Story: Kutega(Seduction)

Story: Kutega(Seduction)

SEHEMU B: ROCK CITY BE LIKE

Andrew kweli akasikikiza ushauri wa marafkizake akaamua kumchukua Michael amsindikize kwenda mwanza kwa mpenzi wake Caren

Location alipo Caren, alitajiwa na Mr Pit baada ya Bella Bunny kumwambia wanaenda mwanza wiki nzima kum support rafiki yao anauguza

Wakatua mwanza kiroho safi, Wakalala mjini maana Michael ni cha uvivu, asbh baada ya kupata cha tumbo wakaanza kuulizia mwanza kwa Caren, uliza uliza hamna anaepajua wakaamua kwenda serikali za mitaa wakauliza, uzuri baba wa Caren ana urafiki wa karibu na mwenyekiti wa serikali za mitaa

Wakaondoka na mwenyekiti kufika karibu na kwa Caren, Andrew akaanza kuogopa hii ilitakiwa kuwa surprise kwa Caren sasa mambo ya kwenda official vepee?!

wakamwomba mwenyekiti tafadhali usiingie ndani, acha tupite kwa nje unionyeshe alafu mimi na rafkiangu tutarudi baadae, nataka nimfanyie Caren surprise nataka nije na wazee kuleta mahari sasa nikienda mimi sio vizuri namvunjia heshima nami kwao sitambulikani

Mwenyekiti akakubali wakarudi, Michael anacheka Andrew kimyaaa!

Ilipofika saa 10 jioni, wakiwa hotelini Andrew akamwambia Michael saa 12 jioni inawadia, sasa tujiandae twende kwa Caren, nataka niongee nae sasa sijajua movement zake zipoje ni hospital kwenda nyumbani au hospital anakaa muda wa siku ngap?!
Michael : twende sasa hivi tukakae pale tuone movement kwenye gari, alafu tumwulizie vijiweni movement zake alafu uende kumcheki ndani
Wakafanya routine mpaka kwa Caren, kumcheki kijiweni Caren hajulikani ndio nani?!​
wakawanga-wanga pale mara wanamwona Caren anapita anatoka dukani, Michael anamwuliza au ndio huyu demu mwenyewe?!
Andrew kumwona Caren akapata ganzi, yupo anaongea na simu huku analia akamkimbilia Caren! Caren! we Caren wewe! Caren kugeuka, tobaaa ni Andrew!
Akamshangaa Andrew?! umekuja lini hapa!?
Andrew: kumkumbatia hataki kusikia maswali, kimahaba, Caren analia, simu bado haijakatwa yule aliempigia upande wa pili anaskiliza
Andrew: mbona unalia mpenzi?! Kuna nini?! Nani anakupigia simu mpaka unalia?!
Caren: (akadanganya) hapana ni mama bado anaumwaa amelazwa, sasa naambiwa hali yake mbaya hata sijui nafanyaje na nimetoka hospital ndio napigiwa simu vocha ikaisha nikaja kununua
Andrew: pole jaman! huku anamchum chum,
Michael yupo kwenye gari anawaangalia huku anatafuna mahindi!
Andrew: Usijali mpenzi, nimekuja mimi tufanye mipango ya kumwuguza mama, kama hospital hawaeleweki tukamwuuguze hata nje ya nchi
Caren: akawa anashangaa, Huyu Andrew king'ang'a balaa!
Lakini Andrew mimi si nilikwambia kuwa sitaki mahusiano na wewe tena, tafadhali niache, sidhani kama nataka kukuhusisha kwenye matibabu ya mama, nimeamua kuwa single kwa sasa
Andrew : ndio nilikuskia lakini sijakuelewa, ulikuwa una maanisha nini Caren, najua unauguza na unachanganyikiwa hauna muda na mapenzi, sasa kwanini tusiuguze wote?!
Caren: siwezi tena mambo ya mahusiano na wala sitaki ( hapo simu haijakatwa upande wa 2 kuna mtu anasikia)
Andrew: hapana Caren siwezi kukuacha uende tu hivi hivi kwasababu unauguza, ujue mimi nakupenda sana Caren usinifanyie hivyo tafadhali, kuuguza tutauguza wote
Caren akakakataa katu katu hamtaki tena Andrew,
Sasa Andrew akawa mkali, kuna nini lakini? kwanini unautesa moyo wangu?!
Caren : Akakaa kimya kwa dk 2,baadae akamjibu sikupendi bwana niacheeeee
Andrew: haiwezekani ukawa haunipendi, mbona tulikuwa tuna do kitandani unasema unanipenda, kila tukiwasiliana kabla sijakupeleka nyumbani unasema unanipenda sasa kitu gani kimetokea siku ile mpaka ukakimbia nyumbani hautaki kutambulishwa?!
Sijakuona tena mpaka leo, haujui kiasi gani nimefurahi kukuona, (huku anamkumbatia Caren na kumchumu) navyokupenda mpenzi wangu, mmmh! basi yameisha najua ulipaniki kutambulishwa hio inaeleweka



Caren: akajinyofoa, kuangalia simu bado ipo hewani, akaikata simu haraka haraka

Andrew ngoja kwanza, kuna kitu nataka nikueleze alafu utajua kwanini sikuile nimekimbia kwenu na kama bado utaendelea kunipenda

Andrew: haya niambie nakuskia au tukakae hotelini kama kusimama hapa unachoka

Caren: hapana tuongee hapa hapa kabla giza halijaingia

Andrew kabla sijakufahamu wewe nilikuwa na mahusiano na mtu, ambae unamjua sana ni familia yako,

Andrew: sawa, kwahiyo? Tatizo likowapi au bado mna mahusiano na huyo mtu?!

Caren: sikujua kama utaweza kunisamehe lakini ndio maana nataka kukatisha mahusiano na nyie wote wawili na naomba unisamehe sana maana sikujua kama mnajuana, ningejua nisingeendelea kabisa na wote tafadhali naomba unielewe

Andrew: akaanza kuwa na wasiwasi na Caren kitu gan tena anaongea?!

Caren: Andrew nimekuwa na mahusiano na Baba yako mzazi kwa muda mrefu sana, tangu nipo na miaka 20 chuoni, alikuwa Shuga daddy wangu na ndio amenisaidia kupata kazi na mpaka nakuwa manager ni yeye kaweka mkono kama God father

Andrew hapo keshabadilisha sura, kesha changanyikiwa, anafura hasira, yani kama hulk kwenye movie vile,

Caren akaendelea kushusha ukweli;

Sikuile nimeenda kwenu, nikiwa natoka chooni nilikutana na baba yako, akashangaa nimefikaje nikamwelezea natambulishwa uchumba namsubiria baba mkweee, akakasirika sana hakutaka kusikia pale alipojua wewe ni mchumbaangu

Andrew: Caren upo serious kweli?! Wewe unatembea na baba yangu ambaye ni mume wa mtu kwa zaidi ya miaka 4, haukujua ameoa au?!

Caren: baada aya kujua ameoa nikakaa nae mbali lakini mtu kama baba yako mwenye power mjini, huwezi kumkwepa nikamwambia mimi nataka kuolewa natafuta bwana akanikatalia hakutaka kusikia tena akanitishia

Nilipokupata wewe nikamficha kabisa sikuwambia

Andrew: kivipi?! Umewezaje kuwa na wanaume wawili kwa wakati mmoja?! Unalalaje na mimi alafu na baba yangu?! Huu ni mwili au wewe ni pepo jini makata?!

Hakuna siku hata 1 ulinizuilia mwili wako na sijawahi kukosa ku enjoy mechi na wewe, kila siku unanipa style mpya tofauti tofauti kitandani unanidatisha sana, inakuwaje unakuwa na wanaume wawili tofauti tofauti na bado unaweza kuwa mzuri na mtamu kiasi hiki?!

Caren: akaanza kujiliza!

Andrew: akamshika bega wewe Caren, kwanini umenifanyia hivyo lakini?! Akampiga kofi shavuni, la kwanza, la pili, la tatu Caren akaanguka chini, watu wakaanzaaa kujaa pale, ikabidi Michael afunge gari aakaachanishe ugomvi kabla shija haijawa kubwa

Kufika ishakuwa too late, Caren kashushiwa mingumi pua zote zimejaa damu, Michael akamshika Andrew, bro! bro! bro vipi tena nyie mnapendana na mnapigana tena? ! Kuna nini?

Andrew: Caren amenifanyia kitu mbaya sitakuja kumsamehe kabisa, anatembea na baba yangu na mimi kwa wakati mmoja

Watu: wakaanza kushangaa wananong'ona, aiiibuuuu wengine wanasema ah huyu mtoto wa mama nanihii yule anaumwa, si unajua tena zile za majirani, majirani wakaongeaa Caren yupo chini bado hajaamka analia, hapo saa 12:45 jioni kagiza kameanza kuonekana

Andrew akapiga teke Caren la tumbo, la matako la kichwa ikabidi wanaume waingilie kati wamtoe Andrew fasta asije akamuua Caren

Caren akachukuliwa na wasamaria wema, kumtenganisha na Andrew

Andrew: kwanzia leo usinijue jue tenaa, sitaki kukuona kwenye maisha wangu malaya mkubwa wewe! tena wewe ni zaidi ya malaya ni kahaba wa kufa na kuponaaa,
jezebeli mkubwa kabisa wewe!

Michael akamchukua Andrew twende bwana hii ishakuwa kesi ya kupiga mtoto wa kike, usije ukafungwa bure Andrew twende,
wakaondoka wakaingia kwenye gari nduki mpaka hotelini, Andrew anatukana, analia Michael anamwangalia hana hata cha kumwambia anamhurumia tu!

Andrew: mimi sitakuja kupenda tena kama ndio hivi, wanawake hawa hawana akili kabisa, akatukana weeee Michael anamwangalia tu!

Majirani wakampeleka Caren kwao, Baba Caren anashangaa vipi kimempata mwanangu,
majirani wakaeleza kila kitu ni fumanizi mwanao kafumaniwa na bwanake barabarani anachanganya baba na mwana, aibuuu! Baba mtu akamwingiza mwanae ndani, akafunga geti majirani wakaondoka

Basi Andrew akapoa wakalala, asbh wakaamsha popo wakapanda ndege kurudi Dsm!

Kufika Dms ilikuwa weekend, Andrew na Michael hao kwa mzee wa andrew akamkuta mama anatoka, Andrew akamrudisha, mumeo yule wapi mama,

Mama anashangaa leo baba yake anamwita mumeo, akamjibu amepumzika kuna nini mwanangu?

Andrew: nenda kamwamshe hapa la sivyo naua mtu

Mama: mmh! akaona isiwe shida, akaenda kumwamsha mumewe, kikao kikakaliwa

Mara wanaskia hodi Michael akaenda kufungua mlango kumbe Andrew alishawapigia wajomba zake na baba wakubwa wamekuja

Kikao kikakaliwa, Andrew akapewa nafasi na wazee ya kuongea yote na Michael shahidi pembeni, kweli Michael akatoa ushahidi kumbe alikuwa amechukua video wakati Andrew anampiga Caren mpaka anaenda kuamulia na matusi alikuwa anamrushia Caren wazee wanashangaa wamerudije Dar salama!

Wazee: Baba Andrew, shida iko wapi?! Kwanini unachepukaaa na watoto wako?

SHUGA DADDY: hili siwezi jibu mbele ya watoto wangu Andrew na Michael tutaongea wakiondoka lakini kweli haya mahusiano yapo kwa muda mrefu na sababu nitawapa, ila kaa mjue mimi sitamuacha Caren mpaka dada yako mjomba abadilikee

Mmh wazee wakaguna, kubadilika huko vepee?!

Wazee wakamuomba Michael, embu tokeni muende hata hapo grocery mkapate pombe alafu nitawaita, wacha tuongee kwanza sisi mengine tutawajulishwa baadae...

Basi vijana wakatoka haooo mpaka kwa Mangi kupata moja moto moja baridi

Wazee wakaendeleza hema zito

Shuga daddy akafungua: oh kuna siri kubwa sana hapa ambayo mimi najua imeendelea kwa muda mrefu,
Unajua ndoa yangu ilikuwa nzuri sana mpaka mtoto anaenda kusoma boarding form 5 huko iliboru, tulikuwa tunapendana sana na mke wangu sana sana, sikuwahi kuwa na mchepuko na Caren ndio mchepuko wangu wa kwanza na wa mwisho na mimi ndio nimemtoa bikra yule binti, kwahiyo hapa swala la ukimwi mimi sina labda shemeji yako au dadako mjomba.

Basi nilimfumania dadako ana kibwana huko ofisini tukayamaliza kimya kimya maana alisema ataachana nae, lakini alinilaumu nasafiri sana, ndio maana anani-miss, uzalendo ulimshinda ndio maana kachepukaa!

Mimi nilimsamehe lakini ule mchepuko ulimpa ujauzito mke wangu, na mchepuko alikuwa anajua akawa ananiletea dharau nyumbani kwangu na fujo, nikamfukuza kwa ngumi kabisaa akaondoka akasema atarudi na polisi sikumwona tenaa!

Nikijua atarudi kweli, lakini hakurudi ule ujauzito ukawa mkubwa sana, mpaka miezi 7 mimi nalisha kama kawaida si nimesamehe! mwezi wa 8 yule mchepuko wa mke wangu akarudi kuja kuangalia mtoto wake, nikagombana nae nikaita polisi wakaja kumtoa
Wiki hio hio Andrew akarudi toka shule likizo, anamkuta mama yake mjamzito wa mieiz 8 akajua hapa anategemea kupata mdogowake, mimi na mamake tukanyamaza kimya mpaka aliporudi shule

Baada ya mwezi mmoja akiwa anaelekea hospital na dereva maana mimi nilikuwa kazini, akapata ajali ya gari aligongana na Lori, alikuwa nusu maiti huyu mke wangu na dereva nae alikuwa mahututi sana, wakamuwahisha hapo muhimbili akapona na dereva wangu huyo hapo nje amepona ila mtoto ndio baaas Mungu alimpenda zaidi

Mchepuko alipoambiwa akasema mimi nimemuua huyo mtoto, baadae alipoeleweshwa na mapolisi, akakubali kusamehe tukazika, tangu hapo mahusiano na mke wangu yakafaa, Andrew alipomaliza mitihani yake ya form 5 kwenda form 6 akarudi tukamweleza, alilia sana,

Mama yake alikuwa ameshapona ni bado vitu vidogo vidogo tu ila asilimia kubwa alikuwa amepona, ndio tukawaeleza kuhusu ajali ya mke wangu ila hatukuwaambia chanzo maana hii ni ndoa nami nampenda mke wangu, basi maswahiba yakaisha,

Tukakaa baada ya mwaka mmoja Andrew akamaliza shule, akiwa anasubiri majibu, mimi nikawa nasafiri kikazi,
Siku hio narudi zangu nyumbani kwa surprise, namkuta mke wangu amelala na mtoto wangu Andrew, chumbani kwa Andrew uchi wa mnyama wote wawili, ina maana walitoka kuzini!

Wazee: tobaaaaaa, lahaulaaaa, sistaaaa ya kweli hayo?!

MAMA Andrew : kimya anajiliza,

Mjomba: akainuka akamzaba kibao begani, wewe dada unalalaje na mwanao, ivi kweli wewe una akili vizuri?! Ili upate nini sasa maana mumeo anakupa kila kitu!

Au kuna siri hapa mnatuficha nyie wawili?! Mali zenu ni za uchawi mnatembea na watoto wenu au? !

Shuga daddy: hamna mimi kwa upande wangu sina ushirikina, hizi mali zangu ni za urithi na wewe kaka yangu unajua, hatuna historia ya kutembea na watoto wetu wala kuua ndugu wala wazazi wala kafara yoyote, sisi sio free mason kabisa!

Kweli kaka wa Sugar daddy akakubali, likabakia kwa mama Andrew

Anaulizwa kilichokufanya atembee na mtoto wake wa kuzaa ni nini akawa hana cha kujibu

Baba Mkubwa: unajua wachaga nyie mnalalaga na watoto wenu huenda alikuwa anadumisha mila bwana mjomba au sio?!

Mjomba: akaja juu sisi hatupo hivyo kabisa huyu labda ana yake atueleze kwakweli wachaga hatupo hivo asee! haya ni mambo yao dada na shem, kwanini nae shem ameenda kutafuta katoto kadogo hapa kuna siri hawa wachawiii wote 2

Sugar daddy: akakataa

Sugar daddy: labda mjomba, dadako akwambie kwanini alitembea na mtoto wake kwanza alafu utajua ukweli upo wapi

wazee: wakamwamuru Mama Andrew aongee ukweli kabisa wala asifiche ili waweze kumsaidia!

Mama Andrew: mimi nimekosa kabisa kuwa na mtoto kupitia mume wangu, na Andrew tumempata kwa bahati sana, mume wangu tangu apate ajali, akapata na kansa na ile chemotherapy na mambo ya Mionzi aliochomwaa, mbegu zake za uzazi haziwezi tena kuzalisha sasa na mimi bado nataka mtoto ndio maana nikatembea na yule mchepuko nikapata mimba ila mume wangu hakutaka kabisa mtoto huyu na najua ile ajali ni yeye kasababisha

Shuga daddy; kivipi labda? Mimi ninao ushahidi kuwa nilikuwa mbali na nyumbani!

Mama Andrew: basi tangu mtoto yule kufa ananichunga chunga sana, nikaamua kumlevya mtoto nikalala nae by the time anatufumania Andrew hajui chochote nikatokaa chumbani na mume wangu ambae alikuwa ana ghadhabu kali sana, nikaenda kuongea nae lakini hakunielewa ndio kaenda kutafuta huyo kimada wake Caren, kitu ambacho Caren hajui ni kwamba huyu baba hazalishi tena na mimi hapa tayar nina mimba ya Andrew miezi 3

Wazee: lahaulaaa imekuwa mimba tena?!

Shuga daddy: sio kweli huyu hana mimba ya Andrew maana haya matukio ni miaka 5 iliopita mimba anaibebaje leo?!

Mama Andrew: tuliendelea na mahusiano?!

Shuga daddy: Andrew akiwa amelewa, amelala au?!

Mama andrew: Akiwa na ufahamu kabisaa

Shuga daddy: sio kweli, ngoja ndugu zangu, subirini hapa hapa, akaenda kumwita dereva

Dereva akaja, wewe dereva embu Waambie hawa kaka zangu na shemeji kuhusu mke wangu

Dereva: mama Andrew tumekuwa na mahusiano ya siri kwa muda wa miaka 3 sio 5,
Mzee akisafiri mimi na yeye tunajivinjari, mahotelini nje ya mkoa, nje ya Tz Akienda biashara zake kwasababu mimi ndio namwendeshaa, njiani tunapaki tuna-do! ila miaka yote tulikuwa tunaenda na kinga

Sasa mwaka m1 uliopitaa mama Andrew akaniambia anataka kuomba talaka kwa mume wake ili aishi na mimi, maana anataka mtoto na mapenzi kwa Baba Andrew yameisha, sikujua kama Baba Andrew anaturekodi kwenye gari, kuja kushtuka record ishafanyika na mzee keshaskia nikanyamaza sikumwambia Mama Andrew,

Tuliendelea bado na mahusiano ya siri ila mechi tukawa tunacheza bila condom maana tulishapima afya zetu

mwezi uliopita Mama Andrew akaja kuniambia ana mimba ya miezi 2, niliogopa sana

Juzi mzee akanifuata baada ya kurudi toka safari akauniuliza kuhusu yale maneno ya kwenye gari, akaniambia kabisa nichague kati ya kazi pale au aniachie mke!

Kuhusu mimba ni ya Andrew sio kweli, maana kabla hajafumaniwa na Baba Andrew hapa, tulipanga mimi na Mama Andrew amnyeshe dawa Andrew akalala akamvua nguo zotee akaniita hapo hapo chumbani tukazini kitandani kwa Andrew, Andrew akiwa amewekwa kwenye kochi, tulipomaliza mimi nikaenda kuoga nikaondokaa, akamrudisha Andrew kitandani na yeye akajilaza, ilikuwa ni mipango tumepanga na mama kumfanya baba akasirike achukie atoe talaka ili tuweze kuishi pamoja.. mama hakujali tena mali za mumewe alitaka mtoto inaonyesha mtoto kwake ni mali kubwa mama hakuridhika na Andrew, kusema ukweli hio mimba sio ya Andrew kabisa ni ya kwangu mimi.

Wazee wakachokaa! sawa Dereva tumekusikia lakini usije ukawa umelipwa na Shuga daddy hapa uje uongee uongo, ili dada-yetu aonekane mbaya

Baba Mkubwa: Ivi shemeji, haya maneno anaongea dereva ni ya kweli?!

Mama Andrew: ndio shemeji ni ya kweli

Baba Mkubwa: unaweza ukayasema mahakamani, au unatuambia tu hapa ili ugomvi uishe?

Mama Andrew: Ni kweli na nitasema ukweli mpaka mwisho! wala sitageuka!

Wazee: Wakashangaa! shemeji kawa Mbogo!
Sawa dereva naomba utusubiri nje tufikie hatima kwanza na naomba usihame hapa mpaka kikao cha familia kiishe ndio tutakuruhusu uondoke na mama Andrew au la..

Wakakubaliana na Shuga daddy akakubali, sawa atabaki pale mpaka hatima ifikiwe, dereva akatoka zake nje

Shuga daddy: mnaona mimi ndio maana nasema sitakaa nimuache Caren kwa upuuzi wa shemeji / dada yenu

Wazee wakashika kichwa maana hii kesi ishakuwa kubwaaa!




TUONANE TAR 3 MARCH 2018 SAA 1 USIKU YA TZ
Hii hapa ndio ilifikia mwisho? Maana kwenye ile ya mahusiano inayoendelea umesema hujawahi kuweka story bila kumalizia.
 
Back
Top Bottom