Stika za fire ni biashara au .....

bobliko

New Member
Dec 2, 2010
2
0
jamani habari zenu wanajamii,
Hivi jamani hizi stika za fire ni kwa ajili ya usalama wa magari au ni biashara?mbona magari ya serikali hayana stika na hayakaguliwi.Haya hayawezi kuungua moto?
Pilli,wiki ya nenda kwa usalama mbona magari ya serikali hayana stika? lakini gari binafsi unaambiwa uweke stika za
Bima,fire,road license,wiki ya nenda kwa usalama.
 
Hizo ni biashara za wakubwa,yapo mengi ya ajabu yanayofanywa hapa Nchini ambayo ukijaaliwa kuyajua yote utakua Kichaa.
 
bado ushuru wa kila tuingiapo kituo cha mafuta, maama serikali sasa inajiendesha kisanii, kila anyefikiria la kwake analipitisha bungeni halafu wanabariki, ili posho zao zipande kwa kila kikao. Ilianza kubadili plate numbe- ikazaa Road license tunayokamuliwa kila mwaka, ikaja fire extinguisher, stika zake bado tutadaiwa stika za triangle na spanner na jeki, ili ukibandika tunajua hivyo vitu unavyo kwenye gari.
Kama sina fire extinguisher, gari likiripuka ni langu halimhusu mtu
 
Acha majungu baba, hebu nunua stika! Wenzio hapo ndo wanapatia hela za safari zisizo kwenye bajet! Kwani stika ikiwekwa kwenye kioo inazuia moto?
 
Maajabu! nyumba ndo zinazoungua kila uchao lakini hawafikirii kuchukua hatua. Labda mmoja, siku moja atazinduka akasema tubandike stika majumbani kuonyesha nyumba ina fire extinguisher.
 
Nilikuwa sijui kuna hii stika! Lakini stika ya nini ilhali tuna fire extinguishers na wanasumbua sana kama hatuna?
Msururu huu hadi unachanganyikiwa hujui unatikiwa kuwa na nini! Windescreen itakuwa imejaa stika!
Hebu tuorodhesheni:
1. Stika ya nenda kwa usalama
2.Stika ya Insurance
3. Road licence
...endeleeeni..
 
Hizi nazo zipo Njiani Kuja
Stika ya Ewura

Stika ya Dawasco

Stika ya Kiyoyozi

Stika ya Seat Belt

Stika ya Parking System

Stika ya Uraia

Stika ya Wilaya unayotoka

Stika ya Chama Unachoshabikia

Hivi ile ya Pick up na Daladala kuandikwa jina la mwenye gari pembeni upande wa kulia mwa gari bado inaendelea?
 
Ni posho ya matrafiki: utakuwa na vyote mwisho atakuuliza wapi stika? Utajisachi na kumwachia chochote siku inatoka hiyo.
 
stika ya fire, ni cheti kuonyesha kuwa mtungi wako wa gesi ya kuzima moto (fire extinquisher) imekaguliwa na upo katika hali nzuri. wahusika wakishakagua (fire extinguisher inspection) na kuridhika kuwa ile gesi (carbon dioxide) ipo katika hali safi, sasa wewe unatakiwa ulipie huo ukaguzi(inspection fee). Ukilipia unatapata risiti na hiyo stika. Na ni muhimu kufanya huo ukaguzi kwa sababu hiyo gas (co2) inaweza kuganda ikikaa kwa muda mrefu bila kutikiswa. Ni muhimu pia kukagua fire extinguisher ili kujua kama pressure yake imepungua chini ya level inayotakiwa. Ni watalaam ndio wanaojua pressure levels ya huo mtungi. Pia wanakagua kuhakikisha kuwa hiyo gesi (amabyo inakuwa katika hali ya poda (powder) haigandi na kutuama chini ya mtungi na ndio maana unashauriwa kutingisha mtungi wako kidogo mara kwa mara. ni muhimu kukagua kama kuna kutu zimeota kwenye nozzle (tundu) ambayo gesi hupitia au kama kuna uharibifu. kwanza kumbuka gesi hiyo ya kuzima moto ni muhimu sana kuwa nayo na inaweza kuokoa maisha yako na wengineo pale moto utakapolipuka. Kwa hiyo suala zima la fire extinquisher na fire stickers linahusu usalama wako. cha msingi pata risiti ya serikali kuhakikisha serikali yetu inapata mapato. .....
 
Back
Top Bottom