STORY: JINI ZUNAIDAH
MTUNZI: HAFIDHU MWINYIMKUU
CONTACT: 0719013038
WHATSAPP: 0719013038
MAHALI: DARES SALAAM
SEHEMU YA KUMI NA NNE
Tunaanzia pale tulipoishia ambapo MJOMBA SELE na mama HAMISI wakiwa wanazidi kuchanganyikiwa bila kujua wafanye nini ndipo wakashauriana kwenda kumtafuta
MAMA: sijui labda tutamfute lakini tutamtafutia wapi?
MJOMBA SELE: hebu twende tutajua huko huko mbele ya safari.
Huku wakinyanyuka na kutoka nje.
MAMA: eeeh bwana wewe hebu ni subiri nifunge mlango wangu.
MJOMBA SELE: hebu Fanya haraka mwenzio nimechanganyikiwa !
MAMA: sasa we ukic hang any ikiwa na Mimi nisemeje? Punguza jazba tujue tunaanzia wapi!
Baada ya kutoka nyumbani kwa mama HAMISI wakaanza kuzunguka kumtafuta ili wajue ameenda wapi lakini jibu walilokutana nalo halikuwaridhisha kwani walienda mpa ka kwenye vijiwe anavyopendelea kwenda waliambulia patupu.
MAMA: mi naona tukatoe taarifa polisi!
MJOMBA SELE: nini? Huko ndo utaharibu kabisaa we umeona wapi vita ya kuku na nyoka anaamulia binadamu?
MAMA: sasa kumbe tufanye je
MJOMBA SELE: hebu rudi kapumzike kwanza na Mimi niende nyumbani mpaka kesho nipate akili nyengine!
MAMA: simu yake umempigia ?
MJOMBA SELE: hapatikani we nenda mwengine tutaongea kesho!
MAMA: sawa ila lolote likitokea naomba tujulishane.
MJOMBA SELE: hamna shida.
**************************************************
Tunarudi upande ambao yupo ZUNAIDAH na SHABAN waliendelea na safari yao isiyokuwa na muelekeo kwa SHABAN mpaka wakafika kwenye jengo moja zuuuri.
SHABAN hakuamini kufika sehemu kama ile aliona kama anaota machni mwake au yupo usingizini anaota kwani Mara kwa Mara alijaribu kufikicha macho yake na kujifinya kama anaota akurupuke kutokana na maumivu anayoyasikia.
ZUNAIDAH: sheby mpenzi karibu nyumbani kwangu! (Akiachia tabasamu mwanana)
SHABAN: asa...nte...I...la...ha..pa...ni wapi?
ZUNAIDAH:mbona kama hujiamini? Hebu twende ndani ( akimvuta mkono)
Kiukweli Sheby mtoto wa kitaa toka azaliwe hakuwahi kufika sehemu nzuri kama hiyo kwani kwake ilikuwa ngekewa kufika eneo hilo.
ZUNAIDAH: sheby!
SHABAN: naam! (Kwa upole)
ZUNAIDAH: bado unaniogopa mpenzi?
SHABAN: hapana sikuogopi!
ZUNAIDAH: nafurahi kusikia hivyo! Na vipi kuhusu ombi langu la kuwa mume wangu?
SHABAN: ni..ni..nime..Ku..ba..li
ZUNAIDAH: mbona kigugumizi? Jibu kama mwanaume basi! ( akijidekeza)
SHABAN: nimekubali
ZUNAIDAH: woow! Nafurahi kusikia hivyo na nakuhaidi nabadilisha maisha yako, sheby huyo atakuwa tajiri ataishi vizuri na hatofkiria shida zaidi ya kuzunguka na magari majini na kila MTU atakujua wewe nani! Ila tu kwa sharti
SHABAN: sharti lipi hilo?
ZUNAIDAH: sitaki unywe pombe, ufanye uzinifu wala kucheza kamali Upo tayari?
SHABAN: je vipi nikitaka kuoa?
ZUNAIDAH: utanioa Mimi
SHABAN: noo! Inabidi nioe binadamu mwenzangu ili niwe na familia yangu
ZUNAIDAH: kwani Mimi siwezi kukuletea familia?
SHABAN hakujibu kitu alikaa kimya
ZUNAIDAH: sawa najua binadamu mnaroho za tamaa saana siwezi kulikwepa hilo, kuoa utaoa lakini mke ntakuchagulia Mimi
SHABAN: khaaa! Mbona unaninyima Uhuru?
ZUNAIDAH: sikunyimi Uhuru ila nakulinda na najilinda mwenyewe.
SHABAN: kivipi?
ZUNAIDAH: mda ukifika unajua,pia Leo hutorudi nyumbani tutakua pamoja hapa!
SHABAN: hapana mjomba atakuwa na wasiwasi
ZUNAIDAH: nimeshampumbaza usijali! Utarudi kesho
**************************************************
Tukirudi upande wa falme ya KASH KASH ambp tunamuona Mfalme AMOUR akiwa ana jadili na mkewe kuhusiana na binti yao.
Mfalme AMOUR alikuwa analalamika kuhusiana na mkewe kushindwa kucheza na akili za mwanae ZUNAIDAH ambapo mpaka leo hajatoa jibu lolote kuhusiana na kukubali kuolewa na BINAMU yake YUKTY kijana kutoka Falme ya ALBASHR.
Mfalme: mama ZUNAIDAH nimechoka kusubiri nini kinaendelea mpaka sasa?
UMMUKURTHUM: Hebu vuta subra kidogo mumewe wangu
Mfalme AMOUR: hapana siwezi kupoteza muda zaidi nahitaji ZUNAIDAH aolewe na YUKTY!
UMMUKURTHUM: lakini hampendi
Mfalme AMOUR: sitojali anampenda au hampendi lazima aolewe na YUKTY
UMMUKURTHUM: hivi kwa nini unamchagulia mtoto mwanaume wa kumuona? We mbona hujawahi kuchaguliwa? Inamaana hukumbuki ulivyokuwa unanivizia Kyle maktaba unajifanya kuja kusoma vitabu wakati wewe umezoea kushika mapanga?
Mfalme AMOUR: sihitaji kukumbuka ya zamani! Kwanza hayo hayahusiani na sasa!
UMMUKURTHUM: sawa lakini mchumba uliyechaguliwa na wazazi wako ulimuoa?
Hapo Mfalme alishikwa na kigugumizi kisha akajikaza
Mfalme AMOUR: naomba usinikumbushe mambo ya zamani
UMMUKURTHUM: nijibu swali langu
Mfalme AMOUR: naomba tulizungumze baadae!
Alinyanyuka na kuingia ofisini kwake.
UMMUKURTHUM: ntakunyoosha tu ( alijisemea)
**************************************************
Ikiwa ni siku nyengine ambapo kumekucha tunamuona MJOMBA SELE akiwa anajiandaa kutoka kwenda kwenye mizunguko ya kumtafuta sheby Mara ghafla ugeni...
SHABAN: shkamoo mjomba
MJOMBA SELE: khaaaa! Wewe ulikuwa wapi mjomba? (Kwa mshangao)
SHABAN: hamna mjomba nilikuwa kwa kina hamisi nikaona usiku umeingia ndomana nikalala huko huko!
MJOMBA SELE: sheby staki uongo, Jana mama HAMISI nilikuwa nazunguka nae kukutafuta wewe na hukuwepo Kule, naomba nijibu ulikuwa wapi?
SHABAN: mjomba umesahau kama niliondoka na HAMISI? Na akakwambia kuna mtaalamu ananihitaji hivyo niwahi na wewe tukakubaliana utatukuta umesahau?
MJOMBA SELE: sawa na hiyo Pete ya dhahsbu umeitoa wapi?
SHABAN akaanza kuumauma meno... Aaaah mjomba bhana hii nimeokota
MJOMBA SELE: wapi?
SHABAN: njiani! Kwani unadhani nimeiba?
MJOMBA SELE: mmmmh! We mjomba yangu kweli? Hebu nisubiri nakuja sasa hivi usitoke sawa?
SHABAN: mi nipo!
JE NINI KITATOKEA ......UNAFIKIRI MJOMBA ANAENDA WAPI?.....USIKOSE KUFATILIA KISA HIKI CHA KUSISIMUA.......BY MELI YA MGIRIKI....