STJ 974 Iko cocobeach imeleta wanakwaya kurekodi video

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Gari ya serikali, Defender yenye usajili STJ 974 iko cocobeach imeleta wanakwaya ku-shoot video, imewaleta imewasubiri wamefanya shooting na sasa ninapoandika hii wanapakia mizigo yao kwenye gari tayar kwa safari ya kuondoka.

Haya ni matumizi sahihi ya haya magari?

hizi picha nilipiga kwa simu, na sikusogea karibu sana bse nilijua itaniletea dhurumai, lakini mnaweza kuona

Photo0178.jpg Photo0177.jpg Photo0179.jpg
 
Attachments

  • Photo0178.jpg
    Photo0178.jpg
    9.9 KB · Views: 198
Lete picha. Lakini inategemea ni video kwa ajili ya matumizi ya Ofisi husika. There is a need for more investigation on this!!
 
watakua wanarekodi ile move ya kova nyingine si aliambiwa na sugu kua arudi studio?ngoja tusubili labda itaeleweka
 
Du, hii kali! JF tumefikia hatua nzuri sana ya kuripoti live uhalifu ndani ya Jamii.
Kwa namna yoyote kitendo cha kutumia gari la serikali kufanya shooting ya Kwaya si sahihi. Je kuna namna yoyote kwaya ikawa kwa nia ya serikali au taasisi yake?
Natamani sana maafisa waandamizi wa ofisi hii waone ufisadi huu.
 
Weka picha halafu lzm tujue ni kwaya gani coz inawezekana ni wizara ya afya wanatengeneza tangazo la ugonjwa wa usubi. No comment yet.
 
watakua wanarekodi ile move ya kova nyingine si aliambiwa na sugu kua arudi studio?ngoja tusubili labda itaeleweka

Mimi ssidhani kama kuna kosa kuazima gari la selikali,kwani wanakwaya sio wananchi? matumizi mabaya ni kama kwenda kwenye ulevi umalaya nk,lakini kuwezesha wananchi kunadhambi gani hapo.
 
Ni kwaya ya aina gani?. Kuna kwaya za dini na nyingine siyo za dini. Inaweza kuwa kwaya ya shule, polisi, jeshi n.k.
 
labda Nyumba ndogo ya boss inaimba na kwaya hiyo bila shaka..., lakini si naskia serikali ishabinafsishwa? Pengine hayo ndo matumizi yake sahihi.
 
Habari imenikumbusha kipindi cha MIKINGAMO kilicho kua na ujumbe "MIKINGAMO ni sikio la umma tuambie nani yuko wapi na anafanyanini kulihujumu taifa nasi tutasema hewani na kwa wanao husika..."

Umenikumbusha mbali sana mkuu,enzi hizo RTD.
 
Gari ya serikali, Defender yenye usajili STJ 974 iko cocobeach imeleta wanakwaya ku-shoot video, imewaleta imewasubiri wamefanya shooting na sasa ninapoandika hii wanapakia mizigo yao kwenye gari tayar kwa safari ya kuondoka.

Haya ni matumizi sahihi ya haya magari? picha coming soon!

Kumbu kwaya tu!, hujui kwamba zinahubiri amani na upendo na kuasa watu waache maovu, sioni tatizo labda ingekuwa imebeba madumu ya gongo,machangu au magaidi.
 
Lete picha. Lakini inategemea ni video kwa ajili ya matumizi ya Ofisi husika. There is a need for more investigation on this!!

chief mi nilikuweko wakati wanafika na hadi walipoanza kufunga mizigo yao, ilikua ni kwaya ya kanisa, walikua wana-shoot video za nyimbo zao, nimeweka nambari ya gari, wahusika wafatilie watajua, kuanzia saa kumi hadi saa kumi na mbili tarehe 21.July.2012 gari nambari STJ 974 ilikua wapi na nani alikuwa nayo?

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom