Sticky: Weka mipaka katika ndoa yako

Sticky: Weka mipaka katika ndoa yako

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
Unapotembea sehemu mbalimbali utagundua kuwa kila nyumba nzuri yenye thamani imezungushiwa uzio, na uzio unaendana na thamani ya nyumba na vilivyomo. Utakuta nyingine uzio mrefu huwezi hata kuona miti iliyopo ndani na nyingine zipo wazi mtu yeyote anapita na kutoka kama anavyopenda. Vivyo hivyo ukiithamini ndoa yako utaiwekea mipaka, mipaka ambayo hakuna anayeweza kuivuka. Hapa simaanishi kumuwekea mwenzi wako mipaka, bali kuiwekea ndoa yako mipaka. Kila mwanandoa lazima ajiwekee mipaka. Mipaka hii itaiponya ndoa na wale wanaotaka ku tracepass na wewe itakusaidia pia kukulinda.

Wewe umeoa/ kuolewa ni kwanini basi unaruhusu mtu wa jinsia nyingine unayemuita rafiki yako akuzoee hadi kuvuka mipaka? Anakuwa huru kukushika na kukutania utani usiofaa na wewe unachekelea tu? Unakuta wafanyakazi ofisini wanashikana shikana na kutaniana na wapo kwenye ndoa, je huoni kama unaruhusu watu watracepass kwenye ndoa yako? Wengine hata kwenda lunch hawawezi bila dada au kaka fulani na wakati wapo kwenye ndoa.

Unapokuwa online unachat je umejiwekea mipaka? Message zako na jinsi unavyochat na watu umeweka mipaka? Watu wamejikuta wanatoka nje ya ndoa sababu ya ku entertain chat zisizofaa na hadi wanajikuta emotionally connected na mtu asiye mwenzi wake. Unafika nyumbani busy na simu na hata mwenzi wako huna muda naye tena maana tayari kuna mtu umeconnect naye emotionally kupitia simu.

Je ndugu wanaweza ingilia maamuzi yenu na kuyabadilisha bila nyie kuwasiliana? Ni nafasi gani wazazi wanayo kwenye ndoa yenu maana hapa pia panahitaji mipaka. Wazazi ni walezi na washauri lakini wenye maamuzi ni mume na mke.

Weka mipaka kwenye ndoa yako, tena mipaka inayostahili maana ndoa ina thamani kubwa
 
mmmmmh haya....

mipaka isiishie ofisini tu, ifike mpaka kwa marafiki na mashoti zenu, mpaka ka ndugu, sio mnachopanga na mkeo mkaamuliwe na kaka mama baba...

ni hayo tu, ingawa nimetoka nje ya mada kidooooogo!!!!!
 
Mipaka ni muhimu sana haswa kwa marafiki wa karibu.

Marafiki zangu wengi hunishangaa pale wanapotaka kutumia urafiki wetu kimazoea. nadhani huwa wanabaki na maswali mengi sana. kuna wakati naweza kujiweka hata mtu kunsemesha anaona ananibugudhi, na kuna wakati najiweka hata mtu anafikiri hili jamaa hamnazo kabisa.

Nachotaka kusema hapa ni hiki........ Huwezi mwekea mtu mipaka kwa kumwambia, mara nyingi atataka kukujaribu, ishi hiyo mipaka mwenyewe nao watakujua hivyo na wataifuata. Penye kukasirika kasirika, penye kucheka cheka, penye kukemea kemea, penye usiriazi, kuwa siriaz, kuwa mgumu, penye kuonya onya bila kupepesa macho na kikubwa zaidi ni kuzingatia ukweli na hekima. (sio kila saa mtu unajichekesha tu iwe kilioni, iwe umeudhiwa, iwe umetendwa, kila hali wewe ni kukenyua tu au kununa tu...etc)
 
Unapotembea sehemu mbalimbali utagundua kuwa kila nyumba nzuri yenye thamani imezungushiwa uzio, na uzio unaendana na thamani ya nyumba na vilivyomo. Utakuta nyingine uzio mrefu huwezi hata kuona miti iliyopo ndani na nyingine zipo wazi mtu yeyote anapita na kutoka kama anavyopenda. Vivyo hivyo ukiithamini ndoa yako utaiwekea mipaka, mipaka ambayo hakuna anayeweza kuivuka. Hapa simaanishi kumuwekea mwenzi wako mipaka, bali kuiwekea ndoa yako mipaka. Kila mwanandoa lazima ajiwekee mipaka. Mipaka hii itaiponya ndoa na wale wanaotaka ku tracepass na wewe itakusaidia pia kukulinda.

Wewe umeoa/ kuolewa ni kwanini basi unaruhusu mtu wa jinsia nyingine unayemuita rafiki yako akuzoee hadi kuvuka mipaka? Anakuwa huru kukushika na kukutania utani usiofaa na wewe unachekelea tu? Unakuta wafanyakazi ofisini wanashikana shikana na kutaniana na wapo kwenye ndoa, je huoni kama unaruhusu watu watracepass kwenye ndoa yako? Wengine hata kwenda lunch hawawezi bila dada au kaka fulani na wakati wapo kwenye ndoa.

Unapokuwa online unachat je umejiwekea mipaka? Message zako na jinsi unavyochat na watu umeweka mipaka? Watu wamejikuta wanatoka nje ya ndoa sababu ya ku entertain chat zisizofaa na hadi wanajikuta emotionally connected na mtu asiye mwenzi wake. Unafika nyumbani busy na simu na hata mwenzi wako huna muda naye tena maana tayari kuna mtu umeconnect naye emotionally kupitia simu.

Je ndugu wanaweza ingilia maamuzi yenu na kuyabadilisha bila nyie kuwasiliana? Ni nafasi gani wazazi wanayo kwenye ndoa yenu maana hapa pia panahitaji mipaka. Wazazi ni walezi na washauri lakini wenye maamuzi ni mume na mke.

Weka mipaka kwenye ndoa yako, tena mipaka inayostahili maana ndoa ina thamani kubwa

Ni somo zuri sana...kwa kweli na si kwa wanandoa tuu...hata kwa wale ambao wapo kwenye serious relationship....ni vyema kujitambua...na kujijengea mahusiano ambayo unapenda na kuyafurahia. Vijana wengi sana wanaathiliwa sana na mitandao..wanajisahau na kuishia kutumiana tuu. Mipaka hata kwenye maisha ya kawaida si makosa. Marafiki wawepo ila tuu wajitambue na kukuheshimu. Ni hayo tuu.
 
Sijui kama watakuelewa...bravo!!!
 
images

images
Kwa kuongezea tu; weka mipaka ya kimaadili, mavazi ya stara kupunguza vishawishi.....
N
images
 
Ni kweli mkuu uliyoongea mipaka inasaidia sana katika mahusiano,bila mipaka utapigiwa usiku wa manane simu na rafiki yako wa kike huku umelala na mkeo halaf anakuambia amemiss kupiga stori na ww bila shaka hapatalalika tena!
 
Kuweka "fence na grilles" imara ni sawa kwa ulinzi wa "nyumba" yako.

Lakini "fence na grilles" hizo zisipowekwa kwa namna inayofaa zinaweza kukuzuia pia kujiokoa kama likitokea la kutokea humo ndani (say moto etc) au kuwazuia hata ambao wangeweza kuingia kuja kukusaidia kama umepatwa na matatizo humo ndani!

So, weka hizo "fence na grilles" intelligently na uache pa kutokea au namna ya kupata msaada - just in case you have to!

Mbarikiwe sana.
 
Ni kweli mkuu uliyoongea mipaka inasaidia sana katika mahusiano,bila mipaka utapigiwa usiku wa manane simu na rafiki yako wa kike huku umelala na mkeo halaf anakuambia amemiss kupiga stori na ww bila shaka hapatalalika tena!
na hiyo inakuwa mbaya sana
 
Mkuu asante sana kwa kutukumbusha ni kweli mipaka ni jambo muhimu nakumbuka ndoa flani ilikua na mgogoro kisa mke anamwita jamaa flani mchumba. Mume wa yule mama hakuifurahia hali ile lkn mke alikua kama kaweka nta masikioni. Ilipelekea kutokua na mahusiano mazuri kati yao. Sasa basi utani mwingine tuwe waangalifu na hasa tuheshimu hisia za wenzetu. Ndoa kiuhalisia ina thamani kubwa na wanandoa wakiweza kutambua hili basi hapatakua na migogoro ya kila mara. Utani kama vile huko maofisini kuitana husband, wife, n.k utani huu waweza kuamsha hisia flani kwa wahusika.
 
Ni kweli mkuu uliyoongea mipaka inasaidia sana katika mahusiano,bila mipaka utapigiwa usiku wa manane simu na rafiki yako wa kike huku umelala na mkeo halaf anakuambia amemiss kupiga stori na ww bila shaka hapatalalika tena!

Mekumisoooo
 
Back
Top Bottom