MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,591
Vijijini kuna mambo sana,
1:Unakuta mtu kafa kwa kichocho lakini anatafutwa nani aliyemroga.
2: Kuna baadhi ya vijiji mtu akikomaa ajikwamue angalau aweke bati, unaambia huyo hachukui muda atakufa.
3:Kuna vijiji akiwekeza ngozi nyeupe sawa akiwa mbongo mwenzao kutoka sehemu nyingine akatajirika huku wanamuona. Hawachelewi kufitiniwa ili aondoke.
4:Mwalimu/Nesi/polisi ni mtu mkubwa sana kijijini. Ila wivu ukiwazidia wanakijiji kutokana na kuwa kwa malimu wanakunywa chai wao hawanywi, huchelewi kukuta umelala juu ya bati.
5:Kuna vijiji wanaogopa kuendeleza sehemu flani kisa tu inasemekana sehemu hiyo kuna wachawi.
Mara nyingi hii hutokea vijiji ambavyo watu wake hukaa pamoja muda mrefu bila kuchnnyika na makabila Mengine. Matatizo haya huisha pale watu wanachangamana na makabila mengine.
Vijiji ulivyowahi kuishi/kusikia/kupita umewahi kukutana na lipi?