Story: Kwanini Upo Single?!

Story: Kwanini Upo Single?!

Me nilifikia wakati nataka kuowaa mara nikagundua mwenzangu analiwa na wengine....
 


C. MATESO YA WANAUME YAWMENIFANYA NIWE SINGO


Mimi nipo singo kwa kupenda


Kanisani sijataka kurudi tena kwa Walokole nasali Lutheran kwa Dini ya wazazi wangu

Huenda wokovu umewasaidia wengi ila sio mimi kwakweli

Nampenda Mungu sana na nasali sana, namtumikia Mungu kwenye huduma ya Mwalimu Mwakasege, hio inatosha kwa sasa

Wanaume kwa sasa hapana ngoja Kwanzaa nipone kidonda



TUONANE J3 TAR 21 MAY 2018 SAA 1 USIKU YA TZ


Honey Money Penny salute!

Hata hivyo sababu za Teresia kupigwa na Mkurya ima kupigwa na Mmasai ama kuambulia 1nightStand hazipo wazi. Ni dharau kwa vile Teresia anacho kipato chake ama ni nini?

Nasubiri ushauri nasaha atakaopewa, labda nitajua chanzo cha mateso ya mwili aliyopitia Bi Teresa
 
B. WACHUNGAJI WAMENIFUKUZIA WANAUME WOTE NILIOWAPELEKA KWAO, NDIO MAANA NIPO SINGO!

Tukaja tena siku nyingine kwa ajili ya darasa letu la wadada single, sikuile tuliacha patamu baada ya kuona kuwa KOKU anachangua chagua midushe ya akina kaka zetu

kweli niajabu, huyu Koku huyu haangalii tabia ya mwanaume haangalii kabila, haangalii dini, haangalii utaifa yeye ni kanyaga twende tu, na anakanyanga kweli kweli maana kuna maneno aliyaongea pale mpaka nikarudi nyumbani kichwa kinauma

hili darasa nimelipenda sana, watu wapo open, wanajiachia hawana aibu wala nini alafu limechangamka mpaka sisi tulio wapole tunachangamka tena

sikuile tulimaliza vizuri, tukapigwa na picha na selfie kibao, tukatamani jumamosi ifike haraka lakini kama unavyojua hamna jumamosi bila kuikanyaga j3 mpaka ijumaa

sikuhio kila mtu alitaka kuongea wa kwanza ajielezee kwanini yupo Singo, Koku katufungulia mlango wa nguvu, basi Mwana saikolojia kufika tu kila mtu anataka kuongea, darasa letu lina makelele sio kitoto, akawa anashindwa amchague nani, mimi hapo nipo kimyaaaaa

Mwana saikolojia: akaamua basi mimi naomba tuongee tu leo mimi nitawajibu mwishoni maswali yenu, kwa sasa naomba nimchague bibi hapa ambae ni mimi niongee maana nimekaa kimya sana, akaomba aanze na mimi na anajua nikiongea nitachangamka maana mimi ni mpole sana,

nikakubali kuongea nikaanza kwa kujitambulisha

Mimi: Kwa jina naitwa Mwelu, ni mwenyeji wa Singida, nina miaka 33, nimeajiriwa kwenye kampuni ya ... Meneja Masoko

Mwana Saikolojia: oh! jamani kazi nzuri hio na kampuni nzuri sana, hongera sana

Mwelu: asante
Mwana Saikolojia: enhe! endelea mami,
Mwelu: Nimefanya kazi kwa miaka 5 sasa, ila sielewi kwanini nipo singo mpaka sasa najua huu sio mpango wa Mungu mimi kukaa peke yangu, alisema atanitafutia wa kufanana nae lakini mpaka sasa sijamuona na umri unaenda, mbaya zaidi kinachonichanganya naumwa sana Fibroid!

Wote: oh! jamani pole sana mami, pole rafiki utapona, pole pole,

Mwana Saikolojia: kwahiyo wewe ni mlokole umeokoka?

Mwelu: ndio, nimeokoka nampenda Yesu sana sana

Mwana Saikolojia: Hospital umeenda wakakwambiaje kuhusu ugonjwa wako? wanakufanyia opereshen au? lini?

Mwelu: nimeenda, wakasema nikitoa Fibroid lazima nizae, nazaaje sasa wakati sina mchumba wala mume wa kuzaa nae?
Nikaenda kwenye maombi nikaombewa lakini wapii! bado zinakuaaaa, nikafunga mwenyewe namwomba Mungu aziondoe lakini wapi hazitoki, nimeshaenda kwa Manabii lakini wapiii bado zimekomaa nimefika sehemu nakaaga kama bumbu wazi, sijui shida iko wapi? sidhani kama nimelogwa asee!
Huu ni mwaka wa 7 sasa nimeishi nazo hizi Fibroid lakini hazitokii! doh nachanganyikiwa sana, nimekuwa singo kwa miaka 33!

Wote: uuuuwi ina maana wewe bikra? hujawahi kuwa na boyfriend?

Mwelu: Boyfrienda Kanisani wanakataza

Wote: Yesu JE? Anakataza pia au?

Mwelu: well, labda, ndio, sina uhakika!

Wote: haujawahi kumwuliza Yesu kuhusu kukupa hata Bwana wa kukufurahisha au akuzalishe kama ameshindwa kuleta Mume akuwowe uzae ndani ya ndoa kama anavyotaka?

Mwelu: kwakweli Yesu hashindwagi

Wote: Mbona Fibroid hajaziondoa miaka 7 sasa, Yesu gani huyo unamwomba usiku na mchana hakujibu? Yesu hana roho mbaya kama wachungaji wako hao, hawakuombei mpaka upeleke sadaka ndio anakuombea vizuri
na umebinuka na hizo Fibroid kwenye maombi miaka 7 lakini bado unazo?

Mwelu: hata sijui huenda ni jaribu langu

Wote: wanacheka kwanguvu sana, wengine walicheka mpaka wakatambaa chini

Mwana Saikolojia: Jamani naomba utulivu tafadhali, naomba aongee muhusika sisi tuwe wasikilizaji maswali nitauliza mimi!

Wote: pole sana mpendwa, hahahahaha, pole! pole! pole!

Koku: samahani Mwelu, unauhakika umeokoka sawa sawa? like asilimia 100? au unachakachua?

Mwelu: sijawahi kuchakachua hata siku 1

Koku: mimi nilivyokuwaga sina bwana kabla sijanunua doli la kiume, nilikuwa najisaga vibaya mno, unauhakika wewe haujichui kweli hata kwa kidole!

Mwelu: hata sijui hayo mambo, sijawahi kufanya hayo, maana Mungu hapendi! na mimi sipendi kumchukiza Mungu
Mwana Saikolojia: Mwelu my dia, sisi tunakupenda mno lakini hatuwezi kumfikia Yesu na Mungu kwa jinsi wanavyokupenda, lakini Mwelu, hii elimu ulio nayo ni degree au masters au diploma au certificate ya Masoko?

Mwelu: nina Masters!

Wote: ahahahahha wanacheka kweli kweli, wengine wakauliza hiyo Master uliipata kwa nguvu ya Chupi au Yesu?

Mwelu: Mungu alinisaidia akanipatia

Wote: wakacheka sana sana sana, doh walokole ni mwisho wa Matatizo! ahahahaha wengine wakasema Yesu akyanani ana kazi kweli kweli

Mwana Saikolojia: jamani naomba utulivu muda unaenda na Mwelu hajamaliza kuongea

Wote: leo tunamwachia uwanja Koku mwalimu acha amalize masaa 3 maana anashida kuliko sisi

Mwana Saikolojia: Mwelu mama achana na hawa bwana vichaa we endelea mimi nakusikiliza

Koku: lakini mwalimu huyu alisema alipata wanaume au hajasema embu atuambie walikuwa wanamtongozaje anawakubalije huenda kuna mbinu mpya ya kutongoza kwa Yesu tuijue na sisi tukikutana nayo tuishinde!

Mwelu: mimi nimewaambiwa kuwa sijawahi kuwa na mume, sijaolewa, sijawahi kuwa na bwana

Koku: kwahiyo wewe hautongozwi au? hata wa kukuchumbia hayupo?

Mwelu: wapo niliwapata

Koku: uliwapataje ndio tunataka kujua na walienda wapi mpaka sasa unabeba ma fibroid si ungewakubalia?

Mwelu: kwakweli, niseme ukweli kama Koku alivyosema ukweli, Koku mimi nakupenda hata kama una maswali kama Polisi,

Wanaume nawapata ofisini kwangu, nikienda kutafuta wateja, nikisafiri kikazi, kanisani pia nawapata, tukienda kwenye makanisa mengine kufanya huduma nawapata!

Koku: wanakutongozaje ndio tunataka kujua mama!

Mwelu: wananiambia tu

Wale wa Kanisani: Bwana Asifiwe, naomba kuongea na wewe, nikiwasikiliza wengine wananiambia Mungu amesema na mimi wewe ni mke wangu, wengine wanasema nimekupenda nataka kukuwowa, wengine wanaogopa kusema wanaenda kumwambia Mchungaji, alafu Mchungaji anakuja kuniambia ofisini kuwa kijana amekuja kunichumbia anataka kunioa

Wote Pamoja na Mwana saikolojia: ahahahahahahha, uuuuwi Yeeesu leo ni siku ya kucheka na kuongeza Maisha! walicheka sana wote

Koku: alafu unamjibuje mzee baba mchungaji?

Mwelu: nakubaliana kuonana na huyo kijana niongee nae nakuta sijampenda

Koku: enheee1 hapo hapo ndio nimekupata! hujampenda! kumbe kutompenda mtu sio dhambi ee?

Mwelu: sijakwambia uchukie watu sasa Koku

Koku: aaah! si umesema hujampenda kwanini usimkubalie sasa si mlokole mwenzio bwana!

Mwelu: hapana sijampenda

Koku: au hana gari na maisha ya kukupa unaogopa kutembea kwa miguu?!

Mwelu: mimi gari ninalo tutaendesha langu

Wote: ahahahahahah ya leo kali, uuuwi ahahahahahha

Mwana Saikolojia: sasa kwanini upo singo Mwelu jamani kumbe vijana unawapata

Mwelu: hao ni wa Kanisani

Kuna wa Ofisini: hao wanakutongoza leo, wanakutoa out kesho, kesho hio hio wanataka kulala na wewe, na ukiwaambia umeokoka hauzini wanaondoka hawarudi wanaenda kukutangaza kwa watu yule mlokole msiende pale hafungui miguu

Kuna wale nawapata nikisafiri Kikazi: ndio hao hao wanafosi walale na mimi kabla ya ndoa!

Kuna wale nawapata nikienda kwenye Kwaya: wanakubali tunaoana lakini mwisho wa zote wanakuwa wahuni tu wanataka kile kile walichokuwa wanataka wa ofisini

Wote: wakacheka sana! doh leo Mwelu umeliamsha dude! ahahahahaha... Mwelu tunaomba uolewe na Yesu yaishe ahahahaha!
hawa raia wa Kazini hawatakuelewa mpaka unakufa!



Mwana Saikolojia: Sasa Mwelu hamna uliofanikiwa kuwapenda mkakubaliana kwenda kwa Kanisa ukamtambulisha?

Mwelu: kusema kweli napataga wachumba

Koku: sio wachumba bwana Boyfriend kwani wamekuvisha pete we nawe!

Mwelu: haya napataga wakaka tunapendana, wa nje ya Kanisa, wanakubali kabisa, wanakubaliana na Imani yangu wanakuwa wamenipenda kabisa

Koku: umewapata wangapi?

Mwelu: nilishawapata kama 5 hivi, nikawapeleka Kanisani, nikamwambia Mchungaji kuwa nimepata mwenzangu wa kuanza nae maisha, na wale wanaume wanakubali kweli kwenda kanisani kuonana na mchungaji na kuongea nae, lakini wakishatoka pale kwa mchungaji hawarudi kwangu tena

nilishawauliza wa 3 wakakata mawasiliano na mimi, nikamwuliza na kwingine wa 4 akaniambia ameshindwa masharti ya hapo kanisani kwako, na hawezi kupangiwa ndoa na kuishi na mimi kwa Masharti ya Mchungaji ambae hamjui

Nikamwuliza na mwingine wa 5 aliniamulia kwa hasira maana nilikaa nae kwenye mahusiano miezi 6 na hakuwahi kunigusa; akaniambia Mama bora tu huyo mchungaji akuoe mke wa Pili tu maana sio kwa vigezo alivyoweka kukuoa wewe! kama unataka kuendelea na mimi ambae sijaokoka twende ila kama unawasikiliza hao maboya we endelea nao wakutafutie mume au wakuoe wewe

wote: ahahahahaha! Mwelu weee utakufa na Bikra zako kama kweli unazo shenzi kabisa

Mwana Saikolojia: kwahiyo hao wanaume ukawaacha waende:

Mwelu: ndio

Mwana Saikolojia: kwahiyo walivyoondoka, ushawahi kuwasiliana nao tena au kujua labda walishaoa au?

Mwelu: ndio wote walishaoa wana maisha mazuri sana, sana sana na wana watoto

Mwana Saikolojia: na wewe unajiskiaje kuona wao wana maisha mazuri na watoto?

Mwelu: sawa tu! huenda hawakuwa wa kwangu, wangekuwa wangu wangeshanioa wakakubali masharti ya mchungaji

Koku: ivi hawa wanaume wanaoa wachungaji wanamuoa Mwelu? ushawapeleka hata nyumbani?

Mwelu: hapana bado, naanza kwanza kanisani ndio kwa wazazi

Koku: kwa mfano kanisani wakamkubali alafu wazazi wakakataa utaolewa?

Mwelu: ndio

Wote: ahahahahah kweli Yesu aje achukue vilaza wake sio kwa upuuzi huu ahahahaha

Mwana Saikolojia: kwahiyo Mwelu wewe Baraka za wazazi hauzitilii maanani kama baraka za Wachungaji wako sio?

Mwelu: Mchungaji ndio anatoa baraka za kwanza alafu wazazi baadae

Wote na Mwana Saikolojia: tobaaaa, ahahahahahah uuuuwi

Koku: unasali Kanisa gani hilo mama?

Mwelu: akalitaja

Wote: wakacheka sana doh akyanani Yesu ana kazi sio kitoto!

Koku: my dia Mwelu, naomba uniskilize kabla boss wetu mwana saikolojia hajakushauri,
Kwanza hilo Kanisa mpo wasomi wangapi wanaoendesha magari wenye Degree na Masters?

Mwelu: tupo 5

Wote: uuuwi hamaaaaa hamaaa!
Koku: mami sikufundishi ukazini au umtende Mungu wako dhambi, hapana ila kaa ujue kuwa
1. Mungu amekupa akili mamitooo, embu zitumie zile akili ulizopewa na Mungu za kuzaliwa

2. hivi hapo Kanisani kwanini usihame lakini? au wamekuloga maana Biblia ilishasema kuwa siku za mwisho watakuwa manabii wa uongo wengi tu sasa ona Mungu amekuletea wanaume weeengi na akakuongezea 5 umewafukuza mwenyewe kwa jinga wako wa kuwasikiliza wachungaji, embu hama nenda hata Lutheran au Katholic rudi kwenye dini ya wazazi wako si ushapata neno la kutosha kwa hilo Kanisa embu rudi kwa Kanisa ulilozaliwa unapoteza Muda my dia

3. Miaka 7 umekaa na Fibroid wakati Mungu ameweka hospitali kwa ajili ya matibabu? unataka kufa au hautaki watoto?
unajua Fibroid ukikaa nazo sana unatolewa kizazi mami? maana zinakula kizazi hatari mpendwa wangu

Mwelu: kweli ee jamaan sikujua

Koku: hukujua au haukutaka kusikiliza madokta ukaweka imani mbele ukaona Madaktari ni mashetani wa kuzimu? unafanya vibaya unaleta ujinga kwenye jamii asee wewe, kumbe ungeshaolewaga muda sasa hivi una familia yako kiroho safi, ona hao majingas wako wachungaji wanakuharibia maisha!

4. Wazazi Mwelu ndio Mungu wetu hapa Duniani Mungu amewaweka Mwelu, ina maana kwa maelezo yako wewe Mwelu unawatumikia sana wachungaji hata wazazi wako huwaangalii uongo?

Mwana Saikolojia: kwani Mwelu kwenu umezaliwa wa ngapi?

Mwelu: mimi wa mwisho

Mwana Saikolojia: Mwelu unawaangaliaga wazazi kweli?
Mwelu: sijaenda kwetu nina miaka 3, wazazi wapo Singida kijijini
Wote: tobaaa, laaana hio Mwelu una shida wewe una laana!
Mwana Saikolojia: pesa za matumizi unawapelekeaga? kuwa mkweli utueleze sisi ni zaidi ya marafiki tumeshakuwa ndugu sasa

Mwelu: sijapeleka nina miaka 3, dadangu yupo na kakaz wanawaangalia inatosha

Mwana Saikolojia: hao ndugu zako wanaishi kijijini au?

Mwelu: wapo hapa mjini

Wote: Mweeeeeluuu! we mbona una roho mbaya hivyo? miaka 3 wazazi hawajala hela yako, hawajaona sura yako?

Koku: unawasiliana nao hao wazazi wako au?

Mwelu: sijawasiliana nao nina miezi 6 sasa, wanaendelea vizuri bwana

Mwana Saikolojia: Kanisani hamfundishwi kuangalia wazazi? maana Biblia ukisoma au zile amri 10 za Mungu, kwenye amri ya 4 inasema waheshimu Baba na Mama yako upate heri na miaka migi hapa Duniani, wewe Heri unaitoa wapi?
Hivi inakuwaje una ajira nzuri wakati wazazi wanateseka kijijini?

Mwelu: Kimya!

Koku: ina maana tatizo lingine lipo kwa Mwelu, tusiwalaumu wachungaji wake huenda wanamfundisha lakini hasikii, huyu Mwelu ana roho mbaya jamani miaka 3 hujaona sura ya wazazi wako? we kweli Mafia, bora Fibroid zikuue tu

Mwelu: weee ushindwe kwa jina la Yesu

Koku: sishindwi, ushindwe mwenyewe paka weeee washakufanya msukule hapo kanisani utaisoma namba, lazima utakufa tu wewe mjaa laana mshenzi mkubwa

Mwelu akaanza kugombana na Koku hapo wee Koku akaonekana amejaa hasira sana sana, akamtukana sana Mwelu, we mlokole Fala kabisa huna hata aibu! mshenzi mkubwa wewe nenda Baharini wakakuogeshe, yani inakuwaje una Masters lakini kujumlisha moja na moja upate 2 unashindwa?

wewe Mwelu shida sio hao wachungaji au huenda wana shida, ila wewe una roho mbayaaaaa, na Mungu hasikii maombi ya mwenye dhambi, yani wewe hauna tofauti na mimi nyau wewe kenge mkubwa!
Yani mimi navyochagua madudu ya kiume na wewe mfunga miguu hatuna tofauti ni bora ungekuwa unapigwa na hao wanaume upate mimba kluliko kujidai unafunga miguu sijui bikra mshenzi mkubwa hao wachungaji wako wanakukula tu wewe boyaaaa usitufanye sisi matahira

Koku akaanza kulia, ningekuwa na wazazi mimi wangeishi kama Mbinguni, Mwelu una wazazi unashindwa kuwaangalia eti dada yupo ulikuja na Dada Duniani?

Ikabidi kila mtu sasa ambembeleze Koku, Koku maskini amewakumbuka wazazi wake analia sana kwa uchungu mpaka makamasi huku anamtukana Mwelu mshenzi kabisa wewe toka huko usituletee magundu humu ndani sisi tunaupendo we pekeyako shetani akamfukuza kwa kumpiga magumu ya mgongo toka bwana hata kama kipindi sio changu toka roho mbaya wewe kafie mbele na ma fibroid yako very stupid na masters yako ya chupi! huna maana

Ikabidi Mwana Saikolojia ahairishe kipindi, Darasa limeingia mafuriko, Mwelu akainuka huyoo akaondoka na mkoba wake, wakabakia waliobaki wanamtuliza Koku alieonekana mwenye jazba kubwa kuhusu Matendo ya Mwelu!



TUONANE TAR 19 MAY 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA


Baadhi ya binadamu wa hovyo sana, wanaenda kanisani kujifunza kumtukuza shetani ama ni nini?

Imeandikwa: Mimi ndimi bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine. Halafu MTU anajitangaza mlokole kisha anamwabudu Mchungaji. Kwamba alisemalo mchungaji ndilo asemalo Mungu. Amkeni nyie, nani aliyewaroga!? Acheni kutafuta wachungaji, mtafuteni Mungu. Njia ya kweli na uzima inajulikana (Yohana 14:6).

Wachungaji watawachunga tu, hamtopata heri za Mungu.
 
Kukataa wanaume bila sababu za msingi...

Kusikiliza sana wachungaji, mwisho wa siku wanakuja kulala nao hao hao...

Kujiona wao ndiyo kila kitu juu ya uso wa dunia, wengine wote ni watenda dhambi...

Cc: mahondaw
Hii ni shida na hivi karibuni itakuwa ni janga la taifa
 
mimi tangu nione picha ya wale jogoo awili aliyeoa na aliye single mhh,sitokaa nioe maishani
Woi kwanini jamaa
Basi muoe Koku au Mwelu
Umewasoma lkn page ya 6 ya 9 na 11
 
Honey Money Penny salute!

Hata hivyo sababu za Teresia kupigwa na Mkurya ima kupigwa na Mmasai ama kuambulia 1nightStand hazipo wazi. Ni dharau kwa vile Teresia anacho kipato chake ama ni nini?

Nasubiri ushauri nasaha atakaopewa, labda nitajua chanzo cha mateso ya mwili aliyopitia Bi Teresa
Jamaaani Tereza mpole hana kiburi
Au unawajua nduguzako wagita ni viburi?!
 
Baadhi ya binadamu wa hovyo sana, wanaenda kanisani kujifunza kumtukuza shetani ama ni nini?

Imeandikwa: Mimi ndimi bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine. Halafu MTU anajitangaza mlokole kisha anamwabudu Mchungaji. Kwamba alisemalo mchungaji ndilo asemalo Mungu. Amkeni nyie, nani aliyewaroga!? Acheni kutafuta wachungaji, mtafuteni Mungu. Njia ya kweli na uzima inajulikana (Yohana 14:6).

Wachungaji watawachunga tu, hamtopata heri za Mungu.
Amen brother asante sana kwa neno
 
mimi tangu nione picha ya wale jogoo awili aliyeoa na aliye single mhh,sitokaa nioe maishani


Inshallah,Kuna Mtasha si Unajua Mji wa Kitalii ARUSHA alinipatia Wireless Router aliweka Bundle ya Mwaka Mzima kama zawadi so huwa nateleza nayo tu.


Nipo single kwa sababu nimeamua kuwa single

Nothing more


Me nilifikia wakati nataka kuowaa mara nikagundua mwenzangu analiwa na wengine....

Honey Money Penny salute!

Hata hivyo sababu za Teresia kupigwa na Mkurya ima kupigwa na Mmasai ama kuambulia 1nightStand hazipo wazi. Ni dharau kwa vile Teresia anacho kipato chake ama ni nini?

Nasubiri ushauri nasaha atakaopewa, labda nitajua chanzo cha mateso ya mwili aliyopitia Bi Teresa


niko single kwasababu ya mazingira tu koz ni mtu wa kuka peke yangu sana


Mje na huku Ushauri: mtu anaetaka kufanikiwa aachane na "Mapenzi" ajali maisha yake!
 
Back
Top Bottom