu.

Watu wenye kumbukumbu, kujadili kwa kina mambo msingi bila kusahau au kukubali kusahaulishwa ni wa muhimu kwa maslahi ya taifa husika.

Awaye yeyote ajuaye ya kwamba umsahaulifu haogopi kukulisha uongo, kukudhuru, kukuhadaa, na kutokupa haki zako msingi kwa maana msahaulifu si mwenye kuvuna tija ya utimilifu wa kutendewa meema na akajali na hachukui hatua kwa maana hata hatua si sehemu ya maisha yake.

Nichukue fursa hii kuwakumbusha ya kwamba msahaulifu au anaekataa au jamii inayoacha ama kusahau kujadili kukemea pasipo kusahau mambo msingi huchimba au hujichimbia shimo ama kaburi lake au lao wenyewe.

Tusiwe wepesi wa kusahau au kukubali kusahaulishwa mijadala au fikra kwenye mambo msingi.

Kujikosoa ni heri ikiwa hivyo iende na mabadiliko ya sera, sheria, kanuni, taratibu na miongozo kukidhi haja ya sasa.

Kelele zozote zaweza kuwa ni chanya au hasi kwa mtazamo wa muda, sehemu, wahusika na utamaduni wa jamii husika.

Nawasilisha

Wadiz a.k.a Baharia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom