Story za mkeo/mpenz wa ndoa

Na mjaribu saa ingine kuja na story za kuongeza kipato ili familia imee sio mastori ya harusin na maofisini mwenu tu kila siku bana yaaani uje na say mpango wa biashara na jinsi ya operationalization mimi ntakusikiliza kila siku hata wa manane ila ya Mke; Honey nikwambie kitu..........
Mume; Enheee........
Mke; Jana ofisini ile kikao yooote mpaka jioni ile tukatoka secretary na bosi tumewaacha ofisin ana inasemekana wana uhusiano wa kimapenzi
Mume; Bad Habit.........
Mke; Inauma sanaaa

At Home......
Mke; Mume wangu
Mume; Naam......
Mke; Hivi unajua this weekend ndo ile send-off
Mume;Owk....ntakupeleka then ukiwa tayari ntakufuata mke wangu.....
Mke; Sasa utakuta kwenye send-off watu huwa wanajikandika mipoda kama wachawi yaani mi sipendagi...........
Mume; Ngrrrrrrrrrrrrrrr.........................ngrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr kalala zamaaaaani as mistory yako inaboa saaaaanaaaaaaa na ni non-constructive

Tafakari................chukua hatua

heheheee umenchekesha na scene yako thanx, ila mapenz ni kuheshimiana, kuvumiliana,....etc. Kwani nyie wanaume hamna maongezi ambayo yanaboa? au yanamboa mkeo? mbona huwa anakusikiliza tena akiwa macho kodo bila hata kupiga kope? just emagine unastory yako then wakati unaisimulia mkeo anachat bbm na tabasamu mwisho anaangua kicheko kikubwa wakati story unayopiga wewe ni ya kuhuzunisha utajiskiaje? si kwamba alikuwa hakusikilizi? au utapata picha kwamba unampigia kelele na siajabu ukatumia mabavu yako na kuanza kumpiga biti hebu wnaume lainikeni kidogo hata kwa nusu saa tu loh!!!
kweli aliyesema think like a man act like a lady hakukosea
 
Kwa mfano dada @sakapal, I'm your husband, tuko garini - unanipigia story zako na wadada wenzio wa kazini,umemaliza unaanza kilichojiri harusini kwa fulani, kisha fulani na mumewe then mara dada huyu kaachana na mpenziwe.
Kwa kweli I wont stand hearing you talking all the way!
na ukianza story za kitchen party I will kick you out of the car!

hahahaaaa yaani umenichekesha hadikahasira kameisha coz wakati naandika hii thread nilikuwa na hasira za kutosikilizwa lol thanx,
siko hivo sina story za kuzungumzia nani kafanya nini ni maongezi hata yanayojiri serikalini, vichekesho utadhani yeye hapendi kucheka aah inachosha kwa kweli. Ila kama uko hivyo tit for tat na mimi ukianza tuu stury zako za ligi kick u out of bed looh sijui kitafuata nini hapo....
 
Wanawake wengi nadhani tuna nature ya kuongea...lakini sioni kwa nini mume akasirike kama mazungumzo si mabaya. Mimi mume wangu nikiwa nae nikikaa kimya dakika kumi lazima tugombane...anapenda sana kusikiliza story zangu...mpaka inafika kipindi nachoka.

Kuna siku niliingia kwenye gari na novel nikaanza kusoma..akauliza NK mbona unanichunia leo? Yeye ni mkimya sana na ni patient anapenda sana kusikiliza na wala hakukatishi hata kama unachoongea kitakuwa kina bore. That is why I love him.

Mimi ni opposite nina tabia mbaya ni mwepesi wa kukatisha mtu akiwa anaongea nikiona story haina mpango.

Wakati mwingine ananunua gazeti la mwanahalisi afu ananambia nimsomee wakati anaendelea ku drive. I think I am very lucky.

Ila najua asichopenda ni kuleta stori tukiwa kitandani. Na hilo naepuka. Kitandani ni dirty talks tu basi.

Nadhani tatizo mlilo nalo nyie waume zenu pia ni waongeaji...muongeaji na muongeaji hawawezi kuwa compatible...nani atamsikiliza mwenzie???? Nikikutana na mtu mwenye maneno kama mie uwa nakaaga kimyaaa. Maana inakuwa kama tunashindana vile.
 
Morning every one!! I salute you all, SALUTE!!!

Ni hivi , leo nina swali kwa wanaume hasa waliooa au walio kwenye mahusiano na mwanamke kwa muda mrefu, tafadhali naomba mueleze ukweli ili kunisaida mimi na hata wadada wengine wenye shida kama hii.

Niko na mahabat wangu, tunatabia ya kuondoka wote home kwenda kazini na kurudi pamoja kwa kutumia kabajaji ketu si unajua bongo usafiriwa shida? Na hii imekuwa ikitupa nafasi ya kuongea mambo mengi njiani na tukifika home ni kuangalia watoto kuoga na kulala. Sasa shida iko hivi, mimi napenda sana kuongea na hili analijua utakuta ile nimeingia tu kwenye gari naanza story sometimes za kuchekesha, sometimes za ofisini yaliyojiri ofisini kwetu siku nzima, leo nani kafanyaje, nani kaambiwa nn na bosi, mkutano leo ulikuwaje, na sometime hata siri za ofisi au mikakati ya ofisi yetu namtaarifu nikijua ni maongezi tu looh. Sijui anakuwa anachoka kusikiliza au hapendi tena sauti yangu yaani utakuta unaongea in btw hata hujamaliza anaongeza sauti ya redio like ninyamaze. Unakaa kimya baada ya muda unaanzisha story ingine heee! unashangaa anakuuliza kitu kingine tofauti labda nilikuwa nasimulia kuhusu habari ya watoto utasikia tuu wale mafundi walimaliza jana uliwalipa hela yao yote looh! nachokaje?
Baada ya kuona shida inazidi na sipati nafasi nzuri ya kusikilizwa nikaona bora nikae kimya na tuwe wote mabubu njia nzima toka mjini hadi home yaani napata shida.
SWALI;- Hivi kwa nini wanaume hampendi kusikiliza masimulizi ya wake zenu? hii hata kijana mmoja hapa ofisini nilishamsikia akiongea kwamba kunarafiki yake ameoa mwaka jana ila ukifika muda wa kwenda kwake hatamani coz anawaza jinsi ya kusikiliza story za mke wake za siku nzima na mkewe huyo anataka mumewe amsikilize hadi amalize. To me huyu kijana anaboreka na hizi story na amechoka kuzisikiliza, sasa kwa nini nyie wanaume msiwaambie wazi wake zenu kwamba usipige story zako za kutwa nzima? au mwambie kwa upole tu pls nimechoka leo naomba tuongee asubuhi au hata ukamwambia nasikia kichwa kinauma reserve the rest for tomorrow huyu mwanamke atakuwa in good place ya kukuelewa that u need a space ila isiwe kila siku. A u hata ukamsikiliza tu then akimaliza yule mwanamke anafurah basi na wewe unaendelea na mambo yako. Naomba niwaibie siri nyie wanaume...,
Sikilizeni wake zenu, hii ni kitu ndogo na ya kijinga but ni kubwa na ya muhimu sana hasa kwa wanawake yaani kama mm hapa naugulia coz sisikilizwi story zangu naishia kujikuta naongea mwenyewe na mbaya zaidi kunawakati anakwambia njoo tuongelee kitandani wakati wa kulala akishapata tunda lake ukirudi kuoga unamkuta anakoroma sometimes unamkuta macho but unaanza story ukijastuka mwenzio alishalala saa nyingi, inaudhi kweli muwe mnatuambia kwamba usiongee baby ninausingizi sana.
Mie napenda sana kuimba hata sometimes unaskia kero kumuimbia coz ukiimba anaona kama unampigia kelele yaani wanaume naomba mnisaidie shida ni nini?
Hampendi story? je ni story za kipuuzi? mbona hamsemi? maudhiiiiiiiiii??

Ever remaining,
Sakapal

Sijamaliza kusoma story nzima lakini hapo red pamenichekesha sanam, loh! ........ ila ngoja nimalizie utamu wote plus comments za wadau
 
Wanawake wote wakiwa hivi mfumodume hauishi kamwe.

Mwanamke ni lazima abadilike kumfuata mwanamme, hata kama mwanmme ni an antisocial jerk.

shida moja ni waongo sana na mngekuwa mnaonyesha from day one unamtongoza mschana kwamba wewe ni anti social au kumpeleka shopping mpenz ni shida kwako walaah hakuna mschana ambaye angewakubali ma boys antisocial, we antisocial kwani we jiwe?
tuna refer day one ulichosema but now unajidai huko ivyo hee! nyie mibaba mnamaudhi sana aaaah!
 
first of all don't salute us coz we have no ranks,okay ni kwamba hamchez na alama za nyakati,hujui mume wako amekumbana na mishe gani instead unaanza kuleta story zako za ajabu ooooh sijui yule mama wa keki leo amezidisha unga wa ubuyu kwenye soda ya bosi aliyokunywa leo ilikuwa na kichupa ndani(hueleweki)unategemea kusikilizwa?na mfumo ndo huo mpaka mtakapokuwa smart,na kwa bahati nzuri na kwenye katiba mpya lipo,no chance for non sense stories.

polee coz kwa mfumo huu mnajiharibia CV with time mtaachiwa manyoya shauri yenu msije sema sijawaibia siri ya wadada walioolewa.
sometimes kweli unamuona hubby yuko down na unajaribu kumcherish hasira zimuishe but badala ya kufurahia kuondolewa huzuni anakuambukiza nawe huzuni mbayaaaaa loooh alijisemea mama Rwakatare. Fungukeni muwaambie ukweli wake zenu hamtapata hizi story za kichwa na miguu tutakuwa tunazireserve kwa ajili ya kichen party tuu.
Ila wanawake wanaweka vitu vingi moyoni na kusubiri kuvimwaga kwa wampendaye au waliye karibu naye... hapo chacha msikilizaji kalewa puuh!
 
Sakapal hebu nenda kasome Code of Conduct (Hapa kikazi zaidi) maana imekupita kushoto

Kuhusu hizo story wanaume hawapendi kusikiliza wake zao wala kuongea nao sijui kwanini lakini ukikuta yuko na mpango wa kando anacheka mpaka jino la 32 unaliona........................
 
Mwanamme anayejua maongezi anamjibu vizuri mkewe na kuyaongoza hayo maongezi kuelekea kule anakofikiri kunafaa zaidi.

Sasa wewe unaona mkeo anaendekeza gossip, badala ya kuonyesha hufagilii na kuongea habari hizo hizo kwa kina zaidi, unamuacha mamaa anakuwa kama anafanya jitihada za kuwa social wakati wewe ume mute.

Unakosa mvuto.

Unaweza kupinduliwa kwa kitu kidogo tu, katokea kijana mtanashati hana lolote zaidi ya maongezi mazuri, anakufanya mbaya.

Halafu utalalamika wanawake wa siku hizi wasaliti.

Kumbe usaliti umeanza mwenyewe kwa emotional neglect iliyo borderline torture.

Mara nyingine mtu anaweza kuanza kuongelea weather sio kwa maana ya kwamba anataka kuongelea weather, anataka ku crack the ice tu kwa nyepesi nyepesi, sasa kama mwanamme kichwa you take that and run, you build up the convo.

Sasa wewe mtu kaanza na weather tu unasema huyu naye kashaanza story zake za ajabu ajabu.

Utaonyesha humpendi, anakuboa. Mtu kama unampenda kweli hata akikoroma utaona kama muziki.

