Habari wanajamii wenzangu!
WanaJamii kumradhi, nimechelewa kurudi, nilikuwa na ugeni mzito ofisini!
Tuanzie hapa leo:
Rafiki yangu. Mimi sijui. Nakiri mpaka sasa hivi, sijawahi kujua nini kilitokea, sijui nini ulikifanya, nikaanza kuyaskia maneno yanayoeleweka kutoka kinywani mwako. Ulizungumza kwa ufasaha sana, neno kwa neno! Macho yako yalionyesha nini ulimaanisha ktk maneno yale. Kulikuwa na mkazo wa ziada.
Nilielewa kila neno. Kuna wakati uliweka nukta lakini bado niliendelea kuskia unachosema. Japo kuna nukta. Akili ikanambia, nazungumza na mgonjwa mwenye uwezo mkubwa wa kujielezea. Sikuamini. Naomba ninukuu ulichosema:
"Manabii wameondoka na maajabu yao! Mungu ana njia nyingi za kuonyesha maajabu yake sasa! Siamini. Siamini kilichonifika. Hapa wodini kuna bibi ana karedio kadogo hivi, asubuhi amenisikilizisha matangazo! Polisi wameeleza taarifa zangu katika radio. Wamesema kuna binti amegongwa jana usiku na gari ndogo maeneo ya Ubungo, kisha gari haikusimama! Kuna msamaria mwema amemuokota majeruhi huyo, na sasa hivi anaendelea na matibabu Muhimbili! Huyu bibi (ukanionyesha kwa uelekeo wa macho yako) akataka kujua kama ndio mimi, ndio akujia na kale karedio. Binafsi nikawa na maswali mengi sana kichwani, kubwa ni kama kutakuwa na uwezekano wa kumuona mtu huyu, alieokoa uhai wangu. Kumbe ni wewe! Ahsante sana, nimeipata fursa hii."
Yule nesi wetu alishaanza zoezi la kutimua watu. Watoke mle wodini, kwamba muda wa kuwaona wagonjwa umeisha. Kuna kitu sikuwa nimeelewa. Muda wote ambao nesi alikuwa akitimua watu mle wodini, huku akizunguka zunguka ktk vitanda ambavyo wagonjwa bado wanabadilishana salamu, mawazo na jamaa zao, hakujaribu hata kidogo, si tu kusogelea kitanda ulichokuwa wewe, bali pia hata kutupiga macho hakuthubutu! Sikuelewa. Baadae nikahisi labda nguvu ya chai ya dada mkubwa, penye udhia.....!
Rafiki yangu ukaendelea kutiririka. Wakati wote uliokuwa ukitiririka binafsi nilikuwa nafanya tathimini za jumla jumla, namna Muumba alivodhihirisha uwezo wake juu ya mwili wako. Ashukuriwe Mungu. Sikupoteza muda kuangalia maumbile yako ya chini, niliyaona vizuri sana jana yake ktk purukushani za kukupandisha katika ile STJ. Of course, katika lile zoezi, nilitumika kukushika maeneo ya kiuno ili kukupandisha garini, wengine sehemu za juu, wengine miguu, nilikuwa na picha halisi ya maeneo yako ya kiuno na vyote vyenye nasaba na kiuno. Mungu mkubwa.
Black beuty. Zamani ungeitwa maji ya kunde. Siku hizi wameboresha, wanasema rangi ya choclate. Mguu ulikuwa mguu kweli. Sio fito. Kimo cha wastani, wambea wanasema eti si mrefu, si mfupi. Sauti yako hata ingetoka gizani, ilitosha kumuaminisha msikilizaji wako kuwa anaskiliza sauti ya binti, hata kama si mrembo basi yatosha kusema ameumbika!
Ni katika mazingira magumu kama yale ya jana usiku, ndio unaweza kuhitaji kitu cha ziada ili uweze kujua majina, umri, eneo husika la mtu - manusra wa ajali kama ilivokuwa kwako. Kuviskia hivyo vyote ni jambo moja, kuvikariri kichwani ili niweze kuvitumia na kutoa maelezo baadae, lilikuwa jambo jengine. Mimi niliweza. Sauti ya kike hasa (Nimeikumbuka sauti ya Spika)! Ningeshindwa vp wakati kwa sauti yako tu, ilitosha kurahisisha zoezi la kukariri.
"Nakushukuru! Sijui hali ingekuwaje kama sio wewe. Ajali za barabarani, huwa zina changamoto nyingi sana, na hasa katika miji mikubwa kama DSM! Ningeweza kuachwa pale, vibaka wangejipatia riziki yao, watu wangenipita, hakuna wa kutoa msaada kwa majeruhi wa ajali, tena nyakati za usiku, nadhani ilikuwa ni kifo. Una moyo kaka, una moyo wa ajabu sana.
Nakushukuru sana kwa wema wako, Mungu akubariki sana ndugu yangu!
Nipe namba yako! Haaa – sasa nitawasiliana vipi na wewe? Unakaa wapi? Unafanya kazi gani? (idadi ya maswali iliongezeka zaidi) Daaah, sasa nakuomba fanya kitu kimoja, jitahidi kadri ya uwezo wako usikose kuja mchana wakati watu wanawaletea vyakula wagonjwa, usikose! Naomba ujue kitu kimoja, hao woote uliowaona wamentembelea hapa asubuhi hii, hamna mwenye nafasi ya kuja hapa mchana, watakuja saa 10, ni dada mkubwa tu ndiye atakaekuja mchana kuleta chakula. Mtakuwa wawili tu, wewe na dada! Si utakuja? Ni lazima uje, nataka uje mchana, kwangu ni muhimu sana wewe kuja hapa mchana. Leo"
Kwa kawaida binadamu huwa hawezi kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja, huwa inatokea mara chache sana. Kwa mfano, katika kubishana, huwa si rahisi wanaobishana wakawa wananong'ona, ni ngumu sana. Ndio ilivokuwa pale ktk kitanda chako, ilibidi tuanzishe mazungumzo rasmi. hatukuweza kunong'ona! Ukaniachia. Nilijikuta nikijimuvuzisha huku nikikuonyesha kuwa sijaridhika, nilitamani baada ya kuniachia, sasa unikumbatie kabisa, zamu yako kuniskiliza! Niskilize huku umenikumbatia! Haikuwezekana.
Maswali yako yote yalipata majibu hasi kutoka kwangu isipokuwa lile la unaishi wapi na lingine la unafanya kazi gani. Uso umeumbwa na haya. Nilijishtukia kubaki mahali pale – wodini, watu wachache sana, kama wawili ama watatu, huku wengi wakiwa wametimuliwa na Yule "nesi wetu" wengine waliobaki ni wagonjwa kama wewe. Nikakuomba tufupishe mazungumzo, kwamba ntakuja tuongee jioni, muda umefika na mimi niondoke, niwahi kibaruani kwangu, kwamba na wewe unaitaji kupumzika!
Nilikukatalia wazo lako la mimi kuja mchana, nililisisitiza kuja jioni. Muda wa mchana, nisingeweza kuja Muhimbili kukuona, kwa aina ya kibarua changu, huo ulikuwa muda wa kazi nyingi. Nilikueleza kuwa, ili niwahi Muhimbili kwa kutokea Mwenge, ilibidi nitoke mwenge walau sa5 asubuhi, na mpaka narudi tena ofisini itakuwa ni zaidi ya saa 8, hii itakuwa ngumu na hasa kukiwa na ukweli kuwa asubuhi nilianzia Muhimbili, na hivo kuchelewa kuingia kibaruani.
Wazo la kupoteza masaa kama matatu kwa safari yangu ya Mwenge – Muhimbili, ulilipinga kwa hoja kuwa, dada ako mkubwa, ofisi zake zipo maeneo ya Mbezi beach, na unao uwezo wa kuweka utaratibu na dada ako akanipitia mimi Mwenge, tukaja wote Muhimbili. Bado sikulikubali wazo hili. Akili yangu ilishahamia ktk aina ya kibarua changu, kwamba ukiwepo unaingiza – usipokuwepo na lako halipo, wewe hukulijua hilo! Nikajikuta natoa sauti ya juu kidogo kumuaga Yule "nesi wetu" na kumshukuru sana. Hatimaye nikatoka pale wodini kwa maelezo kuwa nitapanga na dada ako.
Tukiwa na jamaa zako, tunatembea kuelekea nje ya MNH, nilipata fursa nyingine ya kuwa karibu na "mtu wako." Nadhani kuna seminar alipewa, sijui na nani, mimi sifahamu. Nilimuona akiniongelesha. Safari hii kwa utulivu sana. Aliongea mithili ya mtu anaetaka msikilizaji wake, ajue kuwa yeye ana vitu vinavofanana na hekima, busara ama ustaarabu. Alijitahidi. Aliongea sana, maelezo yake yalionyesha kuwa anajutia vile ambavyo vimetokea baina yake na mimi.
Alitumia muda mwingi wa matembezi yale, kunishawishi niamini kuwa anajutia kile kitendo chake cha kutumia nguvu ya ziada katika namna ambayo baadae alijiona kuwa ni mpum***u. Hakutaka kusema samahani, nilishaelewa kuwa amemaanisha samahani. mkubwa hakosei. Sinaga kinyongo. Ndio kwanza nikamsifia kuwa anajua kupenda. Akacheka. Nikamsisitizia kuwa anajua kupenda, kiasi yuko tayari kupigana na mtu asiemjua, tena usiku, bila kujali huyo mtu ana silaha ama laa! Akaonyesha kufedheheka. Nilielewa kwa nini moyoni mwake mbegu ya chuki ilichipua. Chuki kwa Msamariamwema aliemsaidia mpenzi wake. Mwanaume akifanikiwa kummiliki kiumbe wa mfano wako, huwa kuna artificial intelligence inaji-install kichwani mwake! Wivu!
Dada ako aliingilia mazungumzo kati yangu na mbaya wangu. Alitaka kujua naelekea wapi. Nikamjibu mwenge. akaniomba tuzungumze kwa dakika chache, kabla hatujaachana, kwa sababu anataka kwenda Ubungo kufuatilia vile vitu vyako - mdogo wake, vitu nilivowatajia jana usiku, manusra wangu wa ajali. Aliitumia fursa hiyo vizuri na kuniuliza mambo mengi sana. Aliniuliza kuhusu wazazi wangu, aliniuliza kuhusu ninapoishi, naishije? Na kina nani?, aliniuliza kuhusu shule, aliniuliza kuhusu kibarua ninachofanya, kisha akaniuliza kuhusu wewe. Akaniuliza kuhusu mahusiano, akaniuliza kuhusu wewe, manusra wangu wa ajali! kuhusu wewe, kuna kitu akanambia. Kwanza alisita. Kisha akasema: