Money Penny
JF-Expert Member
- Jun 20, 2016
- 18,204
- 17,560
- Thread starter
- #201
Polewa kumuoa sijapata
Soma page 6 ukimaliza nenda page ya 9 ukimaliza uje page ya 11 utampata tu wa kumuwowa
Polewa kumuoa sijapata
Uje na huku uone wenzio wanapataje wanawakewa kumuoa sijapata
Page??? CjaelewaPole
Soma page 6 ukimaliza nenda page ya 9 ukimaliza uje page ya 11 utampata tu wa kumuwowa
Hahahahaha naaminia sana Smart911Leo hamjaja huku kabisa
Au mnapanga royal wedding yenu na nyie
Hakikisha Smart911 anakupaka makeup asikuletee usanii
Mje huku News Alert: - ROYAL WEDDING ~ HARUSI YA KIFALME..
Amen Broni hvi kwa mwanamke kuwa single mara nyingi haamui yeye wengi hawapendi kuwa single, ila kwa wanaume mfano mimi niko single kwa 7bu umri wangu wa kuoa bdo nikiwa na mwanamke kwa sabubu najua hatanivumilia mpaka nitakapo muoa , atanicheat tu pia ntapoteza ela zangu mana najua as a men kumuhudumia ni lazma,
Page??? Cjaelewa
C. MATESO YA WANAUME YAWMENIFANYA NIWE SINGO
Baada ya darasa la mwisho kuingia maji, wiki iliofuata tukaonana tena kwa ajili ya darasa lingine
Kwa mshangao nikaona Mwelu amekuja sikutegemea nilijua ataacha kweli Mwelu Mafia
Wanafunzi wote walikuwepo na siku ya leo hakuna aliekuwa tayar kuanza kwasababu ya fujo za sikuile
Koku bila kukosa alikuwepo ila alikaa nyuma na Mwelu mbele
Mwana saikolojia akaamua kuukata mzizi wa fitina akamchagua Theresia
Theresia kwa kifupi Tereza, Mwenyeji wa Musoma, Mgita, miaka 34, Mhasibu Mwenyeji Post Graduate, anafanya kazi kwenye kampuni ya simu
Dada mzuriiii, ana mguu kama wa tembo honge la guu, mweupe maji ya kunde, mfupi, ana kishepu chake kizuri zuri kidogodogo
Mwana Saikolojia: Tereza, Leo naomba uongee wewe Leo maana kwa maisha ulionieleza nadhani utaweka heshima leo
Tereza akasalimia pale na nini, akaanza kudondoka
Tereza: mimi sipo mbali na aliyoelezea Mwelu wiki iliopita, Mwelu ndugu yangu mimi nakuelewa sana maana nimepitia huko huko lkn nikaamuaga kukaa pembeni
Kama nilivyowaambia nimesoma chuo hapa mjini Dar es Salaam, nimezaliwa Dar nimekulia Dar, michezo yote ya Dar naijua kifupi mimi ni mtoto wa mjini kwa sasa tunajulikana kama wadada wa mjini ila mimi sio Dada wa mjini zoba
Kwetu nimezaliwa mwanamke pekeyangu na kaka zangu 3 wamenitangulia jumla wa 4 kwahiyo unaweza elewa nimekuwa spoiled kwa namna gani kama mtoto wa mwisho
Nilipomaliza degree ya Kwanzaa, nilitoka chuo na Bikra yangu, mimi sikuwa mtoto wa gate kali ila sikupenda kujichanganya kwenye Makundi sikupenda na darasani nilipataga 1st class chuoni, div 1 form 4 na form 6, form 1 mpaka 4 nilisoma St.Francis kifupi Kwetu tuna akili sana lkn sijui ngoja niongee Mwana saikolojia utanisaidia
Kufaulu kwangu sana kwenye masomo kuliniwekea umaarufu mkubwa sana mpaka wanaume wakawa wananiogopa
Nilipokuwa chuo nikaokokaga kwahiyo yale maisha ya ujana kwenda club nikawa sina
Kiukweli sikuwahi kuwa na boyfriend maisha yangu yalikuwa kama Mwelu
Nilipokuja kukumbuka shuka kumekucha ni pale nilipopata Post Graduate na kuona kila niliesoma nae ameolewa anawatoto, woooo hapo ndio mashetani yalinipanda
Watu wooote niliosomaga nao wana maisha, familia, watoto nikiangalia mimi sikuelewa kwanini sipati mume wa kunioa
Kaka zangu walikuwa na marafiki waliokuwa wananipendaga nikawa nawakataa kwasababu ya wokovu
Tatizo jamani sio Wokovu wala Yesu, Tatizo sijui kwa kweli ngoja niongee labda mtanielewa
Kanisani ni kweli haturuhusiwi kuolewa na wanaume ambao hawajaokoka
Koku: amen sister, mtasanda Duniani mpaka mkome
Tereza: kwahiyo sio kwamba ofisini nilikuwa sipati wanaume lkn nikiwapata leo kesho wanataka walale na mimi kwa mtu alieokoka sawa sawa hawezi kukubaliana na haya labda akina Koku ndio watakubali sio walokole waliookoka kikweli kweli
Uzuri wangu sikuwa najitangaza kazini wala kwa ndugu kuwa nimeokoka nilikuwa naulokole wa kimya kimya... nadhani unaweza niita mlokole wa chinichini
Kuona wenzangu wameshaolewa wote na mimi wanaume wanaonifuata wananiimbia nyimbo za ngono kwanza
Sikuona haja hata ya kuwapeleka kwa wachunga alafu mimi sikuwahi kuwa mtu wa wachungaji, nikiingia kanisani hautajua nikitoka hautajua, gari naacha ofisini naenda Kanisani kwa taxi, nikikaribia ananishusha mbali natembea mpaka Kanisani
Koku: at least wewe haukuwa mlokole zoba
Tereza: wanaume wakaja kukata wale wa mtaani, nikawa nawapata wa Kanisani
Tatizo la wa Kanisani walikuwa wavivu sanaa, wanakaa wanasubiria muujiza hawataki kufanya kazi
Koku: uhuhuhuhuuu! Hehehehehehe Preeeeach! sister Preeeeach!
Tereza: mnaanza vizuri ukija kumfuatilia analala kwa kanisa analala kwa ndugu nilipataga wanaume 10 wote hawakujua naishi wapi nilikodisha hata nyumba uswazi nikawa nawadanganya naishi pale basi tu lakini walokole wa kiume wavivu jamani loh
Basi nikaachaga kudate wapendwa
Koku: hahahaha eti wapendwa mxiuuui ndio mnajiitaga ivo ee?!
Mwana saikolojia: Koku tafadhali tupe utulivu muda sio rafiki
Tereza: nikapataga bwana mchungaji, doh jamaaa ni muhunii, anatembea na waimba kwaya nje ya pale, kunasiku nilienda kwake nikamfumania kabisa anazini na mwimba nyimbo za injili maarufu nikawasha taa kwani unadhani waliacha? ! Ndio kwanza akaniambia nisubirie hapo sebuleni nimhudumie huyu nakuja
Sikurudi tena kwenye maisha yake, na ile nyumba ya uswaz nikahama nikapanga uswaz kwengine
Basi siku moja tumeenda seminar ya vijana huko kanisa la Tabata akanifuata kaka mzuri mwenyewe anaonekana mtanashati, tukaongea akaniomba namba nikampa
Kuja kuwasiliana nae ni mtoto wa Mchungaji, alikuwa Malaya
Hatari, yani akitoka shetani anaingia yeye
Hapo nina miaka 29 nagonga 30, nazidi kuchanganyikiwa sijaolewa
Yule mtoto wa mchungaji akawa ananifosi nilale nae kinyume na ninavyotaka, mjinga sana kwanza Kanisani ukimwona anavyopiga gitaa utasema Daudi wa kwenye Biblia katika kitabu cha Agano la Kale
Fosi za hapa na pale kwenye geto lake nikamponyokaa nikaondoka nimeacha viatu ndani, maana Biblia inasema ikimbieni Zinaa nikakimbia kutoka nakutana na Dada mwimba kwaya anafungua mlango na funguo wala hakushtuka waswahili wanasema kisu chenye makali ndio kinaua mnyama
Toka hapo nikasema wokovu baaaass kama usanii ndio huu staki tena kuskia wokovu
Nikaanzaga kwenda Disco nina miaka 30, naenda Baa nakunywa ovyo narudi nyumbani usiku wa manane Uzuri nilishahama home nikapanga appartment Oysterbay, yani nikawa mtoto wa Yesu mwenye maumivu tele moyoni sikuwa na wa kunisaidia
Nikaanzaga kulia mwenye natafuta wanaume wanibake mara waniue naona kama nimeonewa kwanini maisha hayaendi?!
Ofisini nikapandishwa cheo nikaanza kusafiri na ma boss, tukasafirigi kwenda Kenya nikakutana na libaba limoja likanichangamkia ndio likanibikiri, toka hapo sikumwona tena
Toka nimebikiriwa na miaka yangu 31 sikuwahi kutulia utadhani shetani alifunguliwa huku chini ya kitovu changu, yani zile one night stand nilioigwa sanaaaa, kila mwanajme naekutana nae napugwaaa tena kavuuu nilipigwaaa midusheee nilipigwa machineeé mpaka akili ikakaa sawa nikaanza kuwa mjanja
Nikaenda kupima ukimwi sinaaa, mimba sinaa, nikajiambia kuanzia Leo mimi sitaki wanaume bora mradi nataka mabonge ya bwana
Basi toka hapo mimi nakaaga mahoteli makubwa, nikipata mzungu hayaaa, mwamerika mweusi twendee, mreno twendee, mchina twendee, mbongo twendee ila kwa nkingaa
Nilipigwa machine mpaka nikasahau Yesu anatamkwaje tena
Maisha yangu yalikuwa mabaya sana sana lakini sio kazini
Nikajaga kupata bwana wa kikurya jamani nilijutaaa yule bwana tulianza vizuuuri akanifanya nituliee kutulia kumbe yeye ni malayaaa, nikimfumania ananipigaaa, alafu alivyo mshenzi yule mjinga hakuwahi kutahiriwa Basi mechi ilikuwa mbayaaa yani doh kama una bwana wa kikurya achana nae mapema kabla hamjapiga shoo
Kwasababu alikuwa ananipiga sana, nikaamua kuachana nae akaanza kunifuatilia ilimuuumaa hajawahi kuachwaaa akaanza kunichania tairi za gari anakuja nyumbani anapiga kioo cha nyumba nikaamua kuhama kumbe kamuweka mtu anifuatilie akajua napoishi Basi akija ni ugomviii anapiga kioo cha gari anapigana na mlinzi nikaamua kwenda Polisi, Polisi wakaniambia huyu Bwana ana mtu wake juu tukimfunga kesho anatokaa na hizi kesi za kupiga wanawake anazo nyingi sana, cha kufanya hama mji au fanya chochote
Nikaenda kuomba transfer nikahamishiwa Arusha,
Nikabadilisha simu na namba naanza maisha yangu upyaaa, nikaanza kazi wiki ya 1 ya 2 ya 3 nipo supermarket akaja kijana mmoja akanipenda ananisalimia vizuri mimi nampotezea sitaki kumjua wala anijue
Akawa ananifuatilia akajua napofanya kazi, kila nikitoka kazini yupo getini, alikuwa gentlemen flani hivi ah mwisho wa siku Nikaamua kumsikiliza,
Tukawa marafiki mwezi 1 hajaomba chiu, wa pili hajaomba mechi, mwezi wa 3 akaomba kunioa nikasema eh huenda huyu ni Mungu nikakubali
Nikampeleka nyumbani mwezi wa 4, mwezi wa 5 harusi ikafungiwa Arusha, ndoa ikaanza, Tukawa tunaishi vizuri mwezi wa 1 mapenzi moto moto.. mwezi wa 2, wa 3, wa 4 nikashika Mimba, niliposhika Mimba tu yule bwana sijui alikuwa ameficha makucha, jamani nilikoma, nilikuwa napigwaaa kila akinywa pombe napigwaa nikavumilia vumilia ndoa changa ya miezi 5 na Mimba miezi 2, Mmasai alikuwa ananipigaaa akaniambia acha kazi kwa mana Yeye anahela za kunitunza, nikakataa, basi kila akirudi nikipigooo kasoro jumamosi na j2
Mimba ikakua miezi 8 ikafikia, kazini sikuacha kwenda nikazoea kipigo cha Mmasai akaja mama mkwe kusikia ninakaribia kujifungua, akaishi pale akajua kuwa mume ananipigaaa akamuonyaa akaacha wiki 3... Mimba ikaingia miezi 9 sasa muda wowote najifungua
Sikuhio mama mkwe amelala ndani anaskia tunagombana, jamani nilipigwaaa Nilipigwa miteke ya tumbo nilikumbuka majina yote ya Mungu wa Yesu Kristo
Namimi nikawa mbishi sasa akinipiga na mimi narudisha mechi, nachukua chupa nampiga anakwepa, nachukua meza namrushia anakwepa, nachukua kiti nampiga anakwepa akanikamata akanibana shingo sasa ananikaba kaba na wewe mpaka nashindwa kupumua akaja mamake anaachanisha hawezi mimi huku damu zimeshaanza kunichuruzika
Huku nakabwa huku ananipigaaa mateke ya tumbo Sikuhio nadhani nilipigwa kuliko siku zote nilizowahi kukaa kwenye ndoa
Mamake akachukua Fimbo akampiga mgongoni akaanguka chini, nikaachiwa na mimi chini sikukumbuka kitu najikuta hospital nimelala mama mkwe pembeni kalala, afande pembeni amekaa sikuelewa nikarudi kulala
Asbh nikaamka mama mkwe akaja anachekacheka nikamsalimia afande nae akanisalimia akanieleza kilichotokea kuwa mume wamemkamata yupo kituoni amewekwa ndani kwa kosa la kuua
Tereza: kamuua nani?
Mama mkwe: analia pembeni
Afande: mwanao umempoteza kwa kipigo cha jana kama sio mama mkwe na wewe ungepoteza maisha mshukuru sana Mungu wako
Tereza: nikalia wee mpaka wakaja kunichoma sindano nikalala
Baada ya siku 2 nikatoka hospital, watu wa ofisini wakaja kunisalimia nikawaeleza kila kitu boss akasema basi nikuhamishie Mwanza ukaanze maisha huko nikakataa
Mama mkwe akaja kurudi kwake Umasaini baada ya wiki 1
Baada ya wiki 2 akaja mwanasheria akanisainisha talaka nikasaini akaipeleka jela mume akasaini nikawa huru sasa nimerudi nilipotoka sina mume kafungwa maisha, sina mtoto amekufa, nikafanya kazi wiki 2 nikaona Arusha pachungu, nikaomba kurudishwa Dar maana mwaka na nusu umeshapita tangu nitoke Dar
Boss akanirudisha Dar nikapewa nyumba Mikocheni nikawa naishi hapo na kazini sio mbali
Yule mchumba aliekuwa ananipiga mpaka nikaomba uhamisho alikuja kufungwa maana alimpiga mtoto wa Chief mmoja hapa nchini wakamweka ndani ndio ikawa pona yangu kwa maisha ya Dar
Tangu hapo na sasa nina miaka 34, sijawahi kutaka mahusiano tenaaa, nipo singo sitaki kusikia wanaume wala mapenzi
Mimi nipo singo kwa kupenda
Kanisani sijataka kurudi tena kwa Walokole nasali Lutheran kwa Dini ya wazazi wangu
Huenda wokovu umewasaidia wengi ila sio mimi kwakweli
Nampenda Mungu sana na nasali sana, namtumikia Mungu kwenye huduma ya Mwalimu Mwakasege, hio inatosha kwa sasa
Wanaume kwa sasa hapana ngoja Kwanzaa nipone kidonda
TUONANE J3 TAR 21 MAY 2018 SAA 1 USIKU YA TZ
Ovyo kama yapi shemeji?!hahaha... Money Penny story zako zinafurahisha sana...
Ila wanawake saa zingine mna moyo sana daah!
Alafu kwa nini walokole wanashutumiwa sana kwa mambo yao ya ovyo...
Cc: mahondaw
Jamaani pole saana rafikiNipo Single kwasababu sina fedha za kumtunza mke pili maisha yangu mda mwingi nashinda porini kukata miti na kuchoma mkaa sina mda wa kurelax na kupiga mikasi maana nikifanya hivyo nitakosa hata hela ya kula,nazichanga nipate mtaji wa kuanzisha hata Duka ili nipate mda wa kuwa home hapo ndio nitafuta mwanmke,
Jomoon shem stori zangu zafurahisha nini tenaahahaha... Money Penny story zako zinafurahisha sana...
Ila wanawake saa zingine mna moyo sana daah!
Alafu kwa nini walokole wanashutumiwa sana kwa mambo yao ya ovyo...
Cc: mahondaw
Inshallah,Kuna Mtasha si Unajua Mji wa Kitalii ARUSHA alinipatia Wireless Router aliweka Bundle ya Mwaka Mzima kama zawadi so huwa nateleza nayo tu.Jamaani pole saana rafiki
Mungu Akusimamie ufanikiwe ndugu
Ila nashangaa jamii forum unaingia kwa hela zipi za vocha?!
Ukimaliza kunijibu usome hadithi hii anzia page ya 6 uje ya 9 uje ya 11