Na akileta story nyepesi nyepesi unazipeleka kunako, si kumchunia.

yaani umenifurahishaaa! pata na like ya maneno hapa *100

yaani huo ndo uchawi utakaomlogea mkeo hatabanduka home akikusubiri uje umsikilize, coz sometime anataka akudekee tu na kitu cha kijinga utaskia hebu sogea huko lol unaborekajeeee!!

wanaume wote wangefanya kama ulivoeleza hapo juu mngefurahi na wake zenu for good am telling u, am a woman and i know it yaani akikuona tu tabasamu kubwaaa na .......
 
it is boring for sure!najaribu kuwaza masaa matatu mko kwenye foleni na unaongea tuuuu... mpaka mfike home?mpaka mwaka uishe anatesekaje?bila shaka asubuhi pia mnatumia masaa mawili kwenda job pia unaongea japo hujatuambia unaongea kitu gani maana mtakuwa mmetoka kuamka!!!nashauri uwe unapanda daladala au mnunue gari lingine!!ingekuwa dk 15 tu mmefika home/kazini wala asingekuwa hivyo
 
talking is everything in a relationship, hapo ndio pa kumjua na kumsoma vema mwenzi wako!!! ila tu tujue kupeta chuya na mchele! tupembue pia mawe na mchele! iwe 50/50! sio we unaongeaaaaaaa kama radio, na mwenzio awe na chance pia! lolest!
 
Kwanza pole sana my dear sakapal but i salute u again in the name of..

Kwanza na mimi niseme kwamba inaweza kuwa fault ya either mwanamke au mwanaume katika kutojua stori gani mwenzake anapenda au havutiwi nazo. Ni kweli kuna vitu havilazimishiki kwa mwingine..kwa mfano binafsi sipendi gossip..yaan flani kafanya hiki ama kama kafanya kile (the shigongo style)..Ina maana kama mkewangu analeta stori za namna hii lazima nitamtune off..Lakini pia kuna wakati ambao mnahitaji kurelax hamuwezi kila wakati kuongelea mambo ya maendeleo tu mnaweza pia kuongelea social life..As a man lazima umsome mkeo na unaweza kudirect stori ili na wewe upate cha kuchangia. Sishauri tabia ya kukaa kimya all the way!!!

thanx my dear SnowBall yaani story ndani ya ndoa zinachangamsha na kuboresha mapenz, ila mi bado ninaombi kwa wanaume pls mkiona mnaboreka waambieni wake zenu kuliko kumuacha na sononeko sio vizuri hivyooo..
 
Mmmmh, kukosea tena???

Hivi maongezi nayo yana manual??

Kazi sana dunia ya sasa

Tv na redio zimefanya familia zimekuwa na ufa.

sakapal tafuta hiki kitabu usome

nilikikuta sehemu nikakinunua tu nisome, nilichoka. yaani ni kama walikuwa wananizungumzia mimi. Nikawapa wadada 3, wakisome, yaani kila mdada aliona kama anazungumziwa yeye. huwa tuna makosa mengi sana tunayafanya tunapokuwa tunaongea na wenzetu, lakini hatujui kama tunakosea. sometimes timing mbaya (yupo busy na gazeti au TV wewe ndo unaanzisha stori), hatupo direct (tunazunguka zunguka tuuu, halafu tunategemea wataelewa)... na mengine mengi tu
 
Lakini tena tatizo hapa naliona kwa wadada, si wote "BAADHI"

Anaingia kwenye mahusiano mapya kwa kupretend sana
Ana act like a lady, kuongea point tu
Wakati kabisa anajijua point ni za kukopa
muda mwingi yuko "off brain"
Sasa muda wa kupretend ukiisha yule mtu anaboreka
Labda alichokipenda kwake ni ule u -'On Brain"

Hakuna kitu kizuri kwa kuwa mwenyewe from day one
mtu anajua kabisa kapenda cherehani ya maneno

Kongosho nimekugongea LIKE, ni muhimu mtu ukajua unatumbukia kwenye shimo la kina gani ili ushauriane vizuri na miguu!!!
 
Trust me, sikukurupuka kwenye kuoa mke na sijaweza kumuheshimu na kumtunza kiasi cha kuja kupinduliwa kirahisi kama unavyodhani.
Na wala mke wangu hayuko hivyo

hongera dah utakuwa unaenjoy...
 
Mmmmh, kukosea tena???

Hivi maongezi nayo yana manual??

Kazi sana dunia ya sasa

Tv na redio zimefanya familia zimekuwa na ufa.
siyo dunia ya sasa.................. hata zamani baba alikuwa akirudi nyumbani anakaribishwa, anasalimiwa, anaulizwa kama ataoga kwanza au kula kwanza, maongezi yanakuja baadae. siyo kama ulikuwa unamngojea vile, akitokea tu unaanza na stori zako, bandika bandua..............
 
Sikuongelei wewe, naongelea a scenario.

Hii case iliyoletwa hapa ni emotional neglect.

Huyu mama anaweza kuwekwa katika majaribu kirahisi sana kama akitokea mtu mwingine akaonyesha kumjali na kumsikiliza.

Tusiwaweke wenzetu katika majaribu kirahisi hivi. Inafaa kusomana tangu mwanzo kabisa na kama mtu hamko compatible, hampotezeani muda kabisa.

yaani wewe u have win ur wife kama umeoa am telling u, hutaboreka u have known the secret of woman nahisi hupati hata shida ya kumuuliza umefika... wakati wa majamboz maana wengine wanauliza utafikiri hawajui kama uko happy au bado uko njiani lol. Wanaume wengine huko use this way of Kiranga hutaboreka na mkeo. Ushauri wa buree tu. Thanx much kiranga
 
But then she will drive you nuts with her stories! Kwa kweli kuvumilia mtu akiongea story ambazo huzipendi kila siku ili kuogopa 'emotional neglect' ni utumwa.
Hapa labda tukubaliane aambiwe kama hana story za msingi anyamaze period!

jamani basi jaribu kulainisha maneno like tumia lugha tamutamu kumnyamazisha. Au its better umwambie hivi,'' mke wangu hizo story za A-J mimi zinanibore napenda sana kuongea na wewe but naloose temper ya kukusikiliza zikijirudiarudia, tuongelee vitu vingine'' na hapo waweza suggest topic nakwambia mwanamke anafuata mkondo wa mwanaume kama maji atakuelewa na hutasikia tena makelele looh
 
hahahaaaa yaani umenichekesha hadikahasira kameisha coz wakati naandika hii thread nilikuwa na hasira za kutosikilizwa lol thanx,
siko hivo sina story za kuzungumzia nani kafanya nini ni maongezi hata yanayojiri serikalini, vichekesho utadhani yeye hapendi kucheka aah inachosha kwa kweli. Ila kama uko hivyo tit for tat na mimi ukianza tuu stury zako za ligi kick u out of bed looh sijui kitafuata nini hapo....

Vigezo vya kukick 'ana viishie kwenye gari au jikoni, huko kitandani mbali sana visifike.
 
Nimejifunza mengi baada ya kupitia uzi huu; Asante mleta mada. Sina uzoefu sana ktk hili coz mimi ni mvivu wa kusikiliza lkn pia si muongeaji saaana!

Nahisi, mko katika stage ya kuanza kuchokana at least mwenzio. Jaribu kupeana space, ikiwezekana kutoshare usafiri mnapoenda kazini; ili atleast mkumbukane walau kidogo. Usibadilike, alikupendea jinsi ulivyo na ndio maana ukistopisha story ananuna; ila punguza muda wa kuwa pamoja ili usijiboe na kumboa mwenzio!

Cha mwisho, ulivyouliza humu; muulize the same question mumeo lkn make sure anapata picha ambayo sisi tumeipata in a constructing way.

All the best!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom