Stima au umeme? Lipi na sahihi zaidi?

Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
9,186
2,000
Kama kikitumika Kiswahili neno sahihi ni umeme.

Stima ni lugha chotara yenye kuleta uchochezi
 

KUTATABHETAKULE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,669
2,000
Ni kiswahili Mahalia, yaani kiswahili kinachotumika katika sehemu fulani na kinaeleweka na watu wengi katika sehemu hiyo. Wazanzibari hutamka skuli, watu wa bara wanasema shule. Kwa upande wa visiwani neno hilo limetoholewa toka kwa Waingereza. Huku Bara neno shule limetoholewa toka Kijerumani. Je neno sahihi ni lipi, Skuli au Shule?
 

Salange

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
682
1,000
Kwa muda mrefu mvuke(steam) ulitumika kuzalisha umeme, hivyo kupatikana jina stima. Kuuita stima ni sahihi zaidi kwani asili yake inajulikana. Umeme sijui limetoholewa wapi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom