STJ 974 Iko cocobeach imeleta wanakwaya kurekodi video

hii kitu haina kuremba, wanatumia muda wa dereva, mafuta, wear and tear ya mali za serikali kwenye kwaya huku tunakosa dawa mahospitalini

someone lazima awajibike
 
Ni kwaya ya aina gani?. Kuna kwaya za dini na nyingine siyo za dini. Inaweza kuwa kwaya ya shule, polisi, jeshi n.k.

Kwaya ya dini mkuu, wamerekodi kuanzia mishale ya kumi na nusu hivi, saa kumi na mbili ndio wakawa wanamaliza, ni kwaya ya dini.
 
Hata magari yaliyombeba na kutumika kumtesa dr ulimboka huwezi jua yalikuwa ni stj,stk au hata su.hayo ni mepesi tuu unayoweza kuyaona toka kwa mfumo uliooza na unaoanguka kama ccm.
 
Kumbu kwaya tu!, hujui kwamba zinahubiri amani na upendo na kuasa watu waache maovu, sioni tatizo labda ingekuwa imebeba madumu ya gongo,machangu au magaidi.
huwezi kuleta utetezi dhaifu namna hii, ingekua wanenda kwenye maulid ungekua wa kwanza kuja kubwabwaja hapa na milalamo kibao

i ma a christian na sikubaliani na ufujaji huu
 
chief mi nilikuweko wakati wanafika na hadi walipoanza kufunga mizigo yao, ilikua ni kwaya ya kanisa, walikua wana-shoot video za nyimbo zao, nimeweka nambari ya gari, wahusika wafatilie watajua, kuanzia saa kumi hadi saa kumi na mbili tarehe 21.Aug.2012 gari nambari STJ 974 ilikua wapi na nani alikuwa nayo?

Mkuu, rekebisha hiyo tarehe. Ni 21.07.2011 na siyo 21.08.2011
vinginevyo uko sawa kabisa.
 
chief mi nilikuweko wakati wanafika na hadi walipoanza kufunga mizigo yao, ilikua ni kwaya ya kanisa, walikua wana-shoot video za nyimbo zao, nimeweka nambari ya gari, wahusika wafatilie watajua, kuanzia saa kumi hadi saa kumi na mbili tarehe 21.Aug.2012 gari nambari STJ 974 ilikua wapi na nani alikuwa nayo?


August 21? Kumbe gari lenyewe hata bado halijaja ila linatarajiwa kuja hapo. Ahsante nabii.
 
Gari ya serikali, Defender yenye usajili STJ 974 iko cocobeach imeleta wanakwaya ku-shoot video, imewaleta imewasubiri wamefanya shooting na sasa ninapoandika hii wanapakia mizigo yao kwenye gari tayar kwa safari ya kuondoka.

Haya ni matumizi sahihi ya haya magari? picha coming soon!

Itakuwa wamekodi, manake kuna halmashauri nyingi hufanya biashara ya kukodisha baadhi ya magari yake..Mf. Maswa
 
Mkuu, rekebisha hiyo tarehe. Ni 21.07.2011 na siyo 21.08.2011
vinginevyo uko sawa kabisa.

hasira chief, lakini kuna mdau humu anasema ni utaratibu wa kawaida, eti halmashauri kumbe zinaruhusiwa kukodisha magari yao kwa matumizi ya watu, hii ndio nasikia leo

 
August,21, 2012 bado haijafika, kwa namba hizo stj 974 itakuwa ilishauzwa kama gari chakavu hilo.
 
Mimi ssidhani kama kuna kosa kuazima gari la selikali,kwani wanakwaya sio wananchi? matumizi mabaya ni kama kwenda kwenye ulevi umalaya nk,lakini kuwezesha wananchi kunadhambi gani hapo.

Wana JF tusiwe kila wakati ni NEGATIVE thinking kwa straight issues kama hizi. Wananchi wametumia gari la serikali yao kwa jukumu ambalo naamini ni la kijamii maana mleta uzi hajasema ilikuwa inarekodi nyimbo zenye maudhui gani. Hata kama ni kaswida au Yesu kwa sana, ubaya uko wapi? Serikali imeahidi kuwasupport wasanii na inatimza, ikiacha mnazoza!!!!!!!!!!!1
 
Yaani hii ni aina ya ufisadi mwingine dhidi ya mali za umma.. Nakumbuka enzi za mwalimu magari ya Serikali ilikuwa marufuku kuonekana ciku ya Jumamoci kuanzia saa nane mchana.. Na ciku nzima inayofuata ya Jumapili.. unless kipatikane kibali.. Ciku hizi w/ends magari ya serikali ndo yanakuwa mengi barabarani na sehemu za starehe.. Kama hili inawezekana dereva kadaka tenda.. Au amejitolea kanisani huko.. Au mbaya zaidi boci ndo kaamuru gari litolewe.. Yote kwa yote ni matumizi mabaya.. Serikali inalipa zaidi ya dola milioni 35 kama gharama ya mafuta kwa mwaka..!
 

hasira chief, lakini kuna mdau humu anasema ni utaratibu wa kawaida, eti halmashauri kumbe zinaruhusiwa kukodisha magari yao kwa matumizi ya watu, hii ndio nasikia leo


Safi sana hii,
Next week mdogo wangu anaoa, so nitaenda magogoni kuazima/kukodisha zile BMW.
 
Alafu inaonekana ni gari ya Polisi hiyo.

ni STJ 974
, lazime wenyewe wanajua ni ya nani, kama kuna mtu humu atuambie hii STJ 974 ni ya watu gani?

najua lazima itakua ya idara au ofisi iliyoko serikali kuu maana wao ndio wenye STK, STJ, STG nk hawa wengine wa halmashauri zao huwa ni SM kama sikosei

 
mkuu inawezekana kigogo kakopeshwa {kauziwa) la serikali , ili kukwepa "kodi na trafic" huwa wana acha plate namba za STJ kwa muda.
 
Mfumokristo uko kazini! Ingekuwa niwaislam basi comment zote zingeelekea kwa Watu flani kwamba wanaleta udini! UDINI wenyewe ndio huo! Hii inatokana na Mfumokristo ambapo inaonekana sio tatizo kabisa. Jamani Mfumokristo unaifilisi hii nchi.
 
Back
Top Bottom