Cynic
JF-Expert Member
- Jan 5, 2009
- 5,144
- 1,658
Hawa watawala ni wazuri kweli katika kubuni kero. Unatoka na gari lenye sticker safi ya insurance na road licence (ambazo kila mtu anajua zinachangia ktk pato la taifa). Halafu unasimamishwa na traffic police kwamba huna sticker ya usalama barabarani (zinazofadhiliwa na kampuni la simu) na sticker ya fire extinguisher (fire extinguishers zinapatikana kwa wafanyabiashara fulani). Tutafika namna hii? Ukiwauliza watu, kila mtu anakushangaa. Ila hii Sticker ya Fire Extinguisher ni mpya kabisa (imebuniwa mwaka huu). Yote kwa yote, huku ni kusababisha usumbufu usio wa lazima na pia kutengeneza mianya mipya ya rushwa.