miss ngatara
JF-Expert Member
- Apr 6, 2014
- 473
- 167
Nisamehe mimi, lakini si hata kuandaliwa pia ni raha, hata kama mwisho wa mapishi hukuuona! aaah, aaah, aaah!
Namalizia taraweh! Nitarudi Miss!
Mbona hujarud tena jaman, njoo bas sasa hivi
Nisamehe mimi, lakini si hata kuandaliwa pia ni raha, hata kama mwisho wa mapishi hukuuona! aaah, aaah, aaah!
Namalizia taraweh! Nitarudi Miss!
Mbona hujarud tena jaman, njoo bas sasa hivi
Halahala, usije ungamtengua udhu mwenzio
Huwa napenda Kusaidia watu hasa hasa jinsia ke, kama Maria nilimsaidia sana
Vuta subira Mkuu lin
Poleni kwa kusubiri, hatimaye nimerudi:
Rafiki yangu kuna kosa ukalifanya.
Hukujua kama ni kosa. Baadae nikaja jua lilikuwa kosa kubwa. Wakati tumeshaagana na wewe, tunaondoka kama kikundi cha wanafamilia moja, mimi na wale jamaa zako, ukaniita kwa jina langu (ambalo ulilijua muda mfupi tu, tangu tufike pale kitandani kwako, jina langu halisi lina herufi 4 tu, na ni moja ya majina common sana kwa watanzania wengi, sijui kwa nini)
Kosa la pili.
Bila kujijua. Na mimi nikaitikia wito wako. Nikarudi peke yangu. Huku wale wengine kwenye ile convoy wakiwa wamebutwaa, wanaangalia nini kimetokea. Hawakwenda. Hawakurudi. Walisimama. Wakaona ulivokuwa unaniomba nikuinamie pale kitandani. Na mimi nikatii.
Kosa la tatu. Mara, ukaonekana unaninongoneza sikioni.
Nakukumbuka rafiki yangu, na hapa kama nakuona na mguu wako wenye POP, juu ya kitanda! Umeunyoosha. Nilikuwa katikati ya kukusikiliza na kutokukusikiliza. Nadra sana mimi kuwa ktk hali kama hii. Ni moja ya nyakati ngumu sana kuwahi nipata. Mie. Jf wananijua kama slim5. Mimi. Mwenyewe.
Binafsi sikupenda namna lile jopo la jamaa zako, walivokuwa wakinipa heshima ile mbele ya mpenzi wako. Masifa tele. Tena masifa yanayotaka kwa watu wa jinsia kinzani na ya kwangu. Mbele ya mtu wako. Niliyahisi maumivu ambayo jamaa yako alikuwa akiyahisi.
Ni kama vile wewe rafiki yangu na wale jamaa zako, mlimsahau mtu Yule. Mlisahau nafasi yake. Ni kama hamkutambua uwepo wake pale. Aliumia. Na mimi niliumizwa na picha ile. Kama wa kiume, nilihisi namna gani inaumiza aina ile ya mapito. Ilibidi iwe. Ikawa.
Nikiwa kati kati ya kukusikiliza na kutokukusikiliza, nikaskia ukilisemesha sikio langu. Kwa kuwa nilishakuwa na msongo wa mawazo kichwani, wala sikuelewa. Sikuelewa ulikuwa unasema nini. Niliskia sauti yako ikitoka katika mfumo wa maneno. Sikuelewa maneno yale yalibeba maana gani. Uliponiuliza nimeelewa, nikajibu, ndio.
Pamoja na nyakati ngumu uliokuwa nayo siku ya kwanza pale hospitali, bado uligundua kuwa sisemi kweli. Nakudanganya. Uligundua kuwa nimekubali kukuelewa huku nikiwa sijakuelewa. Uliongeza nguvu ktk mkono wako ulioshika shingo yangu. Nikahisi maumivu. Nikajikaza kisabuni. Nilifundishwa kujikaza penye maumivu, na hasa kama anaeniumiza ni mtoto wa kike. Hakuna mwanaume mkamilifu alie tayari kuonyesha udhaifu wake kwa mtoto wa kike. Nikajikaza. Ukasisitiza sana.
Wakati wote wa hii scenario, wale jamaaa zako pale karibu na mlango wa kutokea wodi hii, walifanya kama kigenge na kuwapisha wengine wenye haraka ya kutoka, watoke. Hawakuwa na sehemu nyingine ya kutazama. Walitutazama sisi. Walintazama mimi. Wakakutazama wewe. Ni kama tulikuwa tunaigiza. Igizo la watu wawili. Mgonjwa kwa upande wake. Msamaria mwema kwa upande wa pili. Kuna kitu kilinipata. Mshangao.
Nilishangaa kuona hujali kitu. Hujali wale jamaa zako, hukujali uwepo wa boyfriend wako mtata rafiki yangu, yote kwa yote rafiki yangu hukujali kwamba pale ni hospitali, kwamba upo ktk kitanda cha hospitali, kwamba wewe ni mgonjwa na mimi ni Mtembezi tu pale hospitali!
Rafiki yangu, nilishangaa kuona hukujali kile kikundi cha watu ulichokisababisha pale mlangoni, watu ambao nilikuwa najua kuwa muda mfupi baada ya kutoka pale, watakuwa maofisini kwao wakiwajibika. Ulikuwa unawachelewesha. Ukasababisha minongono kati ya dada zako. Wakawa wanaongea ktk namna ambayo mimi na wewe hatukuweza kuskia kitu. Ni hapa, kwa mara ya kwanza nikamskia jamaa yako mtata akichangia ktk majadiliano yale. Tena alichangia maelezo ya memba wengi ktk kundi lile.
Mchelea mwana kulia, hulia yeye! Ndio ilivokuja kuwa. Huku mimi na wewe. Kule wanafamilia na mpenzi wako. Mtafaruku. Wakapishana Kiswahili. Dada ako mmoja na shemeji yako, lugha zikagongana. Chanzo, mimi na wewe hatukukijua. Mzozo wa watu wanaogombana huku wanajitahidi makelele ya mzozo wao yasisikike. Hatukuwaelewa.
Rafiki yangu. Mimi sijui. Nakiri mpaka sasa hivi, sijawahi kujua nini kilitokea, sijui nini ulikifanya, nikaanza kuyaskia maneno yanayoeleweka kutoka kinywani mwako. Ulizungumza kwa ufasaha sana, neno kwa neno! Kama si wewe uliefikishwa MNH pasi na fahamu. Macho yako yalionyesha nini ulimaanisha ktk maneno yale.
Kulikuwa na mkazo wa ziada. Niliskia. Nilielewa kila neno. Kuna wakati uliweka nukta lakini bado niliendelea kuskia unachosema. Japo kuna nukta. Akili ikanambia, nazungumza na mgonjwa mwenye uwezo mkubwa wa kujielezea. Sikuamini. Naomba ninukuu ulichokuwa unanambia:
Story nzuri sema inakata stimu kusibiria next part
Munkari samahani, hilo uwa kichwani ni la kitambaa ama natural!
Haha yani anatukatia stimu mi ananiudh